Header Ads

Faida za zabibu kiafya

FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA


Zabibu ni matunda matamu yanayopendwa yakiwa na faida nyingi kiafya kwa mwili. Kuna zabibu za rangi ya kijani, nyekundu na kama nyeusi. Unaweza kula zabibu kama matunda, zabibu zilizokaushwa (raisin) au kama juisi ya zabibu. Zabibu hutumikana sana kutengeneza mvinyo (wine)sehemu mbalimbali duniani.
Faida za zabibu kiafya hujumuisha kusaaidia kuondoa kukosa choo, mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri, kupunguza uchovu na kuzuia mtoto wa jicho.
VIRUTUBISHO VILIVYOPO NDANI YA ZABIBU
Kwa kila gramu 100 za zabibu zina wastani wa virutubishi vifuatavyo;
Nishati kilokaro 69Wanga gramu 18.1Sukari gramu 15.48Kambakamba gramu 0.9Mafuta gramu 0.16Protini gramu 0.72
Vitamini
Vitamini B1, B2, B3, B5, B6, B9Vitamini CVitamin EVitamin K
Madini
Kalsiamu miligramu 10 mgChuma miligramu 0.36Magneziamu miligramu 7mgManganizi miligramu 0.071Sodiamu miligramu 2mgPotasiamu miligramu 191Fosforasi miligramu 20

FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA

Ulaji wa zabibu katika mlo wako una faida nyingi kiafya, zikiwemo:

Kutibu Pumu

Zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu..

Huimarisha Mifupa

Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi kwenye zabibu, na madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya. Kula zabibu mara kwa mara inasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri kuwa mkubwa. Pamoja na kuimarisha mifupa, madini haya husaidia mwili kufanya kazi vizuri.

Hulinda Dhidi ya Magonjwa ya Moyo

Zabibu huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu na ina kampaundi za flavonoids aina za resveratrol na quercetin ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Haya yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo na shinikizo la damu.

Kusafisha Figo

Zabibu zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo, pia hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mokojo unaotengenezwa na figo.

Kupunguza Lehemu (cholesterol)

Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu kwenye damu. Zina kampaundi kama pterostilbene ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza unywonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo.

Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani

Kama tulivyoona hapo juu kampaundi zinazopatikana ndani ya zabibu kama resveratrol ambazo husaidia kuondoa sumu zinazoweza kuleta saratani mwilini. Baadhi ya kampaundi nyingine huzuia seli za saratani kukua na kuzaliana; kuimarisha mfumo wa kinga wa mwili.
Zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi pia kama kuzuia choo kigumu, homa na kuongeza damu.
Hakikisha unaosha zabibu kwa maji safi ya moto kabla ya kuzila.

Ahsante

No comments

Powered by Blogger.