Header Ads

BBC


Kampuni ya Dangote yawafuta wafanyikazi kwako

Image captionAliko Dangote,mtu tajiri zaidi barani Afrika

Mfumuko nchini Nigeria huenda umeathiri kampuni ya Dangote Group inayomilikiwa na mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote.

Kampuni hiyo imeripotiwa kuwafuta kazi wafanyikazi 48 wakiwemo wataalam 36 wa kigeni na raia 12 wa Nigeria.

Ripoti zinasema kuwa hatua hiyo inatokana na gharama ya juu ya kufanya biashara katika taifa hilo na kampuni hiyo imeshindwa kupata fedha za kigeni kuwalipa wafanyikazi hao wa kigeni.

Lakini msemaji wa Dangote Group Tony Chiejina aliambia BBC kwamba ufutaji huo hauna uhusiano na mfumuko.

Kampuni hiyo inasema kuwa ilikuwa inaimarisha biashara zake na kwamba kazi zengine zimechukuliwa na kampuni tanzu.

Kampuni ya Dangote Group ni miongoni mwa kampuni zilizo na wafanyikazi wengi katika sekta hiyo.

Miezi miwili iliopita ,kitengo cha habari cha Bloomberg kiliripoti kwamba bwana Dangote alipoteza dola bilioni 5.4 mwaka huu kutokana na kuanguka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria ,Naira.

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

FacebookMessengerTwitterWhatsApp

Rejea mwanzo wa ukurasa

Swahili navigation

Uongozaji BBC

SportWeatherRadio

Masharti ya matumiziKuhusu BBCSera ya FaraghaCookiesAccessibility HelpParental GuidanceWasiliana na BBCCopyright © 2016 BBC. BBC Haiwajibiki kwa taarifa kutoka tovuti zisizo zake. Muongozo wetu kuhusu na juu ya wavuti za nje

No comments

Powered by Blogger.