Header Ads

MOURINHO AANZA KUJIKOMBA KUELEKEA MCHEZO WA CHELSEA VS MAN UNITED



Jose Mourinho amesema kwamba kumbukumbu nzuri aliyonayo ndani ya klabu ya Chelsea haitamzuia kufanya kazi yake katika mchezo wa kesho wakati Chelsea itakapoikaribisha Manchester United Stamford Brigde.

Mourinho ndiyo kocha pekee mwenye mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kwa muda wote, akiwa ameshinda taji la Premier League mara tatu kwenye vipindi viwili tofauti alipokuwa klabuni hapo huku akibaki kuwa kipenzi cha mashabiki wa Chelsea.

Lakini licha ya kukiri kuwa hana uhakika ni kwa namna gani atapokelewa atakapokuwa amerejea, kazi yake kubwa ni kuhakikisha anapata matokeo chanya dhidi ya Chelsea.

“Kusema kwamba nitajali sana nitakaporejea pale si kweli kwasababu, kusema ukweli, ninapoenda kwenye mechi siangalii kuhusu hilo. Naangalia zaidi mchezo utakavyokuwa. Najaribu kujindaa mwenyewe kwaajili ya mchezo, hivyo siwezi kusema kama nitajali kuhusu hilo,” amesema.

“Nini hasa ninachotarajia? Sijui. Wanaweza kufikiria kuhusu mimi na kukumbuka mahusiano yetu mazuri na kuonesha reaction nzuri. Wanaweza kuningalia na baada ya dakika tisini kusema kwamba mimi ni meneja wa Man Utd na alikuwa akicheza dhidi yetu, hivyo si mtu ambaye tunampenda kwa wakati huu.”

Mourinho, ambaye alifukuzwa na Chelsea mwezi Desemba mwaka jana baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwa klabu hiyo, amesisitiza kuwa hatajiingiza kwenye vita ya maneno kufuatia msimu kuondoka vibaya klabuni hapo.

“Baadhi ya makocha, wanapoondoka kwenye vilabu walivyokuwa wakivinoa, wanapenda kusafisha nguo zao chafu, kwa maana ya kwamba wanapenda kuongelea masuala yaliyopita,” aliendelea kusema.

“Mimi si miongoni mwa watu wa aina hiyo. Ninapoondoka kwenye timu, naondoka nikiwa na moyo safi kabisa, kwasababu lengo langu lilikuwa ni kufanikiwa. Nilijitoa kwa kila kitu kwaajili ya mafanikio ya klabu na nisingependa kurejea pale na kuongea yasiyofaa.

“Lazima nijaribu kutunza vizuri vyote nilivyofanya, na kwenye klabu ya Chelsea, nimefanya mambo mzuri sana hasa kwenye suala la matokeo ya timu, nimekuwa na marafiki wengi pamoja na mepenzi ya dhati kutoka kwa mashabiki.

“Mashabiki hawajabadili mahusiano mazuri waliyonayo juu yangu eti kwasababu tu kwa yaliyotokea msimu uliopita. Hivyo lazima niheshimu heshima kubwa waliyonijengea kwa kipindi chote nilipokuwa pale.”


No comments

Powered by Blogger.