Udanganyifu wa mtihani wa darasa la saba
VIDEO: Matukio Sita ya udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016
on
October 27, 2016
COMMENTS
Baraza la mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ambapo kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2, kabla ya kutangaza matokeo hayo, katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde ameyazungumzia Matukio Sita ya udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016.
1. Moja ya matukio ya udanganyifu ni pamoja na la shule ya msingi Tumaini Sengerema ambapo mmiliki wa shule akishirikiana na wasimamizi alifanya mtihani na kuwapa majibu watahiniwa, wakayaandika kwenye sare zao wakaingia nayo kwenye chumba cha mtihani.
2. Shule ya little flower ambayo iko Serengeti, mwalimu mkuu akishirikiana na wasimamizi waliharibu mtihani wakaufanya na wakawapatia majibu wanafunzi, katika shule hiyo afisa wa baraza alipokuwa akifanya ufuatiliaji wa mitihani alimkamata mwalimu wa shule hiyo ambaye ni msimamizi akiwapa wanafunzi majibu.
3. Shule ya mihamakumi ambayo iko Sikonge mkoani Tabora, walimu walichukua form za kujibia mitihani, wanafunzi wanaingia chumba cha mtihani kutimiza wajibu tu baadae walimu wanachukua zile karatasi na kuanza kutoa majibu wao wenyewe
4.Shule ya Kashi Manyara, mwalimu alijificha chooni akiwa amepanga njama na mtahiniwa mmoja kwamba atoke na karatasi ya maswali ambapo mwalimu atafanya na baadaye mwanafunzi arudi chooni kuchukua majibu.
5. Shule ya St. Getrude Ruvuma, mwalimu mkuu na walimu kadhaa walifanya njama kuwaonyesha wanafunzi wote ambapo walipanga walimu wakae bwenini na kwenye nyumba ya mwalimu na wakaweka kikundi cha wanafunzi kadhaa ambao watakuwa wanapeleka maswali na baadae kuyaendea.
6. Shule kondi pamoja na kasandalala Sikonge watahiniwa walikuwa wote wanakosa kwa namna moja
katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde amesema baraza la mitihani Tanzania limeshatoa taarifa ya walimu na wafanyakazi wengine waliokosa maadili na baraza hilo litafanya ufuatiliaji wa makusudi kwa wanfunzi waliofaulu hasa watakapochaguliwa sekondari kuona umahiri wao wa kuwawezesha kufaulu.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV OCTOBER 27 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
RELATED ITEMSAYO TV
COMMENTS
← PREVIOUS STORYAyoTVMAGAZETI: Mchujo mpya bodi ya mikopo, CAG ashtukia ulaji wa mil 775 kila eka NSSF
NEXT STORY →VIDEO: Waziri Lukuvi ametaja maamuzi yaliyochukuliwa katika shamba la Sumaye Mabwepande
SOMA NA HIZI
VIDEO: Baada ya Mchungaji Lwakatare kuwatoa wafungwa DSM, sasa ni zamu ya Dodoma
VIDEO: Majibu ya Meya Kinondoni kwa wanaohoji uwepo wa Dk. Tulia na Ndalichako
AUDIO: Maneno alioyaongea kocha anayedaiwa kumrithi Hans Pluijm Yanga
TUPIA COMMENTS
VANESSA MDEE ALIVYOTUMBUIZA MOMBASA
KITU ALIKIBA ALIFANYA MWANZA KWENYE FIESTA 2016
MGAWANYO WA STORI
MGAWANYO WA STORI
Select Category Ajali (76) AyoTV (1,547) behind the scenes (7) Burudani (4,402) Duniani (290) Featured (22) Magazeti (1,787) Michezo (3,283) Miji/Nchi (53) Mix (3,127) on air with millardayo (88) Siasa (640) Sticky Post (1) TBT (36) Zaidi (2,629) Amplifaya Top10 (87) beef (15) BreakingNews (84) fB insta twitter (355) HekaHeka (397) Maajabu (82) magari (8) Mali za Mastaa (45) Nyumba/ Mijumba (66) social network (45) Stori Kubwa (911) Stori Muhimu (29) Stori Pekee (150) Videos (304) Vituko/ Comedy (216)
ZILIZOSOMWA SANA
Post a Comment