Header Ads

Pumu (asthma)

Tiba ya Pumu: unatakiwa kufanya nini  ukiwa na pumu?
Pumu ni ugonjwa ambao unashambulia watu wa pande zote za dunia, na inakadiriwa kuwa karibu watu milioni 300 wana  ugonjwa huu duniani. Ni ugonjwa ambao hushambulia watu wa jinsia zote na rika zote lakini mara nyingi zaidi watu hupata ugonjwa huu utotoni. Watoto wengi huanza kupata dalili za ugonjwa huu wanapofikia umri wa miaka mitano. Watoto wali kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na maradhi haya ni wale wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, wale wanaolelewa kwenye mazingira yenye moshi wa sigara na wale wanaozalia kwenye familia zenye kipato kidogo.
Watoto wenye ngozi nyeusi wanakuwa hatarini zaidi kuliko weupe. Mambo mengine yanayochangia ni mtoto kuwa na mzio (allergy) wa kitu fulani na/au kuzaliwa na wazazi wenye asili ya kuwa na maradhi haya. Watoto wa kiume hupata ugonjwa huu zaidi ya watoto wa kike lakini hali hubadilika wanapokuwa wakubwa. Katika ukurasa huu tutaona ni nini tiba ya pumu na jinsi ya kufanya ukiwa na ugonjw huu ili uweze kuishi na kufanya shughuli zako za maisha bila kusumbuliwa na maradhi haya.
Pumu inatoka Wapi?
Katika ukurasa uliotangulia wa “ujue ugonjwa wa pumu” tuliona nini maana ya pumu na ni nini kinatokea tunaposema mtu amebanwa na pumu. Nina uhakika umekuwa unajiuliza huu ugonjwa unatoka wapi au unasababishwa na nini. Kwa kifupi sana hapa chini tutatoa majibu kwa swali lako.Vyanzo vya pumu vimeeleweka kuwa ni kama ifuatavyo:
Mzio (Allergy): Karibu watu wote wenye pumu wana mzio (allergy) ambayo ni hali ya miili yao kutopenda vitu fulani pale vinapovutwa na hewa mtu anapopumua, vikiliwa, vikiingizwa mwilini kwa kudungwa sindano au vikigusa ngozi zao. Lo lote likitokea katika hayo mtu mwenye mzio anaweza akawashwa macho, akatokwa na kamasi, akapumua akitoa sauti ya vifilimbi, akatokwa na vjipele juu ya ngozi au akapata tumbo la kuharisha. Baadhi ya vitu vinavyosababisha hali hiyo (allergens) ni protini za wanyama, poleni ya mimea, nyasi, vumbi, mende na baadhi ya madawa.
Katika kujilinda, kinga za miili yetu zilizopo ndani ya damu mara nyingi husababisha njia za kupitisha hewa kutoka na kwenda mapafuni kuvimba ambako kunahusishwa na pumu.
Moshi Wa Tumbaku
Uchafuzi Wa Mazingira: Dalili nyingi za pumu zinatokana na uchafuzi wa mazingira na hasa wa majumbani kutokana na mvuke unaotokana na vifaa vya kusafishia nyumba na rangi za kutani. Majiko ya kupikia yanayotumia gesi yanayotoa hewa aina ya nitrogen oxide ambayo pia huhusishwa na tatizo la pumu. Watu wanaopika kwa kutumia gesi hupatwa na matatizo yanayoambatana
na pumu kama kupumua kwa shida na kubanwa na pumu.
Vitu vingine kwenye mazingira vinavyoaminika kusababisha pumu ni sulfur dioxide, nitrogen oxide, ozone, hali ya hewa ya baridi na hali ya kuwa na unyevunyevu mwingi katika hewa (high humidity).
Kula Kupita Kiasi: Watu wazima wenye uzito mkubwa sana wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata pumu ukilinganisha na wale wenye uzito wa kawaida. Utafiti unaonyesha kuwa hatari ya kupata pumu isiyotokana na mzio (nonallergic asthma ) ni kubwa
zaidi kuliko ile inayotokana na mzio (allergic asthma).
Ujauzito Na Uzazi: Jinsi uliovyoingia katika dunia hii ina uhusiano na uwezekano wa kupata pumu baadaye. Watoto waliozaliwa kwa operesheni wana asilimia 20 zaidi ya uwezekano wa kupata pumu baadaye – inawezekana kuwa maambukizi yanayoathiri kinga za mwili kutokana na uwepo wa bacteria wakati wa operesheni yanahusika na tofauti hii.

Akinamama wanaovuta sigara wakati wa ujauzito husababisha watoto wao matumboni kuwa na uwezo mdogo wa kupumua na kuongeza hatari ya watoto wao watakaozaliwa kupata pumu. Utafiti umeonyesha kuwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (njiti) wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuja kupata pumu baadaye.
Msongo Wa Mawazo: Kupatwa na msongo wa mawazo mara kwa mara kunaongeza uwezekano wa kupata pumu, moja ya sababu ni tabia za mtu anapokuwa na msongo wa mawazo kama vile kuvuta sigara kunakochochewa na msongo wa mawazo. Maelezo ya hapa karibuni yanaonyesha kuwa mfumo wa kinga za mwili hubadilika mtu anapokuwa na msongo wa mawazo!




Follow me on
Welfarejambo.blogspot.com
Contacts 
             0765896355 on whatsapp 
             0684127127.
Email address 
            Welljambo78@gmail.com 
Instagram 
          welfare Jambo 
Facebook 
            Well Jambo 


No comments

Powered by Blogger.