Header Ads

YAFAHAMU GROUP YA DAMU NA TABIA ZAKE*

YAFAHAMU GROUP YA DAMU NA TABIA ZAKE*


*GROUP A*

Hawa tunaweza kuwaita ni vegetarians wanahitaji sana mananasi na zabibu kwa wingi.
Watu wenye damu ya kundi hili Mara nyingi ni wale watu ambao tunaweza kusema hawaambiliki yaani wakiamua kitu wameamua mpaka wakitekeleze hata kama ni kibaya.

Tunaweza tukasema pia ni watu ambao ni wabishi sana au wabishani na hawakubali kushindwa hivi hivi.
Watu Wa kundi hili pia huwa wana changamoto ya kuwa na upungufu Wa acid mwilini hivyo huandamwa na vidonda vya tumbo.
Ni watu ambao hushambuliwa sana na saratani za mishipa ya fahamu,utumbo,mifuko ya mayai,mfuko wa kizazi na mlango wa uzazi kwa wanawake,kibofu cha mkojo,figo,kongosho na tezi za mate ya kinywa na na mate ya umio.

Wana hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya Moyo,kupata lehemu mbaya mwilini,kwenye Moyo,wako hatarini pia kupata kiharusi na ugonjwa Wa shinikizo la damu Wa Moyo.

Vyakula wanavyotakiwa kula kwa wingi ni mbogamboga za Majani na nyama nyeupe nyama nyekundu sio nzuri sana kwa watu hawa.
Hawatakiwi kugusa kabisa au kutumia Mara kwa Mara vyakula hivi :-nyama nyekundu,ngano,machungwa (vitamini C),na maziwa.
Wakila ndizi,maembe na mapapai huwasababishia waamkapo asubuhi kutokwa na makamasi kwa wingi.
Hawatakiwi kugusa kabisa acidic food kama machungwa na jamii yake.

Watu Wa kundi hili wanapenda sana wali na Mara nyingi ndio Chakula chao kikuu.
Hawatakiwi kugusa kabisa ngano na mahindi na endapo wakatumia vyakula hivi hasa kwa wanawake huwasababishia kupata hedhi Mara mbili kwa mwezi.

Tabia zao ni hizi hapa:-
👉🏿ni watu Wa gharama sana hasa wadada au wanawake.
👉🏿huishiwa au wanakuwa na upungufu Wa damu sana.
👉🏿ni wavivu nikiwa na maana hawawezi Nazi ngumu ngumu.
👉🏿sio waongo au wadanganyifu,ni wakweli (they don't like cheating)
👉🏿ni wasirisiri sana.
👉🏿ni waoga sana.
👉🏿wanapenda kujifichajificha kama ni usiku hupenda kukaa gizani sana.
👉🏿ni waaminifu sana na hapa Mara nyingi unawakuta Maafisa utumishi kwani hufuata sheria.

Ni watu ambao pia hawaumwi Mara kwa Mara.

*GROUP B*

Hili ni kundi la watu ambao ni wazungumzaji yaani ukiwapa nafasi ya kuzungumza ni kama vile umekosea na hapa Mara nyingi unawapata watu kama MCs.

Ni watu ambao wana tabia zilizojitosheleza yaan wamekamilika.

Ni watu ambao husumbuliwa sana au wako hatarini kupata magonjwa kama uvimbe Wa fizi,na pia wanawake walioko katika kundi hili wako hatarini kupata ugonjwa Wa kisukari aina ya pili.

Watu Wa kundi hili hawashauriwi sana kula vyakula vya aina ya kuku,Karanga,korosho,na nyanya.

Ni watu ambao wakipata wakipata maambukizi ya virusi vya aina yoyote ile huwa machizi au vichaa kutokana na kwamba vinaenda kuharibu mfumo wake Wa fahamu....Mara nyingi wao wenyewe tu hawapendi kuku ingawa hawaruhusiwi kula.

*GROUP AB*

Hawa ni watu ambao Mara nyingi hawaeleweki yaani wana tabia za A na pia tabia za B wakati mwingine.

Ni watu ambao wanaweza akaanzisha kitu asikimalizie ukakuta kaishia katikati halafu kaanzisha kingine.
Ni watu ambao wako hatarini kuyapata magonjwa kama kiharusi,dengue,magonjwa ya Moyo,shinikizo la Moyo,na lehemu kujaa kwenye mishipa ya damu.

Watu Wa kundi hili Mara nyingi wakifikia uzeeni uwezo wao Wa kufikiri hupungua kwa haraka.Lakini Mara nyingi kupungua kwa uwezo Wa kufikiri hutokana na magonjwa kama shinikizo la Moyo,kisukari na lehemu kuwa nyingi sana mwilini.

AB ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana Wa kukabiliana na magonjwa yaani kinga yao ya mwili ni imara ukifananisha na makundi mengine yote ya damu

*GROUP O*

Hawa ni watu ambao ni jeuri na kiburi na wanajiamini sana.

Ni watu ambao ni wababe,wagumu,wenye ubinafsi na wanafanya maamuzi yao pale wanapoamua na sio kulazimishwa.

Ni watu ambao wanakuwaga na roho nzuri sana ila hawapendagi uongo hivyo usije ukajaribu kuwadanganya hata siku moja.

Ni watu ambao ni rahisi sana kupata shambulio la ghafla la Moyo,hawana kinga ya kutosha ya kipindupindu,wana kinga kiasi ya TB na malaria isiyo Kali,wako hatarini kupata saratani za kongosho,tumbo,matiti na mlango Wa kizazi,magonjwa ya maambukizi ya ngozi,na vidonda vya tumbo.
Wanapata sana maumivu ya kiuno,magoti pamoja na mgongo.

Ni watu wasiopenda vitu vichachu kutokana na uwepo Wa acid kwa wingi mwilini mwao hivyo wanasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo na huwa wanasumbuliwa sana na tatizo la choo (constipation) pamoja na kisukari.

Hawatakiwi kula ngano na mahindi Mara kwa Mara au kutokula kabisa.
Hawapaswi kabisa kugusa au kula machungwa,passions,ukwaju,maembe mabichi nk na vyote vyenye acid.
Hawatakiwi kabisa kula ugali au wali,mahindi ya kuchoma au kukaanga au kupika hayawafai kabisa.

Wanaume walioko katika kundi hili wanahitaji protein kwa wingi kuliko wanawake kutokana na kuhitaji nguvu kwa sana katika shughuli zao na miili yao kwa ujumla.

Kundi hili pia hutokewa na mvi za mapema sana.
Kwa wanaume hapa ndipo unawakuta ambao wana mapaja yasiyolingana yaan moja kubwa lingine Dogo.
Kwa wanaume wanatakiwa kula matunda sana kama maembe,mananasi,ndizi,matikiti maji (ule na mbegu zake) hapa pia kama ni tunda unakula lote mfano nanasi unalimaliza,papai unalimaliza,na pia matunda ya rangi moja kula kwa pamoja.
Ukitengeneza kitu kama juice ya matunda unywe yote kwa wakati huo na sio kutengeneza ya wiki au siku kadhaa.
Wanapenda sana kula nyama yenyewe hasa ya mbuzi ya kuchoma

Vyakula vinavyowasaidia au wanavyohitaji sana mwilini ni matunda matunda,mboga mboga za Majani,protein kwa wingi yaani nyama,maharage,mayai na maziwa.

*NB:Ndizi zinasaidia sana kurudisha kumbukumbu na kuimarisha ubongo hivyo kuimarisha Akili*

Watu Wa group A na B wana uwezo mkubwa sana Wa kukabiliana na ugonjwa Wa kipindupindu ila AB ni zaidi.
Utafiti pia umeonyesha group O kwa wanawake wana uwezo mdogo Wa kutunga mimba na pia wana mayai kidogo yasiyokuwa na afya njema hivyo kupelekea kushindwa kutungisha mimba hivyo kwa wanawake Wa kundi hili ni muda muafaka Wa kuweza kujitahidi kuzaa mapema ili kuondoa uwezekano Wa kuja kukosa mtoto hapo baadae

No comments

Powered by Blogger.