Header Ads

Namna ya kupunguza tumbo la mama baada ya jifungua

Jinsi Ya Kupunguza Tumbo (BaadaYa Kujifungua)

Furaha kubwa ya mama mja mzito ni kumzaa mtoto aliye na afya njema na asiye na shida yoyote. Lakini kwa akina mama wengi, furaha hii hukatizwa na unene wa tumbo unaokuja baada ya kujifungua.Shida kubwa huwa ni tumbo ambalo ni nene kuuliko mwili. Sababu hii huwafanya akina mamawengine kutoupenda mwili wao.Kuna habari nzuri katika uandishi huu, kwani wataweza kujuajinsi ya kupunguza tumbobaada ya kujifungua.

Iwapo watayafuatilia maagizo haya vikamlilifu, basi unene wa tumbo baada ya kujifungua utaisha.

1- Kuwa na motisha
Ni muhimu kwa mama kuwa na motisha anapoamua kulipunguza tumbo baada ya kujifungua. Tena, anafaa kuwa na uvumilivu. Kupunguza tumbo hilo huchukua muda sawia na ule wa kubeba mimba. Kwa ufupi, inawezekana kwamba kama tu ilivyochukua miezi tiza kwa tumo kunenepa, itachukua miezi sawia kupungua.Hivyo basi, mama hafai kufa moyo au kuwa na haraka. Kuna uwezekano kwamba mama anaweza kufanya vitu ambavyo hakuzoea pale awali kama kufanyamazoezi, kuacha vyakula fulani na kuanza kuvila vingine. Hii ni safari inayohitaji motisha.

2- Kunyonyesha mtoto

Njia ya pili ya kupunguza tumbo ni kumnyonyesha mtoto. Ni asili kwa mwili wa mwanamke kurudia hali ya mbeleni pole pole baada ya kumzaa mtoto.Kwa mfano, mfuko wa uzazi hurudia hali yake ya kawaida. Vile vile, iwapo watakua na subira na kuwanyonyesha wanao, basi tumbo hurudia ukubwa ule wa awali.

3- Kuepukana na pombe

Iwapo mama anakunywa pombe kwa wingi baada ya kujifungua, ni ngumu kwa tumbo kurudi ukubwa ule wa kawaida. Pombe, pamoja navinywaji vyenye sukari nyingi, huadhiri njia ya ini ya kufanya kazi. Adhari mojawapo ni kutotengenezamisuli ifaavyo mwilini.Ini linapolemewa kuunda misuli, mwili hujaa mafuta na kusababishamtu kunenepa. Hivyo basi, mama anapokunywa pombe, sio tumbo tu linalonenepa; mwili wote huadhirika. Hivyo basi, unywaji wa pombe haufai baada ya kujifungua.

4- Kufanya mazoezi ya tumbo

Huenda ikawa vigumu kuanza mazoezi mara tu mama anapojifungua. Hivyo basi, ni vyema kusubiri mpaka mwili utakaporudia hali ya kawaida na kupata nguvu. Hata hivyo, mama hafai kufanya mazoezi mazito au mengi sana.Kwahivyo, anza kwa mazoezi madogomadogo yanayolenga tumbo. Kwa mfano, unaweza kulala kwa mgongo na kuyakunja magoti. Baada ya hapo, unauinua mwili wa juu polepole kisha kulala tena. Rudia zoezi hili mara kadhaa kwa siku. Kuna mazoezi mengi ambayo utaelezwa na daktari.

5- KutembeaKutembea ni aina ya mazoezi ambayo husaidia kupunguza tumbo.

Inawezekana kutembea kukaonekana kama mazoezi duni, lakini, husaidia sana kwa kulainishatumbo.Mtu anapotembea, misuli mingi mwilini hutumika, ikiwemo ile ya tumbo. Hivyo basi, mafuta yaliyokusanyika sehemu ya tumboni huisha na tumbo kupungua. Zoezi hili linaweza kukufaa sana iwapo utambeba mtoto wako mgongoni (kuongeza uzito).

6- Kufanyisha misuli mikubwa mazoeziHata ingawa lengo ni kupunguza tumbo, mama anafaa kuifanyisha misuli yote mazoezi.

Unapofanya mazoezi yalengayo tumbo pekee, mafuta huchomeka polepole mwilini.Iwapo unataka kulipunguza tumbo haraka, basi unaarifiwa kufanya mazoezi yalengayo misuli mikubwa mwilini. Hii ni kama miguu, mikono na mgongo. Hii itazuia kulipunguza tumbo na kubakia na mafuta (unene) kwingine mwilini.

7- Kupumua kwa undani

Zoezi hili ni rahisi sana na mama anaweza kulianza saa moja tu baada ya kujifungua. Mama anafaakuketi kitako na kuvuta hewa kwa ndani.Anapoivuta kwa ndani, anafaa kuukunjua mgongo na kasha kuifungia hewa ile kidogo tu. Kasha,anaitoa pumzi ile na kutulia kidogo, kasha kurudia. Zoezi hili husaidia misuli ya tumbo kulegeza na kumfanya kupona kwa haraka.

8- Kufunga kitambaa cha kupunguza tumbo

Hii ni njia mojawapo ya zile zinazotumika sana na ambayo imewkuwepo kwa muda mrefu. Muda mfupi baada ya kujifungua, kitambaa spesheli kilichotengenezwa kwa pamba hufungwa tumboni.Lengo la kitambaa hicho ni kupunguza kufura na kuirudisha misuli kuwa na ukubwa wa kawaida. Kwa kawaida, kitambaa hicho hufungwa kwa muda wa wikimoja kasha mama anapumzika kiasi na kurudia tena. Kitambaa chakawaida kilichoundwa kwa pamba kinaweza kutumika pia.

9- Kula chakula cha kutoshaKadri na maelezo fulani kuwa mama akila kiasi atapunguza tumbo, ni bora kuzuia njaa kabisa.

Kando na kutopunguza tumbo, njaainaweza kuzuia kupona kwa haraka.Mama anapokaa njaa kwa muda, kuna uwezekano kuwa atakula chakula kingi baadaye. Kula chakula kingi kutachangia kunenepa kwa tumbo.

10- Kula vyakula vidogo mara nyingi kwa sikuBadala ya kukaa njaa kwa muda kasha kula chakula kingi baadaye, ni heri kula vyakula vidogovidogo mara kadhaa kwa siku.

Hii inawezesha mwili kusiaga chakula chote bila kuhifadhi cha ziada kama mafuta mwilini. Nguvu itokanayo na kula vyakula vidogovidogo hutumika kikamilifu na kuzuia kunenepa tumbo na mwili kwa jumla.

11- Punguza vyakula vya ‘kujituliza’Kwa kawaida, mama anapojifungua, yeye hudaisha vitu kadhaa anavyohisi kwamba mwili unahitaji ili kuwa imara.

Baadhi ya vitu hivyo ni chakula.Shida ni kuwa, vingi vya vyakula hivyo huwa na sukari, mafuta na bidhaa zingine ambazo huongeza mafuta mwilini. Kwa mfano soda, keki, viazi, peremende na bidhaa zilizotengenezwa kwa ngano. Ni sawa kuvila vyakula hivi, lakini, vinafaa kupunguzwa muda uendavyo.

12- Kula vyakula vya mimeaUtafiti unaonyesha kuwa vyakula vya mimea (sio nyama) vina mafuta kidogo na madini mengi ya protini ya mboga.

Hivyo basi, vinapunguza kuongezeka kwa mafuta mwilini na kuzuia kunenepa.Akina mama wanahimizwa kujiepusha na kula nyama wakati huu na kula vyakula vitokanavyo namimea.Baadhi ya vyakula hivyo ni:*.Mboga kama mchicha (spinach), sukuma wiki na kabichi.*.Matunda kama machungwa, maembe, mapapai, tikitiki maji, parachichi, mapera na mengineyo.

13- Kupunguza kiasi cha chakulaMama anakubalika kula chakula zaidi ya kawaida anapokuwa na mimba.

Hii ni kwasababu ana binadamu mwingine ndani yake mwenye mahitaji mengi. Hata hivyo, baada ya kujifungua, anafaa kupunguza kiasi cha chakula alacho.Kula chakula ziada kinalifanya tumbo kuwa nzito na kukusanya mafuta. Hii huchangia kwa tumbo kukaa likiwa nene au kuzidi kunenepa.

14- Kula kiamsha kinywaKiamsha kinywa ni mojawapo wa mlo muhimu sana kwa mama aliyejifungua.

Anapokula kiamsha kinywa, mwili huchangamka na kusiaga chakula chote kikamilifu. Mwili pia hukaa tayari kuvipokea vyakula vingine wakati wa mchana na kuvisiaga vizuri.Mwisho kabisa, hakuna uwezekanowa mama kuhisi njaa kupita kiasi na kuchangia kwake kula kupita kiasi. Kwa njia hii, tumbo la baada ya kujifungua hupungua.

15- Kunywa maji baridi ya kutoshaMaji husaidia mwili wa mama aliyejifungua kupona kwa haraka.

Pili, maji hujaza tumbo na kuzuia mama kula chakula kingi kupita kiasi. Hivyo basi, anaweza kurejelea hali yake ya kawaida bila kuhisi njaa.Kunywa maji baridi kutasaidia kuchoma mafuta mwilini wakat mwili unapojikakamua kuyapa joto.Hivyo basi, mafuta yanatolewa mwilini na tumbo kupungua.

Ahsante

No comments

Powered by Blogger.