Header Ads

Cheka uongeze siku

CHEKA UONGEZE SIKU ILIVYOKUWA SIKU YA KUTAHINIWA HAWA JAMAA.
"Mwerevu na Mjinga walienda ktk usaili, walipofika
kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Mwerevu
kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote
wapate kazi. Basi Mwerevu akaingia na maswali
yakawa hivi:-
Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?
Mwerevu:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila
ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu
mbalimbali..
Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa
Uhuru huo?
Mwelevu:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl.
J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.
Msaili:- Inasemekana ktk sayari ya Mars
kunaviumbe wanaishi, je ni kweli?
Mwerevu:- Watu wengi wanasema hivyo lakini
haijathibitishwa na wanasayansi.
Baada ya Mwerevu kutoka basi Mjinga akapewa
majibu yote..
Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-
Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwka gani?
Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa
mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu
mbali mbali.
Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?
Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J.
K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia .
Msaili:- Hivi wewe ni chizi?
Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini
haijathibitishwa na wanasayansi.""

No comments

Powered by Blogger.