Header Ads

Ugonjwa wa jongo (Gout)

Maumivu ya jongo (Gout):
Gauti (Gout ) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid ) katika damu.

     Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili).
    Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout ) au ikawa sugu (chronic gout) . Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri maungio (joint) zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

Visababishi
Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha
uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.
Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi (risk factors)
      Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.
Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti

Ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari,
Magonjwa ya figo,
Unene uliopitiliza,
Ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).
Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na
Matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

Dalili
      Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha.          jointi moja au joint chache.
      Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa cha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
      Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
       Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
       Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
       Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.
Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis ) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo
Vipimo vya gauti hujumuisha
Kiwango cha uric acid katika damu.
     Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
     Kiwango cha uric acid katika mkojo
     Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
X ray ya jointi iliyoathirika
      Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)

Matibabu
Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumo wa maisha wa mgonjwa.
Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na
Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol
Dawa za kutuliza mcharuko mwili (nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs ) kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac n.k. Pia ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda vya tumbo au mzio.
Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili (inflammation). Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye jointi iliyoathirika kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe. Kwa kawaida maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa angalau 48.
Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku. Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulia makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu (trophy) au wagonjwa wenye vijiwe vya uric katika figo.
Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:
            Kuacha kunywa pombe
            Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
           Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
          Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
          Kula kiasi kikubwa cha wanga
Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo

     Matarajio
Wagonjwa wanaofuata masharti na ushauri wa daktari huweza kuishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, ni vema kufahamu kuwa mara nyingi gauti ya ghafla hatimaye huwa gauti sugu.

Madhara ya gauti
Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
Vijiwe katika figo
Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo

Kinga
     Kwa kawaida gauti haizuiliki, hata hivyo mgonjwa anashauriwa sana kujiepusha na vitu vinavyoweza kuchochea shambulizi na dalili za ugonjwa huu

Tiba mbadala ya gaut

Juisi ya limau

Juisi ya Limau ina viinilishe vya asili ambavyo vinaweza kusaidia kutibu maumivu ya jongo au gout kama tulivyozoea wengi wetu. Tafiti zinaonyesha kuwa matunda jamii ya chungwa kama vile machungwa yenyewe, machenza, na limau au ndimu husaidia kuyeyusha asidiiliyogandamana katika damu na hivyo kukupatia nafuu ya haraka itokanayo na maumivu ya gout. Tengeneza juisi hii ya limauukichanganya na maji na unywe mara tatu kwa siku kwa majuma kadhaa.

2. Siki ya tufaha

Kwakuwa tunda la tufaha ni zuri katika kudhibiti gout hakuna shaka kwamba siki yake isiweze kudhibiti gout. Na kwa kawaida siki ya tufaha inafanya vizuri kutibu gout kuliko hata tunda lake. Siki ya tufaha ina asidi nzuri iitwayoacetic acid ambayo huongeza kiasi cha alkalinindani ya mwili na kuunda usawa na mazingira mazuri ya pH (Potential Hydrogen) na hivyo moja kwa moja kuwa msaada mkubwa katika kupunguza na hata kutibu maumivu ya gout. Kumbuka pia hakuna utafiti ambao umefanywa kuthibitisha madai haya ya siki ya tufaha kuwa na uwezo huu. Unaweza kuchanganya siki ya tufaha katika chakula unachokula au kuongeza kijiko kikubwa kimoja katika glasi ya maji na unywe mara moja kila siku.

3. Baking Soda

Baking soda ina faida nyingi na matumizi mengi sana ikiwemo kukusaidia katika tatizo lako la gout. Sodium bicarbonate iliyomo kwenye baking soda huifanya damu kuwa na alkalini zaidi kitu ambacho ni mhimu katika kudhibiti gout. Chota kijiko kimoja kidogo cha baking soda na uiweke katika maji robo lita na unywe kutwa mara mbili kwa majuma kadhaa. Kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu usiitumie hii baking soda kujitibu gout.

4.  Nanasi

Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation). Kwahiyo kuwa na mazoea ya kula nanasi kila siku kunaweza kuzuia usipatwe au hata kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

5. Zabibu

Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout kwa haraka zaidi. Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho pycnogenols ambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout. Kula kila siku zabibu na utaona matokeo mazuri dhidi ya maumivu yako ya gout.

6. Tangawizi

Tangawizi ina matumizi mengi na imekuwa kwenye orodha ya dawa za asili au mbadala kwa ajili ya kutibu maradhi mengi kwa miaka mingi ikiwemo gout. Chemsha maji kama unachemsha maji ya chai, chukua tangawizi mbichi yaani ile ambayo siyo ya unga, kwangua (grate) kipande kimoja au viwili vya tangawizi ndani ya maji hayo yanayochemka, acha ichemke kama dakika 10, ipuwa na unywe kama chai kutwa mara tatu kwa wiki 3. Unaweza kuongeza asali au hata sukari kwenye huo mchanganyiko wa maji na tangawizi.

7. Ndizi

Ndizi zina kiasi kingi cha Potassiamu na Vitamini C na zinao uwezo pia wa kupunguza maumivu yatokanayo na gout kwa kuyeyusha asidi iliyoganda kwenye mkojo kuwa katika umajimaji ambao mwili wako unaweza kuutoa nje kirahisi. Kula ndizi kila mara kama unasumbuliwa na gout.

8. Mcheri

Tunda la mcheri lina kiasi kingi cha Vitamini C ambayo ni msaada mkubwa katika kupunguza asidi katika damu. Matunda 20 ya mcheri yakiliwa katika vipindi tofauti tofauti katika siku yanaweza kufanya maajabu dhidi ya maumivu yako ya gout. Ukinywa juisi ya mcheri pia ina matokeo yaliyo sawa na ukila matunda yake.

9. Unga wa mkaa

Pengine tayari unajuwa kuwa mkaa unao uwezo wa kuondoa harufu mbaya na hata sumu mwilini. Lakini lile ulikuwa hujuwi hadi sasa ni kuwa unga wa mkaa ambao unapatikana kwa kuusaga tu mkaa, unaweza pia kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

Changanya unga huu wa mkaa katika maji, chukua kitambaa kilichotengenezwa kwa pamba na ukiloweke kwenye hayo maji kisha funika katika eneo lenye maumivu ukiacha hapo kwa dakika kadhaa mara kwa mara kwa siku kwa majuma kadhaa kutasaidia kama siyo kuondoa kabisa maumivu ya gout.

 

10. Maji ya Kunywa

Maji ni mhimu sana katika kushusha maumivu ya kwenye maungio ikiwemo goutMaji ndicho kilainishi mhimu katika viungo vyote vya mwili. Kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10 za majimajiyaliyo katika joto la kawaida na siyo ya baridi, ukifanya hivi kila siku baada ya wiki 2 au 3 utakuwa huru kabisa na maumivu ya gout.

 

11. Juisi ya maharage machanga (French Beans)

Kunywa Juisi hii ya maharage machanga kwa muda wa mwezi mmoja ili kupata matokeo mazuri. Shida itakuwa namna ya kuyapata haya maharage hasa kwa wale walio nje ya D’salaam lakini ukihitaji nijulishe.

 

12. Mharadali

Mharadali (Mustard) ni nzuri sana katika kupunguza maumivu ya gout. Chukuwa mharadali ya unga na uweke kwenye eneo lenye maumivu na uuache ufyonzwe na ngozi yako kwa usiku mzima na utakapoamka asubuhi utajisikia vizuri kabisa.

 

13. Mchanganyiko wa juisi ya matunda na mboga mboga

Mchanganyiko wa juisi ya tango, magimbi na karoti unawea kutumika kutuliza maumivu yatokanayo na gout haraka sana.

14. Mafuta ya nyonyo

Pasha kidogo mafuta ya nyonyo katika moto kisha pakaa eneo lenye maumivu taratibu kama vile unafanya masaji kwa dakika kadhaa mara mbili mpaka tatu kwa siku, fanya hivi kila siku mpaka utakapopona kabisa.

No comments

Powered by Blogger.