Header Ads

Haiba na Tabia za watu

Yafahamu makundi mkuu manne ya Haiba na tabia za watu
1.sangwini
2.melankoi
3.fregmatiki
4,koleeiki

Je Wewe Uko kundi lipi?
Je unaifahamu haiba na tabia yako?

Basi fatilia kwa makini Pamoja nami kujifahamu upo kundi lipi hii utanisaidia kujitoa kwenye matatizo yanayokukumba na kutengeneza mstakabari wa maisha yako

Kundi la kwanza  ni watu wanaoitwa
Sangwini

Sifa za sangwini

  1.Ni watu Wenye Ujasiri Mkubwa Sana. 
Sangwini ni watu wenye ujasiri mkubwa sana. Huwa hawaogopi kuongea, hawaogopi kujitokeza mstari wa mbele, wanaujasiri mkubwa wa kujitokeza mbele kukabiliana na yeyote au chochote. Mwanaume ambaye ni Melankoli ambaye ameoa mke Sangwini usiku nyumbani akitokea nyoka mwanaume atakuwa anakimbia kurudi nyuma na mke wake atakuwa anakimbia mbele kukabiliana na huyo nyoka na mume yeye atabakia kumuhamasisha mkewe pigaa, pigaa, mkanyage kabisa mpaka afe, ila yeye hatathubutu kumsogelea. Sangwini hawaogopi kusimama mbele ya umati wa watu na kucheza au kuongea kwenye kadamnasi.

2. Mara nyingi sio watu wa kuwekea sana jambo moyoni.
Sangwini hana chumba cha kuhifadhi mambo moyoni kwa muda mrefu. Anakasirika kwa haraka sana na hasira zake zinaisha kwa haraka sana kwasababu ya ile sifa ya misisimko. (emotion) misisimko yake ikishuka tu na hasira zinashuka pia anarudi kuwa kawaida kabisa. 
3. Wanapenda kutawala mazungumzo.

4. Sangwini ni watu wenye nguvu (Energetic) na mara nyingi hutumia nguvu nyingi badala ya akili nyingi.
Ni watendaji wazuri sana wa kazi, lakini tatizo lao ni kwamba wanatumia nguvu nyingi sana katika utendaji wao kuliko akili. Mara nyingi kazi nyingi zinazohitaji akili zaidi kuliko nguvu huwa zinawashinda. Ndio maana kwenye baadhi ya maofisi wanasababisha migogoro kwasababu kama wamepewa kazi za akili mara nyingi huwa wanashindwa kufikisha matarajio ya wakubwa wao na hapo ndipo migogoro hutokea.

5. Wanapenda kujiunganisha na mambo mbalimbali bila kufikilia kwa undani (Engaging).
Kikundi chochote kinachoanzishwa, au kanisa, au chochote watu wa kwanza kujitokeza na kujiunga huwa ni kundi hili la Sangwini. “Deal” likitokea watu wa kwanza kujiunga ni Sangwini. Mara nyingi huwa wanajiunga hata kama hawajui chochote kuhusu hicho wanachojiunga bora wamesikia tu wanahitajika watu kujiunga wao watajitokeza kwa haraka. Lakini ujue kama jinsi ambamvyo wanajiunga kwa haraka bila hata kufikiri fikiri, ndivyo watakavyo ondoka, baada ya muda mfupi wataondoka bila hata ya kuwa na sababu yoyote ya msingi. Walio wengi wa hawa ndio wanaoongoza kwa kuhama hama makanisa kila kukisha na hata ukiuliza kwanini wanahama hama hawawezi kukupa sabau yeyote ya msingi. 

Kukitokea vyama vya kupanda mbegu kidogo na kuvuna sana, hata kama wengine watajiunga lakini Sangwini ndio watakuwa wakwanza kwenda kupanda bila hata kujali wala kujiuliza hayo mavuno yanatokana na nini.

6. Wanapenda Umaalufu na Kujulikana.
Sangwini wanapenda sana kuonekana mbele yaw engine. Wanapenda sana umaarufu wanapenda sana kujulikana na kila mtu na hasa katika maeneo yatakayomletea sifa. Wanapenda sauti zao ndio zisikike, wanapenda sura zao ndio zionekane. Ukitaka uwe rafiki wa Sangwini mpe umaarufu.

7. Ni wabunifu sana. Mara nyingi huwa hawalali njaa. Ni wajasiliamali wazuri sana.
Ukimkuta Sangwini kalala njaa, basi huyo kama ni mjini tunasema wakuja huyo bado anasoma ramani. Sangwini wana uwezo mkubwa sana wa ubunifu wa kufanya vitu mbali mbali hata kama ni vidogo vidogo na wakajiingizia kipato na kusukuma siku. Wanaweza kuongea tu na pesa ikaingia. Wanauwezo wa kubuni vitu ambavyo kwa kawaida usingevizania kuwa vingeweza kuwaingizia kipato.
Siku moja Dar es salaam nilikutana na wanaume wawiwi njiani. Mmoja alikuwa amevaa gauni anajifanya kama ni mwanamke na mwingine amevaa shati na tai ndefu imepita chini ya uvungu wa miguu yake ikatokezea huku nyuma kama mita mbili au tatu hili inaburusa, hiyo tu ilikuwa ni kazi wakipita watu wanacheka wanawapa pesa watoto wanakwenda shule, wanakula wanalipa kodi za nyumba nk.

8. Ni watu wanaopenda urafiki (they are Friendly)
Sangwini anapenda sana marafiki na mambo ya undugu. Wanapenda kutengeneza marafiki kila mara. Kina anapokwenda anapata marafiki wengi tu wapya. Ni hodari sana katika kutembelea ndugu na jamaa na marafiki na kuimarisha mahusiano. Tofauti sana na kundi kama Melankoli, kundi la Melankoli hataki mambo ya ndugu ndugu, au sijui mambo ya vikao vya ukoo au kukutana kutana, hayo ni mambo ya Sangwini. Wewe angalia hapa humu facebook Sangwini anaongoza kwa kuwa na marafiki wengi. Yeyote atakaye muandikia kumuomba urafiki kwa Sangwini hajali kama anamjua au hamjui anadini au hana dini Sangwini kwake ni ku-add tu hayo mabo mengine yatajiseti mbele kwa mbele kwake yeye bora amepata marafiki wengi zaidi. Wakati mtu kama Merankoli mpaka aje kuku-add ujue umepitia michujo ya aina yake kweli. Ni mtu wa watu. Ni mtu wa mahusiano. Nk.

9. Wapo Tayari Wakati Wowote Hawahitaji Maandalizi. 
Mara nyingi hata kwenye kazi nyingi za kujitolea Sangwini ndio huwa watu wa kwanza kabisa kujitokeza kwenye jambo lolote. Huwa hawahitaji kujiuliza uliza mara mbili wanaamua hapo hapo na wanakwenda. Ikitangazwa inahitajika watu wajitolee msaada wa damu salaama Sangwine anaweza kujitokeza hapo hapo wakati watu wa makundi mengine wanaweza wakasita kwanza wengine wakasema ngoja kwanza tukajadilianane na wife then tutaleta jibu. Sangwine hana cha kwenda kujadiliana na mke wala mume anafanya hapo hapo. Kama ni mchango na anahela mfukoni atatoa hapo hapo hakuna cha kusubiri.

Tatizo ni kwamba Sangwini hanaga ratiba maalum na hata akiwa nayo hawezi kuisimamia. Kama alikuwa anakwenda Kariakoo ukakutana naye ukamwambia bwana utakwenda siku nyingine huko twende zetu kunduchi unisindikize. Bila kubisha sana atageuza na kuacha shughuli zake na kwenda na wewe kunduchi.

10. Mahali pao pa kazi hapana mpango mzuri pamejaa vitu ovyo ovyo. 
Wakati mwingine ukiingia kwenye ofisi ya Sangwine unaweza usipate taabu sana kugundua haiba yake ni ipi kwa haraka sana utagundua. Sangwini wengi wahana mpangilio mzuri katika maendeoe yao. Kama ni ofisini utakuta mafaili yamekaa hovyo hovyo makaratasi kila mahali, yeye mweneywe ili apite anapita kwa kuruka ruka unaweza ukavikiri ni kama jalala la makaratasi kumbe ni ofisi ya Sangwini. Kama ni mama nyumbani Sangwini, akianza kutafuta mwiko usishangae ukaukuta umewekwa juu ya neti.
Ukiingia mlangoni kwake unakutana na sufuria za ugali wa juzi alizoloweka ziko kuanzia mlangoni, viatu juu ya kitanda mito ya makochi iko nyumba ya pili barazani kwa jirani, yaani ilimradi ni vurugu vurugu hakuna mpangilio hakuna utaratibu. Mume mmoja alikuwa ananiambia pasta wala usije ukashangaa kukuta brazia ya mke wangu kwenye friji. Nikacheka sana alikuwa anajaribu kuonyesha jinsi mkewake asivyoweza kupangilia kitu.

Nyumbani kwa Sangwini kama ni nguo za watoto humo humo za baba humo humo za mama humo humo. Ikifika wakati wa kutafuta nguo za kuvaa kutokea wanapanga foleni kama vila wako mnadani kila mtu anachagua za kwake na mbaya zaidi nguo safi na chafu zote zipo kwenye kapu moja utajua hii safi nah ii chafu kwa kuweka puani harufu ndio itakutofautishia chafu na safi.

Madhaifu ya sangwini

1. Kukosa Nidhamu Ambako Kunadhihirika kwa Njia Nyingi.
Moja wapo ya madhaifu ya Sangwini ni kukusa nidhamu ya kutosha katika mambo mbali mbali. Kama ni masomo Sangwini sio mpenzi wa kusoma sana na kujisimamia mwenyewe. Mwalimu akitoka na yeye anatoka. Kama ni mashureni wanao ongoza kwa kupiga kelele darasani ni Sangwini. Mitaani/ makazini na kwinginepo, wanaoongoza kwa uchokozi na vurugu ni Sangwini. Huwa na nidhamu ya chini katika mambo mbali mbali.

2. Ni watu wa “Milipuko” Hii kwa Kawaida Huisha kwa Haraka kama Ambavyo Huanza.
Sangwini ni watu wa milipuko. Anaweza akalipuka kufanya jambo kwa nguvu sana lakini huwa na nguvu ndogo sana ya kuliendeleza jambo hilo. Mara baada ya muda kidogo tu huishiwa nguvu za kuendeleza hilo jambo alilolianzisha na mara moja huliacha na kushika kitu kingine. Sangwini ni kundi linaloongoza kwa kuchumbia chumbia mara kwa mara na kuacha au kuvunja uchumba bila hata sababu zinazoeleweka. Wanachumbia hawaoi, wanaanzisha hawamalizi. Wanaanzasha baishara kabla hata haijakomaa wamesha acha. Wanaanzisha makanisa kabla hata hayaja komaa wanaacha na kuanzisha mengine au kitu kingine.

3. Kukosa utulivu wa ki-akili. Mawazo ya Sangwini, hayajatulia. (not concetrated).
Mawazo ya Sangwini yametawanyika. Sangwini anatatizo la kuelekeza mawazo yake kwenye jambo moja (concetration) “They are not focused” Hii huwasababisha kuwa na uwezo mdogo wa kushika mambo mazito ambayo yanahitaji “concetration” Mara nyingi ndio kundi linalo ongoza kwa kubamizwa na masomo. Wanafunzi walio wengi wa kundi hili hawafanyi vizuri sana katika masomo yao. 

4. Si wepesi Kustahimili Mambo Magumu au Shuluba.
Sangwini hapendi maisha ya shida, anapenda maisha rahisi na mteremko yasiyo hitaji kumghalimu sana. Hupenda kazi rahisi rahisi, yasiyomfanya atoke jasho sana au aumie sana. 
Sangwini anapenda kuchumia kivulini na kulia kivulini.
Sangwini wengi mashuleni wanachagua masomo yaliyo rahisi na yasiyo “complicated” nimefuatilia nikagundua ni marachache sana tena kwa uchache kumkuta Sangwini anapenda hesabu. Kama atapata nafasi ya kuchagua masomo waliowengi wasingechagua masoma magumu kama hesabu n.k.

5. Wanaahidi ahadi nyingi ambazo hawatakuja kamwe kuzitimiza.
Sangwini ni hodari sana wa kutamka na kuahidi mambo makubwa makubwa na kwa mikwara mingi. Tatizo lake Sangwini linakuja kwenye kutimiza hizo ahadi walizo ahidi. Madaftari mengi makanisani makazini na kwinginepo yamejaa ahadi za Sangwini ambaye yeye mwenyewe tayari Alisha sahau siku nyingi kama anadaiwa na mbaya zaidi hana mpango wa kutekeleza kile alichokiahidi.

6. Ni wazuri kwa kukopa na mara nyingi huwa hawalipi madeni yao.
Kwanza lazima ufahamu kuwa Sangwini wana ujuzi mzuri wa kuongea na kumshawishi mtu kuingia “line” katika jambo fulani. Wanapokuja kukupa wanakuja la lugha laini na tamu sana na wakati mwingine kukuahidi jinsi ambavyo hata wewe utanufaika na na kufurahia matunda ya kumkopesa yeye hicho kiasi cha pesa na kukuahidi kuwa hata kabla ya ile tarehe ya kurejesha atakuwa amesha rejesha kila kitu. Mambo huwa tofauti sana na makubaliano. Walio wengi wakikopa ni wagumu sana wa kulipa madeni. Huko magengeni wanakopa, madukani wanakopa na kwenye maeneo mbali mbali wanakopa na hawalipi na hiyo kusababisha mnigogoro na magombano katika jamii. Sangwini hajali usumbufu wa kudaiwa. Akilini mwake deni sio miongoni mwa vitu vinavyomsumbua kama ambavyo ingekuwa kwa kundi kama Fregmatiki akidaiwa anaweza hata asipate usingizi kwajili ya deni. Sangwini anaweza akawa anadaiwa madeni makubwa tena na kundi la watu wengi hiyo haitamuondolea usingizi atalala tena kama hajaset alam anaweza hata kupitiliza masaa ya kulala.
Unapomkopesha Sangwini kuna mawili ulipwe au usilipwe.

Sangwini kiboko yake ni Sangwini mwenzake. Ukitaka kufurafia mechi ni pale Sangwini kamkopesha Sangwini mwenzake na hataki kulipa. Hapo ndi po huwa nyasi zinawaka moto. Mwishowe huishia kupelekana kwenye vyombo vya sheria na mwishowe kulipana kiduchu kiduchu kwa muda mrefu mpaka mdai anaamua kusamehe na kusahau.

7. Uwezo wao wa Kufikiri Upo Chini.
Uwezo wao wa kufikiri upo chini pia hawana uwezo wa kufikiri kwa undani. Mara nyingi hutegemea kichwa cha mtu mwingine kupata majibu ya maswali yao. Sangwini hapendi kuushughulisha ubongo wake hata kwa vitu vidogo tu. Hesabu ndogo tu ya gengeni hawezi kupiga mwenyewe mpaka atafute caluculator ndio apige mahesabu. Sangwini hawezi hata kujua au kukumbuka tarehe ya leo. Utasikia mara nyingi Sangwini anauliza, “hivi leo juma ngapi? Au leo tarehe ngapi, au hivi huu ni mwaka gani? Juma moja lina siku saba tu lakini Sangwini siku hizo saba zinamshinda kufikiri na kuchambua na kupata jibu kuwa leo ni siku gani mpaka atafute jebu kutoka kwenye kichwa cha mtu mwingine. Tarehe zipo 30 lakini Sangwini hawezi kujua leo ni tarehe ngapi mpaka atumiye ubongo wa mtu mwingine. Huwa najiuliza kama tahehe zingekuwa 366 kwa mwezi mmoja maisha ya Sangwini yangekuwaje?

8. Sio wazuri kuwa viongozi wa juu au kushika nyadhifa za juu kabisa.
Sangwini sio wazuri wa kupewa uongozi wa juu kabisa. Sangwini akiwa ndiye kiongozi wa juu kabisa lazima kanisa au shirika au taasisi itayumba na utatarajia migogoro na marumbano na magomvi ya kila mara katika kanisa, shirika au taasisi. Sangwini anapaswa afanye kazi chini ya mamlaka nyingine asiwe yeye ndiye “top” Sio wazuru wa kuwa viongozi wa juu kabisa kwasababu Sangwini wanatatizo katika swala zima la maamuzi. (Decision making) Maafuzi ya Sangwini mara nyingi huwa sio ya kina mara nyingi huwa yanatokana na “emotion” baada ya muda akitulia vizuri anagundua kuwa hakuwa ameamua vizuri na tayari utekelezaje wa maamuzi hayo unakuwa umeshafika mbali mahali ambapo hawawezi tena kurudi nyuma. Sangwini akishika nafasi ya juu kabisa atakuwa ni kiongozi mwenye maneno mengi na ahadi nyingi lakini utekelezaji wa hali ya chini. Kwahiyo mnapofanya uchaguzi mbalimbali zingatia kama nafasi ya juu kabisa ile ya “final say” isiende kwa Sangwini hata kama ndio wengi wanamtaka huenda ni ushabiki tu akiingia madarakani mtajuta kwanini mlimchagua.

9. Hawapendi Kuchulkuliwa Hatua za Kinidhamu Pale Wanapokuwa Wamekiuka Taratibu. 
Sangwini anatatizo katika swala zima la nidhamu. Hapendi kuchukuliwa hatua za kinidhamu hata kama atakuwa amekosea kabisa. Utakapoanza tu kumuonya basi atakasirika sana kwa hayo maonyo. Wengine watazila kula au watazira kufanya jambo fulani kisa nini ulimsema au kumuonya kwa kosa fulani. Wanataka hata wakikosea wasiambiwe ukweli kama wamekosea. Sangwini akionywa au kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa makosa yake anaweza akalia sana na kulalamika kila mahali kanakwamba ameonewa kwa kiasi cha hali ya juu sana. Wakati mwingine akichukuliwa hatua kwa makosa yake au kuonywa wakati mwingine huamua hata kujiua kutokana na kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Huu ni udhaifu mkubwa alio nao Sangwini. Ni mtu mwenye hasira sana tena wakati mwingine hasira zilizopitiliza.

10. Sio Wazuri Kushika Nafasi za juu za Uongozi.
Sangwini anahitaji kuwa chini ya mamlaka nyingine. Sio wazuri kushika nafasi za juu kabisa katika uongozi. Kama Sangwini akiwa ndiye kiongozi wa juu kabisa yaani “top leader” huenda kanisa au kampuni au taasisi isiwe katika hali nzuri. Wanatatizo kubwa katika eneo la “decision making” maamuzi yao huwa sio ya kina wanaamua kabla hawajachambua na kufikiri kwa kina na baadae wanapokuja kukutana na ukweli na uhalisia inakuwa ni “too late” maamuzi yalisha fanyika na hatua za utekelezaji zilishaanza kutendeka. Sangwini akiwa the “top leader” mwenye “final say” basi utatarajia migogoro, magomvi na hali ya kutoelewana katika shirika au taasisi. Nivizuri tunapochagua viongozi kulizingatia hili.

11.Masangwini kwa maadili wapo chini sana na ni mrahisi sana kuwayumbisha wengine kwani wana uwezo mkubwa sana wa ushwawishi hasa wakiwa katika nafasi mbalimbali za uongozi,Japo wana uwezo mkubwa wa vipawa, lakini kwa bahati mbaya sana, kwa kuwa hawana kiasi ni wepesi sana kudidimia na kukosa kukua katika vipaji kutokana na tabia yake ya kukosa kiasi,Sangwini hana UMAKINI, they are very careless.Walio wengi ni wachokozi na ni waanzilishi wazuri wa migomo na vurugu japo baadaye hukimbia hii ni kutokana na tabia yao ya kuenenda kihisia zaidi.Si wepesi kustahimili mambo magumu, they like easy things.Hunia mengi na kutimiza machache au hawatimizi kabisa.

12.Ni mwepesi kuendeshwa na matukio na si mipango.Uwezo wao wa kustahimili nafasi za juu ni mdogo sana.Hawapendi kuchukuliwa hatua za kinidhamu pale wanapokosea.Wanalalamika sana hasa pale mambo yanapokuwa ndivyo sivyo.

13.WANAPENDA SANA UCHOCHEZI.Husahau majukumu yao ya msingi.Ni wepesi kutafakari vitu visivyo vya muhimu na kusahau yale ya msingi.

14.Mara nyingine huwa wabinafsi sana.Hukosa hali ya kujiamini na hivyo hunisababishia kujishuku.

MELANKOLI

Melankoli ni nani?.

    Kwaasili wanafahamika kama (wakamilifu) Perfectionists. 

   Mungu ni wa pekee sana na alipenda na sisi wanae tuwe wa pekee kama yeye.Melankoli ni mtu anayesemekana kuwa wa tafakari za kina sana hali ambayo kwa kawaida huweza kumsababishia kuwa na mahangaiko pindi mambo yanavyoenda kinyume na mitazamo yake. 

     Ni mtu mwenye siri sana na kwa hali ya kipekee kuwa wabunifu wa maswala makubwa na ya maana sana.
     Tofauti na haiba nyingine, melankoli anasemekana kuwa mtu anayejali sana ubora, hii humfanya awe mtu wa kusahihisha sana.

itaendelea na madhaifu ya melankoli na Haiba zingine

No comments

Powered by Blogger.