Header Ads

Nani mpangaji wa maisha yako

Chagua maisha sasa

1.Huwezi kuchaguwa wazazi wa kukuzaa na mahali pa kuzaliwa, Lakini unaweza kuchaguwa aina ya maisha utakayoishi!
NA NDICHO ULICHOFANYA UMECHAGUWA KUISHI UNAVOISHI SASA.

2.Mtu wa kwanza kulaumiwa kwa jambo lolote kuhusu maisha yako ni WEWE,
Wa pili ni WEWE,
Na watatu ni WEWE,
USITAFUTE MCHAWI.

3.Kuna majukumu unaweza ukawaachia watu wengine, lakini si jukumu la kuyaishi maisha yako.
HAKUNA ANAYEWEZA KUISHI KWA NIABA YAKO,
WAJIBIKA WEWE.

4.Weka bidii katika kila unataka kukifanya, husisha moyo wako na akili zako,
KAMA UNATAKA KUPATA MATOKEO MAZURI.

5.Mtegemee MUNGU daima, kamwe Usitegemee akili zako na uwezo wako tu,
Kuna mahali huwezi kupenya bila MUNGU.

Chukua Hatua

No comments

Powered by Blogger.