Header Ads

Mchachuko sehemu ya 21

MCHACHUKO….(21)
MTUNZI…EMMANUEL F. KWAY
AGE..(18+)

ILIPOISHIA
Aliuliza Kimti huku akichungulia nje ila Adrian hakujibu na kunyoosha mpaka ndani na kujitupa juu ya sofa akiwa hana raha hata kidogo,
Hakukaa sana alihisi geti lina pigwa kwa nguvu sana tena kwa fujo nyingi na kufanya hofu izidi kumtanda sana huku akitafuta njia ya kutokea.

SONGA NAYO.
“tajiri kuna watu getini wana kuhitaji”
“wakina nani?”
“mimi sijawajui”
“sasa huwajui si ukawaulize”
Kimti alichomoka mbio mpaka getini kisha baadae kurudi ndani mpaka kwa Adrian.
“wanasema wametoka mbeya Mmoja anaitwa Mzee… Mzee..”
Kimti alivuta kumbukumbu na jina kumpotea kichwani
“Mzee nani?”
“jina limenitoka subiri kidogo tajiri”

Kimti alitoka tena nje na kwenda getini na kurudi mpaka seblen kwa Adrian na kutoa jibu kamili, Adrian aliruka kitini kama mkuki baada ya kusikia jina la Baba yake mzazi kuwa yupo getini,
aliweka kila kitu sawa na  kwenda mpaka getini akitembea haraka haraka.
“shikamoo Mzee!”
Alisalimia Adrian kwa adabu zote huku mikono yake ikiwa nyuma kisha kumsalimia MAMA yake na msichana mwingine aliyekua kati kati yao!
“yaani muda wote tuna gonga kumbe upo ndani umekalisha izo korodani zako!”
Alifoka Mzee Mwangenya baba mzazi wa Adrian alikua ni mwingi wa maneno mengi sana,lakini Adrian alishamzoea tayari hakua na tatizo na Baba yake,
walikaribishwa mpaka ndani na moja kwa moja Adrian kuleta glass ya juice na kuwapa wazazi wake nayeye  kuketi pembeni ya sofa na kuzungumza mambo mengi ya kijijni Mbeya, hawakuelewa kuwa Adrian akili yake haipo hapo kabisa alikua akimuwaza Fiona aliyekatwa katwa mapanga mbele yake.
“Sasa mwanangu Adrian, muda mwingi sana tulikua tuna kwambia uowe naona umeshindwa sijui una tatizo gani una mali nyingi, mimi na mama yako tume kaa chini na kuamua kukuletea mwanamke uwe  una ishi nae huyu hapo anaitwa Sikuzani, ni mtoto wa mzee Jumanne Mwapalala, ni msichana kigoli atakufaa”
Alizungumza Mzee Mwangenya baba mzazi wa Adrian
“jamani wazazi wangu, mimi mbona nina mchumba tayari na nilitaka nije nae mwezi ujao”
Alijetetea Adrian baada ya kumuangalia sikuzani
“hapana hapana hapana, sisi hatujui hilo huyu ndio tuna mjua sisi hapa”
Maneno hayo yalimfanya Adrian amthaminishe msichana huyo aliye kua mbele yake akiwa ameshika malapa mikononi mwake ameji funga kanga iliyotoboka huku akiwa amepakata mfuko wa Rambo mikononi mwake akitizama tizama huku na kule, alipiga chini jicho lake na kuona gagulo jeusi lililotokeza chini ya kanga.
Na kushindwa kuelewa nini akifanye aliwaheshimu sana wazazi wake lakini kwa kitendo cha kumletea mwanamke au kumchagulia mtu wa kuoa kilikua bado hakijamuingia kichwani mwake.
“lakini Mzee nimesha kwambia nina mchumba tayari,”
“funga mdomo sisi wazee wako tumeona mbali sana tumeona mbali, sisi tume kuzaa wewe hapo, sisi ni wa kwanza kuliona jua, huyu ndiye sisi tuna mtambua na tuna taka ufunge nae ndoa”
Katika siku ambazo zilikua ndefu kwake ilikua ni siku iyo ya Jumanne alikumbuka wasichana wengi masista duu ambao ana tembea nao waliojua kuvaa mjini, leo hii akatoke na mwanamke kutoka shamba tena amesuka mistari kichwani amepauka.
Hakua na chaguo lingine zaidi ya kukubali ili kuwaridhisha wazazi wake waliomzaa,
Walikaa kwa mtoto wao hapo siku mbili na siku ya tatu kurudi zao Mkoani Mbeya  wakiwaachia Baraka tele watoto wao Adrian na sikuzani.

“Mpenzi!”
Aliita sikuzani usiku huo baada ya kutoka chumbani mpaka sebleni na kumkuta Adrian akiwa anaangalia t.v
“umeniitaje?”
“Mpenzi”
“koma ishia hapo hapo, tena ukome na ukomazike Mimi sio mpenzi wako, pale nili waheshimu tu wazee, ila ki ukweli wala sikupendi na kile chumba tulichokua tunalala uhame leo hii, umenisikia binti”
“ndio”
“sio ndio! uhame,”
Alizidi kufoka Adrian huku akimuangalia sikuzani ambaye alikua amevalia Jins usiku huo wakati wa kulala.
***
“Nasra karibu sana!”
“Ahsante Adrian”
“siku nyingi sija kutia machoni”
“nilikua safarini nilikua mkoa vipi lakini, nilikua siku pati kwenye simu”
“matatizo tu, nitakupa namba zangu nyingine”
“Any way nisha lipa nusu ya marejesho ya pesa zile, wiki ijayo namalizia malipo thanks Adri, kama una mda jioni leo twende nika kupe shukrani tukae tunywe tufurahi sote”
“hakuna tabu Nasra”
Yalikua ni maongezi ya Adrian pamoja na Nasra ndani ya ofisi ya Adrian akizidi kumthaminisha malaika aliyekua mbele yake akiongea kwa mapozi yote na midomo yake iliyokua myekundu iliyojaa lip shaini ya rangi ya papo ikimechisha na topu aliyovaa huku jicho likiwa limejaa mascala na kumfanya awe kama mdoli,
“okay sawa ngoja niwahi nita kutafuta”
Aliaga Nasra na kumuachia Adrian nyuma lawama hasa alipokua akitingisha singida Dodoma na kufungua mlango.
baada ya dakika mbili watu wawili waliovalia jezi za polisi waliingia mpaka ofisini kwake na kumfanya Adrian aanze kutetemeka kwa hofu. Tukio la Fiona ndilo lililo mjia hapo hapo.
“habari yako Mr. Adrian?”
Alisalimia askari mmoja na kuketi
“nzuri tu”
“una mfahamu Fiona?”
“ndio namfahamu”
“una mahusiano nae gani?”
“ni mpenzi wangu”
“sawa, nafikiri unajua kilichotokea?”
“ndio nafahamu”
“pole sana, sasa ulikua una hitajika mahakamani wiki ijayo tume kuletea barua hii hapa”
“ahsante nitakuja”
“pole sana”
Majibu aliyokua akiwajibu ki ujasiri wenda ndio yaliyofanya maaskari wale wasiendelee kumuuliza tena maswali mengine sababu walijua hana hatia kabisa.
Baadae jioni kufika alipokea simu kutoka kwa Nasra na kumuomba wakutane Kilimanjaro hotel iliyokua mitaa ya  bara bara ya OHIO posta hapo ndio alipokua,
Aliwasha gari na kumfuata mpaka alipo na mwanamke huyo kuingia ndani ya gari lake.
“sasa tunaenda wapi?”
Alihoji Adrian
“sema wewe”
“sasa mimi nitajua mfuko wako upoje?”
“sema popote pale”
“twende kwetu pazuri tabata”
“poa”
Adrian aliangalia site mirror baada ya kuona hakuna gari upande wake aliingia barabarani na safari ya kwenda tabata kwenye baa hio mpya kuanza.
njiani alijaribu kuongea mambo mengi akimuuliza maswali ya hapa na pale Nasra juu ya maisha yake na nini anafanya mjini.
Baada ya kufika kwetu pazuri waliagiza vinywaji huku wakiendelea kusikiliza nyimbo na kuwaona watu wakicheza,palikua pamechangamka sana,
Waliendelea kunywa pombe nyingi na Nasra kuonekana amezidiwa sana akilala mika apelekwe kwake.
“unaishi waaaaapi?”
“siiiijui”
Adrian alikua ana mtihani mgumu sana hakuelewa nini akifanye alifikiria sana na kuangalia saa yake ambayo ilikua ime timu saa nane ya usiku,
ilikua ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu lazima achemshwe na kuliwa, alimshika Nasra kiuno na kupepesuka mpaka ndani ya gari.
Hakua na chaguo lingine zaidi ya kurudi nyumbani kwake akiwa na Nasra lakini aliwaza sana baada ya kukumbuka kuna kidudu mtu anaitwa sikuzani nyumbani kwake.
Hakujali aliendelea kuendesha gari na baadae kufika kwake ambapo alifunguliwa geti .alimshusha Nasra ambaye alikua hajielewi kwa pombe alizokunywa nyingi kuzidi kipimo!.
Msobe msobe mpaka ndani na kumkuta Sikuzani yupo seblen amekaa
“Mpenzi ume toka wapi?”
“nilikwaaambia nini?”
“na huyo nani?”
“wewe huyu hakuhusu funga bakuli”
Alisema Adrian huku akipepesuka kidogo.
“hapa hamuendi popote pale, mimi ndiye mke wako”
Alifoka Sikuzani na kutanda mbele ya Adrian bila kujua kuwa mwanaume huyo ana mkono mwepesi sana na mwenye hasira za karibu.
Kama kawaida Adrian alitabasamu huku hasira ziki mpanda taratibu.
Sasa unaweza kusoma simulizi za mtunzi kway inst @storyzakway

ITAENDELEA.................
(kwa stori nyingi tembelea hii link www.facebook.com/

No comments

Powered by Blogger.