Header Ads

Ufahamu Ugonjwa wa Pangusa,dalili zake, na Tiba yake

PANGUSA

pangusa ni nini?
Huu ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa njia ya ngono, huambukizwa na bakteria anayefahamika kitaalamu kama haimophilus ducrey.
Bacteria huweza kupita kwenye ngozi laini kama ya uke kirahisi bila hata kuwepo kwa michubuko.
Wanawake huweza kuhifadhi bacteria hawa bila kuonyesha dalili yeyote na kuwaambukiza waanaume wengi zaidi.
ugonjwa huu huleta vidonda vikubwa sana kwenye sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo, huweza kuzimaliza kabisa sehemu za siri kama matibabu yasipopatikana.
Ugonjwa huu hupatikana kwenye sehemu za joto na wagonjwa wengi ni wanawake wanaojiuza hasa sehemu za mijini.
ugonjwa huu hurahisisha zaidi maambukizi ya virusi kwa ukimwi kwa waathirika wa ugonjwa huu.
Baada ya kuambukizwa mgonjwa huchukua siku 3 mpaka 14 kuanza kuonyesha dalili.

Dalili za ugonjwa wa wa pangusa..
~Baada ya maambukizi vipele hutokea kisha huchimbika na kutoa vidonda vikubwa ambavyo husambaa pande mbalimbali za sehemu za siri na kuchimba mashimo ya vidonda.
~Vidonda hivi hua na maumivu makali na hutoa damu pale vinapoguswa.
hali hua mbaya zaidi kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi.
~Kutokwa na majimaji ukeni yanayoambatana na Maumivu makali ya sehemu za Siri
              
Vipimo vinavyofanyika
Daktari mzoefu anaweza akagundua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini kwa uhakika zaidi majimaji yanayotoka sehemu za siri huchukuliwa na kupimwa maabara.

Matibabu
Vidonda vinatakiwa viweke visafi, vioshwe na sabuni mara kwa mara
dawa zinazotumika kutibu shida hii ni kama:

Azithromycin - 1 g Vidonge (PO) kama dozi au
Ceftriaxone - 250 mg kwa njia ya Sindano Kama dozi
Erythromycin base - 500 mg PO Kila baada ya Masaa 8 kwa muda wa siku 7 au
Ciprofloxacin - 500 mg PO Mara mbili kwa siku au Kila baada ya Masaa 12 kwa muda wa siku 3

Azithromycin na ceftriaxone Kama dozi zimeonyesha Mafanikio katika matibabu

Ceftriaxone ni chaguo kwa matibu kwa mama mjamzito , ingawa ciprofloxacin imeonyesha kutoa madhara machache kwa mtoto akiwa tumboni kwa mama na mama anayenyonyesha

Wapenzi wenye maambukizi ya Pangusa au chancroid Inabidi wachunguzwe Isu kupimwa na kutibiwa kulingana na dalili ambazo huanza kujitokeza au kujionyesha Dani ya sku10 .

Jinsi ya kuzuia
~Matumizi ya kondom kwa usahihi.
~Kua na mpenzi mmoja muaminifu.
~Usishiriki ngono kabisa kama huwezi kutumia kondomu.
~Epuka wapenzi wengi.

4 comments:

  1. Replies
    1. Hellow doctor, nimeona post yako kwa u tube naomba kuuliza hizi dawa azithromycin, ceftriaxone na erythromycin natumia zote kwa pamoja kamadozi au mojawapo kama dozi plz

      Delete
  2. Hellow doctor, nimeona post yako kwa u tube naomba kuuliza hizi dawa azithromycin, ceftriaxone na erythromycin natumia zote kwa pamoja kamadozi au mojawapo kama dozi plz

    ReplyDelete

Powered by Blogger.