Mafanikio yako hivi
JIFUNZE KITU HAPA
SOMO LA KWANZA.
Nilikuwa kanisani nikimsikiliza muhubiri mmoja maarufu, muhibiri alitoa mfukoni noti za shilingi elfu kumi kumi zilizokuwa na jumla ya Tsh laki moja, akauliza, "ni nani miongoni mwenu anataka nimpe hii laki moja?"
Watu wengi waliokuwa mle kanisani walinyosha mikono, kila mmoja alikuwa akishauti mimi! Mimi!. Nikaanza kushangaa ni nani atakuwa na bahati ya kupewa ile pesa kati ya mamia ya watu waliohudhuria ile ibada.
Pia nikajiuliza kwa nini (ambapo bila shaka na baadhi ya wahudhuriaji wengine nao walijiuliza) atoe kitita cha shilingi laki moja kirahisi rahisi hivyo.
Wakati watu wakiendelea kupiga kelele kusema nipe mimi, nipe mimi huku wamenyosha vidole vyao, kutokea nyuma akaibuka msichana mdogo mwenye umri kama miaka 18 hivi, akaenda mbele kule aliko yule muhubiri akafika mbele na kuchukua ile laki moja kutoka mkononi mwa yule muhubiri.
"Safi sana, msichana! Umefanya vema," alisema yule muhubiri.
"Wengi wetu tunapenda kukaa tu na kusubiri mambo mazuri yaje yenyewe. Hii haitaweza kuwasaidia hata kidogo, unatakiwa kuinuka na kutafuta mafanikio. Mafanikio hayawezi kuja kama umekaa tu.
Na maisha yetu ndivyo yalivyo, tunaziona fursa nyingi sana zikiwa zimetuzunguka, kila mtu anahitaji mambo mazuri. Ila tatizo hatutaki kusimama na kuzifuata hzo fursa. Simama sasa na ufanye kitu, usisubiri mafanikio huku umekaa, kamwe hayatakuja. Usijali kuhusu watu watasema nini. Chukua hatua.
SOMO LA PILI.
Baadae yule muhubiri akatoa tena noti ya shilingi 10000 na akainyanyua ili wote tuione. Nikafikiri anarudia kama mwanzo tena. Lakini akauliza swali jepesi. "Noti hii inathamani gani?" Waumini wakajibu "shilingi elfu kumi". "Mko sahihi" akawajibu.
Akaichukua ile noti akaifinyanga finyanga na kuwauliza tena noti ile inathamani ya shilingi ngapi!? "shilingi elfu kumi" wakajibu wale wauminii!
Akaitupa chini ipe noti, akaikanyaga kanyaga sana, akaichukua na kuuluza tena noti hii ina thamani ya kiasi gani? "Shilingi elfu kumi" waumini walijibu vilevile.
Muhubiri akawaambia nataka muweka katika akili yenu hili, "mtu hata aichakaze, aikunje kunje na kuikanyaga noti ya fedha, thamani ya noti itabaki pale pale."
"Maisha yetu ndivyo yalivyo, tunatakiwa tuwe kama noti ya shilingi elfu kumi. Ktk maisha kuna kipindi tutasalitiwa, tutakanyagwa, tutaonewa na kupigwa. Ila usiache thamani yako ipotee, kwa sababu mtu amekuumiza tu, hiyo haimaanishi ndio thamani yako imepotea. Wewe ni wa thamani mno jinsi ulivyo. Usiache thamani yako ipotee kwa sababu ya wachache!.. M?Mungu awe Pamoja nawe katika safari ya maisha yako. Daima tusikate tamaa
By well Jambo
Post a Comment