Header Ads

WATOTO MARUFUKU KUSIMAMIA HARUSI

OFISA Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Chunya, Theresia Mwendapole, amepiga marufuku kwa wakazi wa wilaya hiyo, kuwatumia watoto kwenye sherehe zikiwamo za harusi.
 
Mwendapole alitoa agizo hilo juzi, baada ya kukithiri kwa tabia hiyo na kwamba kosa hilo ni kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.

Alisema mtoto haruhusiwi kusimamia harusi kama bwana na bibi harusi na kwamba atayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mtu atakayebainika kufanya hivyo na kukutwa na kosa, adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya Sh. milioni moja.

Aidha alisema kifungu cha 95 sehemu ndogo ya 1, 2 na 3 kinaeleza kuwa ni jukumu la kila raia mwema, maofisa ustawi wa jamii na polisi kutoa taarifa sehemu husika na kushughulikia uvunjwaji wa haki za watoto kwa mujibu wa sheria hiyo.

Mwendapole alisema sheria hiyo inapiga marufuku kwenda kwenye kumbi za starehe kama baa na casino.

No comments

Powered by Blogger.