Header Ads

Dentistry/Dental surgery/Odontology

Dentistry/Dental Surgery/Odontology
Tawi la utabibu la magonjwa ya kinywa na meno.
Branch of medicine concerned with diseases of the mouth, teeth, jaws and adjacent tissues.

PERIODONTICS
Tawi la taaluma ya kinywa na meno linalojishughulisha na utafiti pamoja na matibabu ya magonjwa ya fizi
Branch of dentistry comprising the study and treatment of diseases that affect the gums and periodontal insertion.

GINGIVITIS
Fizi kuvimba na kutoa damu.
Inflammation and bleeding of the gums.

PERIODONTITIS (PYORREA)
Ni mangonjwa ya fizi na mfupa unaoshikilia meno yanayoambatana na kinywa kutoa harufu mbaya,meno kulegea na hatimaye kungo’ka kabisa.
Infection and loss of the gum attachment characterized by bad breath, tooth mobility, separation, and progressive painless tooth loss.Subgingival Calculus
Ugaga ndani ya ufiziDental Stains/Smoker’s Periodontitis
Rangi kwenye meno/ magonjwa ya fizi yatokanayo na uvutaji wa sigaraHalitosis (bad breath)
Harufu mbaya ya kinywaGingival Recession/Gingival Enlargement/Gingival Smile
Kulika kwa fiziPeriodontal Surgery/Mucogingival Plastic Surgery/Aesthetic Surgery
Matibabu ya magonjwa ya fizi kwa njia ya upasuaji.Gingival Graft/Gingivectomy/Gingivoplasty
Urekebishaji wa fizi kwa njia ya upasuaji.Periodontal Pocket/Root Furca
Kuchimbika kwa fiziDental Hyperesthesia (Sensitive Teeth)
Meno kufa ganziTooth Separation/Tooth Displacement/Loose Teeth
Meno kulegea/ kutingishika

PERIODONTIST
Daktari bingwa wa taaluma ya kinywa na meno inayojishughulisha na kinga, kugundua na kutibu magonjwa ya fizi na mifupa inayoshikilia meno
A dentist specialized in the prevention, diagnosis and treatment of periodontal diseases.

CURETTAGE, SCALING and ROOT PLANNING
Kusafisha meno yenye ugaga wakati wa matibabu ya magonjwa ya fizi.
Used in the hygienic phase of periodontal treatment.

PERIODONTAL MAINTENANCE PHASE
Kudhibiti ukuaji na muendelezo wa magonjwa ya fizi kwa mgonjwa.
Control of the evolution and activity of the disease, and support for the periodontal patient.

IMPLANTOLOGY
Taaluma ya kinywa na meno inayojishughulisha na kupandikiza meno bandia kwenye mfupa wa taya kwa kutumia vifaa maaalum.
Branch of medicine and dentistry that restores lost teeth with bone-integrated dental implants.

OSTEO-INTEGRATION 
Muungano wa sehemu ya mfupa na kichuma (titanium screw) cha kupandikiza meno ili kujishika na kufanya kazi yake kama kawaida.
Biological process whereby bone tissue directly adheres to the surface of an implant to provide a direct, functional and stable connection.

ORTHODONTICS/MAXILOFACIAL ORTHOPEDICS
Taaluma ya kinywa na meno inayojishughulisha na kugundua , kurekebisha meno yaliyoota vibaya pamoja na kutibu matatizo ya muonekano mbaya wa uso.
Branch of dentistry comprising the study and treatment of malpositioned teeth and their consequences for the maxillars, as well as growth disorders of the lower third of the face.

INTERCEPTIVE ORTHODONTICS
Taaluma ya kurekebisha mpangilio wa meno kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6-12.
Orthodontics performed during mixed dentition (6-12 years of age).

ORTHODONTIST
Daktari bingwa wa taaluma ya kinywa na meno inayojishughulisha na kinga, kugundua, na kurekebisha mpangilio wa meno yaliyoota vibaya.
Dentist specialized in the prevention, diagnosis and treatment of dental and skeletal malocclusions.

PEDIATRIC DENTIST
Daktari bingwa wa kinywa na meno anayejishughulisha na kinga, kugundua, na kutibu magonjwa ya kinywa na meno kwa watoto.
Dentist specialized in the prevention, diagnosis and treatment of bucco-dental diseases in children.

CONSERVATIVE DENTISTRY
Taaluma ya kutunza na kuziba meno 
Encompasses the dental procedures aimed at preserving, restoring and maintaining dentition.

ENDODONTICS
Taaluma ya kinywa na meno ya inayojishughulisha na kutibu jino kuanzia kwenye mzizi.
Branch of dentistry comprising the study and treatment of dental pulp nerves through root canals.

ENDODONTIST
Daktari bingwa wa kinywa na meno anayetibu meno kuanzia kwenye mzizi.
Dentist specialized in the treatment of the dental pulp and related complications.

PERIAPICAL SURGERY
Upasuaji mdogo wa uvimbe unaozunguka mzizi wa jino. 
Surgical technique to access and remove chronic lesions of the dental pulp (e.g., granulomas and cysts) that can affect the tissue or local structures of the dental root.

DENTAL AESTHETICS
Taaluma ya kinywa na meno inayojishughulisha na muonekano wa meno, kurekebisha rangi ya meno unaompatia mtu tabasamu linaloridhisha na kuendana na muonekano wa uso wake.
Branch of dentistry concerned with the appearance of teeth, improving the color, shape, contact area, texture and transparency of clinically faulty crowns to provide a smile in harmony with the face.

2 comments:

  1. This is a great inspiring article.I am pretty much pleased with your good work.You put really very helpful information. Keep it up. Keep blogging. Looking to reading your next post. Invisalign Milton Keynes

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.