Header Ads

Mambo ya Shule

Jamaa kaingia chuo katikati ya simesta
kaishiwa akamuandikia baba yake barua.
‘Chuoni mambo mazuri sana, kuna
maajabu hapa maprofesa hapa
wamegundua njia ya kufundisha mbwa
kuongea, mlete Bobi na shilingi laki 5,
baada ya muda atakuwa anaweza
kuongea. Mzee wa watu haraka akatuma
mkwanja na mbwa, haikuchukua muda
mkwanja ukaisha. Denti akamtumia baba
yake barua nyingine kuwa wameboresha
program sasa wanaweza kumfundisha
mbwa kusoma, mzee aongeze kimilioni
tu. Mzee wa watu aliyekuwa tayari
anajisifu kijiji kizima akauza ng’ombe
akatuma mkwanja. Likizo ikafika Denti
akabaki anawaza anaenda kumwambia nini
baba yake. Alipofika tu baba yake
akamuulizia Bobi wake. Denti akamuita
baba yake pembeni,’ Baba hili
nitakalokwambia sitaki mama asikie’. Baba
akauliza,’Vipi tena?’. Denti akaanza,’
Jumapili iliyopita tumeamka vizuri na
Bobi, yeye kama kawaida yake akaenda
kuchukua gazeti la Mzalendo na kukaa
kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla
wakati anasoma akaniita akanambia hivi
baba yako bado anaendelea na kale
kachangudoa ka pale mtaa wa pili?
Nilishtuka’. Baba akaingilia
kati,’Ungemuua hapo hapo mbwa mshenzi
huyu anataka kuniharibia mambo yangu?’,
Denti akajibu,’Baba na mimi lilinijia wazo
hilohilo sikumchelewesha nikamtwanga
nyundo ya kichwa’. Baba akamsifu
mwanae’Safi sana safi sana mwanangu’

No comments

Powered by Blogger.