HAYA NDIO MAZOEZI YA KUUFANYA UKE KUA MDOGO NA KUBANA..[KEGEL EXERCISE]
Sababu
nyingi sana zinaweza kuchangia kupungua kwa nguvu za misuli ya uke na
na tumbo la chini kwa ujumla ikiwemo ujauzito, umri mkubwa, kuzaa
watoto, upasuaji na kua na uzito mkubwa.
Mazoezi ya kegel husaidia kukaza misuli inayoshikilia viungo vya chini
ya tumbo ikiwemo mfuko wa uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo na uke..
Wanawake wengi ambao wana misuli iliyolegea hawafiki kileleni kirahisi
wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine huhitaji uume mnene ili
kusugua mishipa yao ya fahamu ya uke kirahisi na kufika kileleni kuliko
wanaofanya mazoezi haya. Lakini pia mzazoezi haya husaidia kuzuia mkojo
kutoka wakati wa kucheka, kushindwa kuzuia mkojo ukibana na kushindwa
kuzuia choo kubwa ikebana..
Elimu ya afya ya nchi ambazo hazijaendelea kama Tanzania hujali zaidi kutibu na kuzuia magonjwa ila sio matatizo kama haya..
Hivyo kama mwanamke una tatizo hili au
mwenzako ana tatizo hili twende pamoja ili uweze kurudi kwenye maisha
yako bora ya zamani ulipokua mbichi..
Jinsi ya kufanya mazoezi haya….
Tafuta msuli sahihi…
Kuufahamu msuli wa kuufanyia mazoezi nenda chooni kukojoa alafu katikati
ya kukojoa zuia mkojo. Ukifanikiwa huo ndio msuli sahihi..
Fanya mazoezi sasa….
Baada ya hapo malizia mkojo wako kisha nenda kitandani..lala kwa mgongo
kaza msuli uleule uliokaza wakati wa kuzuia mkojo. Kaza msuli kwa
sekunde kumi kisha legeza kwa sekunde kumi.
Kua makini….
Kwa matokeo mazuri kaza msuli huo tu, usikaze misuli ya tumbo, mapaja au
makalio. Usibane pumzi pumua tu kawaida wakati wa zoezi hili.
Fanya mara tatu kwa siku..
Kaza na kuachia msuli huo mara kumi asubuhi, vivo hivyo mchana na
jioni.. lakini pia unaweza kukaza msuli huo popote ulipo ata kama hakuna
sehemu ya kulala kwa mgongo. Kwenye foleni ya benki, kwenye gari, ukiwa
ofisini kwani hakuna mtu atakayegundua unafanya nini..
Mwisho: mambo yote ninayo ongelea
kwenye hii blog yanawezekana tu iwapo mtu ana bidii ya kufanya kitu
husika. Usifanye kitu kwa wiki moja ukategemea mabadiliko yeyote. Kila
kitu kinahitaji bidii kupatikana katika maisha ya binadamu.
Post a Comment