Wakatisha tamaaa
💥Je unamfahamu mtu anayekatisha tamaa?
Kabla hatujamfahamu mtu anayekatisha tamaa ni vema tukafahamu baadhi ya sifa za mkatisha tamaa.
#Mkatisha tamaa Mara zote ni yule ambaye amekuwa akikwambia na kukuonyesha ni jinsi gani utashindwa na pia huwa anakupatia mifano mbalimbali ya watu waliokuwa na malengo Kama yako ila walishindwa kutimiza malengo yao.
.
#Ni mtu ambaye amekuwa akikushawishi kutoamini uwezo ulionao. Mfano; utakuta mtu akikwambia kwamba jinsi anavyo kufahamu si mtu wa kufanya makubwa kwa kuwa huna uwezo/ujuzi wowote. Hii sio kweli!! Kwani mtu yeyote anaweza kufanya makubwa akiamua na kwa kufahamu uwezo alio nao.
#Mkatisha tamaa ni mtu anayependa kukujaza hofu na hali ya wasiwasi.
#Mkatisha tamaa ni mtu anayependa kulalamika pia ni mtu wa kukupa visingizio mbalimbali kwa nini uendelee kuwa wa kawaida. Ni mtu asiyependa kukuona ukiendelea na kuwa wa tofauti.
#Mkatisha tamaa ni asiye amini kuna kujifunza baada ya kukosea. Mfano; Unaweza kumkuta mtu akisema kuwa wewe si wakufanya jambo fulani kwa kuwa tu siku moja ulikosea kulifanya jambo hilo.
💥Hizi ni baadhi za sifa za mkatisha tamaa ila mtu huyu anasifa nyingi.
Swali la msingi, je mkatisha tamaa ni nani?
💥Mkatisha tamaa anaweza kuwa mtu yeyote, ninaweza kuwa ni mimi , wewe au yule. Ninamaanisha kuwa mkatisha tamaa anaweza kuwa ndugu yako, wazazi wako, majirani zako, wafanyakazi wenzio au mtu yeyote atakayekutana naye kwenye maisha.
💥Note:: Tusiishie tu kumfahamu mkatisha tamaa ila ni vema tukajua ni jinsi gani ya kuishinda hali ya kukatishwa tamaa.
💥Njia pekee ya kutokukatishwa tamaa ni kutokukubaliana na Maneno ya wakatisha tamaa. Usiiruhusu nafsi yako kuyaamini Maneno yao.
💥Siku zote kuwa na imani ya kuweza kwani hakuna lisiloshindikana chini ya jua. Kikubwa Imani.
Post a Comment