WATAALAMU KARIBU WATAKUGUNDUA DAWA NYINGINE YA KUTIBU MALARIA
Matokeo ya utafiti wa kimataifa yanaonyesha kwamba
wanasayansi karibu watafanikiwa kutengenza dawa yenye athari zaidi ya kutibu
ugonjwa wenye kuleta maafa mengi wa Malaria.
Dawa hiyo inayoitwa "NITD609"
ambavyo inatokana na mada ya 'spinoindolones' imeanza kutengenezwa kwa jitihada
mbalimbali za wanasayansi wa Marekani, Singapore, Switzerland, Thailand na
Uingereza.
Wanasayansi hao wanasema kwamba, dawa hiyo ambayo ni ya kumeza
inatofautiana na dawa nyinginezo za Malaria zilizopo madukani kwa kuponya
ugonjwa huo haraka, kutokuwa na madhara kwa mtumiaji na kuweza kutibu Malaria
kwa kutumiwa dozi moja tu.
Utafiti bado unaendelea kuhusiana na majaribio ya dawa hiyo na kwamba dawa hiyo imeonyesha mafanikio mazuri katika kutibu Malaria baada ya kujaribiwa kwa panya watano waliokuwa wagonjwa bila kuwa na madhara yoyote.
Wataalamu wanasema pia kwamba dawa hiyo ya NITD609 inatofautiana sana na dawa ziliopo za Malaria kwa umbo na kwa kikemia na kwamba ingawa dawa zilizopo zinaweza kutibu ugonjwa huo lakini zimeshindwa kufikia matarajio yanayotakiwa. Wataalamu sasa wanasubiri kuijaribu dawa hiyo kwa binadamu, suala ambalo litaanza baadaye mwakani.
Ingawa sote tunajua lakini si vibaya kukumbusha hapa kuwa watu karibu milioni 500 huugua ugonjwa wa Malaria kila mwaka duniani, ambapo vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo ni karibu milioni moja huku watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ndio wanaoshambuliwa zaidi na Malaria. Ugonjwa huo umekuwa ukisababisha vifo na matatizo mengi katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuliko maeneo mengineyo duniani.
Post a Comment