Header Ads

KUTUMIA AKILI ZAKO KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA SOMA HAPA





Sehemu ya 1 
TUMIA AKILI ZAKO KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA NA MWL MWAKASEGE (ARUSHA JAN 2017)




SEMINA YA NENO LA MUNGU ARUSHA UWANJA WA RELI
TUMIA AKILI KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA
NA MWL CHRISTPHER MWAKASEGE
15-JANUARY -2017
Bwana Yesu asifiwe watu wa Arusha, heri ya Mwaka mpya. Semina hii kwa mara ya kwanza iko live karibia asilimia kubwa ya nchi yetu kwa kutumia vituo mbali mbali vya redio (Tazama chini nimeandika)
Katika semina hii tuna malengo makubwa mawili
1. Kuweza kuona umuhimu wa akili na sehemu yake katika maisha ya kiroho.
2. Ili uweze kutumia akili kiroho ili ufanikiwe kimaisha.




_3 Yohana 1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo._
Mungu anataka ufanikiwe kila eneo sio kiroho tu bali anataka ufanikiwe kila eneo
Dondoo za somo
1.Tofautisha kati ya kuzitegemea akili na kuzitumia akili.
_Mithali 3:5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;_
_Mithali 23:4 Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe._
_Waebrania 5:14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya._
Wakristo wengi sana waliokoka wamekwama hasa kwenye eneo hili la kwanza, ile kwamba biblia inakataza kutegemea akili haina maana tusizitumie. Maana kuna tofauti kati ya kutumia akili na kutegema akili. Maana yake ni kuwa tegemeo na imani hazitakiwi kuwa kwenye akili inatakiwa iwe kwa Bwana katika Kristo Yesu. Ila Mungu katupa akili ili tuzitumie, maana kuna wapendwa wengi sana baada ya kuokoka wamemweka akili zao pembeni, kwa sababu wanaona kutumia akili ina maana hauna imani sio kweli na haiko namna hiyo inatakiwa utumie akili zako vizuri.
Huwezi kuenda kiroho bila akili, kwa hiyo kutumia na kutegemea ni vitu viwili, usivichanganye maana huwezi kwenda kiroho bila ya akili. Kwa hiyo hili ni jambo muhimu na jifunze kuvitenganisha kwa sababu unaweza ukatumia gari na huwezi weka imani yako kwenye gari kuwa litakufikisha salama. Ila unatumia gari huku tegemeo lako likiwa kwa Mungu.
2. Bila imani sahihi, akili zinafanya kazi kimwili badala ya kufanya kazi kiroho
_Wagalatia 3:1-3 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?_
Wagalatia walianza katika roho na waliondoa akili, maana hamna mtu aliumbwa hana akili, na wakawa wanazipita kama basi lililojaa na hawazitumii popote. Na anaposema Enyi Wagalatia msio na akili na waliondoka kwenye imani na walibaki na mapokeo na sheria za dini. Mtu yeyote aliyeokoka na akaacha kutumia akili anaanza kwenda kwa kufuata mapokeo na sheria ya dini. Maana ni hatari sana akili kukaa upande wa mwili, au wa adui kwa hiyo akili ili ziwe safi lazima ziende kiroho na ziwe upande wako.
Wachawi wakitaka kukukamata wanaanza kwa kuloga akili zako ‘’Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga’’ ina maana akili zao hazifanyi kazi ma wamekuwa wajinga kwa maana hiyo ina maana kuna kitu kimeondoka kwao. Kwa kawaida imani ndiyo inaunga akili na roho kwa hiyo kuondolewa kwa akili walikuwa wanakosa kitu kikubwa sana.




3 Akili yako isipotumika kiroho ipasavyo mafanikio yako ya kichumi yanakwama
Hapa tutaangalia mifano 3 mikubwa.
Mfano wa Kwanza
_Mithali 30:24-25 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari._
_Mithali 6:6-11 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha._
Biblia inasema chungu ni wanyama wadogo sana, hukusanya chakula wakati wa kiangazi ili watukitumie kipindi cha baridi, na biblia inasema hawana kiongozi na Mungu anasema kajifunze kwao. Kwa hiyo suala la kukosa akiba ni tatizo la kiakili maana ndivyo biblia inasema. Kwa hiyo kama chungu anatumia akili katika kuweka akiba iweje mwanadamu usiwe na akiba? Huweki akiba kwa kuwa unapata sana lakini kwa sababu unatumia akili.




Biblia inasema ewe mvivu mwendee chungu, na ukiwa mvivu kufikiria biblia inasema kajifunze kwa chungu. Kwa maana hiyo kuna matatizo ya kimasikini kwa sababu kwa kipato, bali ni kwa sababu ya kukosa nidhamu ya pesa.
Kinachomsukuma chungu kufanya hivyo ni mabadiliko ya tabia ya msimu, kwa sababu akili zimetengenezwa kukupitisha kwenye nyakati tofauti tofauti na kila wakati unakitu cha kufanya kama hari kwa chungu ni kuweka akiba.
_Mithali 24:30-34 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha._
Umasikini umempata kwa sababu amelima shamba bila kutumia akili, na alishindwa kupalilia na anaona ukuta umebomoka na wanyama wanaharibifu wanapita hapo na yeye anaanza kuomba kuwa Bwana asipojenga mji, sasa kama hajajenga, au unafikiri wa kukujengea huo ukuta ni nani, ni vizuri sana kutumia akili zako.
Mtu baada ya kuokoka anapoteza ushuhuda, unakuta mtu shamba lake hapalilii na unamuliza kwanini anasema ooh nilibanwa na maombi, mara ooh nilikuwa kuhubiri mara nilikuwa kanisani sasa biblia inakusaidia kukuita mvivu na hauna akili na kukuambia kuwa huna akili sio tusi bali ni mazingira uliyoyafanya baada ya kuweka akili pembeni na unakwama kimaisha.
Mtu yeyote anayefuatilia masuala ya uchumi wa nchi Tofauti tofauti na unagundua tatizo ni tofauti za kufikiri kwa watu waliko katika nchi na ukitaka kujua tofauti ya nchi na nchi kimaendeleo ni namna ya kufikiri. Ukienda nchi za nje na wakagundua kuwa una akili watatamani sana ubaki katika nchi yao na mtu mwenye akili anapata shida sana anapokosa muda wa kufikiri. Fanya kitu chochote bila kutafakari, itakupa shida sana.
Mungu hakutuumba tuishi kwa muujiza bali kwa neno na ndani ya neno kuna maelekezo ya namna ya kufanya , na kilichosababisha ni muujiza ni dhambi. Mungu anaingilia kati mazingira yanayokwamisha wewe kupata kile Mungu anataka.
Sasa unaweza ukaelewa kwa wale wapelelezi waliposema kuna watu wakubwa, na Mungu anakupeleeka kwenye nchi ambayo inawatu wakubwa, lakini kuna sehemu Mungu anataka makae kwa pamoja ili Mungu aweze kushiriki na kukusaidia, dhambi ilipoingia ndipo ilituvuruga.




Wale watu ambao hawajaokoka wanatumia akili sana na wanafanikiwa ila wanafanikiwa kipumbavu, maana biblia inasema kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamaiza. Kwa sababu unafanikiwa na mbinguni huendi, na utoaji wako unapata shida unafanikiwa na unamaliza wengi na kwenye shughuli za kimungu huonekani. Na kama ulizipata kwa nia nyingine jua kabisa shetani hawezi kupa pesa ili kubomoa ufalme wake mwenyewe lakini umetumia akili na umefanikiwa, na umetumia akili nje ya kiroho namna Mungu alivyokusudia
Ndio maana hata maneno kwenye biblia hayamo na yamefichwa ili kubeba uzito wake. Nilisoma kuanzia mwanzo hadi Ufunuo natafuta neno maendeleo sikulipata, nilitafuta biblia za zamani na za kiingereza ndio nikapata neno nuru maana maendeleo yanayoleta giza au kaharakisha dhambi siyo ya Kimungu. Hivyo Mungu aliposema kuwe nuru ina maana kuwe na maendeleo. Na maendeleo sio kuwa na pesa maana biblia inasema uzima wa mtu haupo katika wingi wa vitu alivyonavyo.
Zipe kazi akili zako na umewahi kufikiri Mungu anakuonesha sehemu kuwa 10% ndio ulitumia akili na 90% akili yako haikutumika na kwa sababu hiyo vitu vyote nilivyoviweka kwenye 90% hukuweza vitumia utasema kama yule tajiri kuwa wale ndugu zangu kule duniani watumie akili zao ipasavyo.
mfano wa pili
Usipotumia akili yako vizuri unashindwa kupenda ipasavyo
Yesu alipoulizwa habari za amri kumi kwenye _Mathayo 22:37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote._ Biblia inatoa ufafanuzi wa namna ya kumpenda Mungu, kwa maana hiyo huwezi kumpenda Mungu kwa roho tu bali inatakiwa umpende Mungu na kwa akili pia Katika _Warumi 5:5 na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi._
Roho Mtakatifu alileta kitu kwetu cha kumpenda Mungu, japo kuna roho ndani yako ambayo inapendo la Mungu, lakini pia na akili zote zitume kumpenda Mungu na moyo wako wote.
_1Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe._
_Tito 2:3-4 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;_
Weka akili pembeni kwenye ndoa ujue hiyo ndoa inakufa, kwa sbabu wapendwa wanatakiwa wapendane kiroho, biblia inasema kaa na mke wako kwa akili na sio kiroho. Na wapendwa wengi wanapenda kiroho na akili hazipo, na wanakuwa na shida sana. Na Roho Mtakatifu anapoingiza akili unamuona mwenzako hayuko kiroho, na akili lazima zikubali kuelewa maana biblia inasema walifuniliwa akili zao ili waweze kuelewana na maandiko.
Maana unakuta mpendwa anaaga kuwa mwezie kuwa leo ntachelewa kurudi amina, mwenzio anataka kujua kwanini utachelewa na je hilo huwezi lifanya kwa muda mwingine na akikuuliza hivyo unaanza kusema huniamini hapana sio hakuamini inatakiwa unyooshe maelezo kwanini utachelewa. Pia unasema nimepata 20,000/- napo anataka ufafanuzi ili kuweza kuelewa vizuri umeapata wapi hizo hela.
Ndoa zinakufa kwa sababu pendo linapotakiwa kuhuisha akili ila linauka akili, si mnasikia huku mjini watu wanasema nimependa hadi akili zangu hazifanya kazi. Huwezi sema umependa hadi akili zako hazifanya kazi, bali inatakiwa ukipenda na akili zako zifanye kazi na ndipo upendo unakuwa na maana.
Sio chepesi kama tulivyosema, maana tunapata mafundisho upande mmoja tu kuwa kilitokea nini dhambi ilipoingia na tunashindwa kujua baada ya kuokoka tunatumiaje akili ili kuweza kutumia akili vizuri ili zikae upande wa Mungu.
Mfano wa tatu
Akili isipofanya kazi kwenye eneo haki inapotea
_Mithali 28:16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake._
Ukiona kiongozi anakunyima haki yako ya msingi usianze kukemea pepo bali ombea akili zake maana ndiko kuna shida. Kwa maana hiyo ina maana kapungukiwa na akili kwa sababu kama unaweza jua kuwa kuna upungufu wa akili ina maana kuna kipimo cha akili. Ina maana wakitumia haki pungufu wanaonea watu kwa sababu akili zinatumika kwa kiwango kidogo. Ni jukumu lao kuweza kujua hiki kitu ninachokufundisha kuwa ni akili ya kiwango kipi inayotakiwa kuweza kumpa mtu haki yake.
Mfano wa nne
Akili isipotumika kiroho unashindwa kuunganisha maisha ya kiroho na maisha ya kawaida
Luka 24:44-49 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.




Kabla ya ahadi hizo za Roho Mtakatifu Mungu aliwapa uwezo katika akili zao ili waweze kelewa maandiko. Kwa hiyo ufunuo unapokuja lengo lake ni kuzifanya akili zako zielewe maandiko na uweze kuhusianisha na mazingira ya kawaida na maandiko. Ndio maana walihitaji ufunuo katika akili zao ili waweze kuelewa Torati na Zaburi. Ili waweze kuunganisha na mazingira waliyokuwa wanayaona yaani akili zielewe kitu cha kiroho na kukileta kimwili.
Watu wanapotazama biblia na maisha yao ni tofauti, na wanapotazama maisha yao na maandiko yako tofauti yaani eidha watarudi nyuma au watapoa kiroho na kwa kuwa wanaogopa kuonekana wamerudi nyuma wanabaki wanafunzi wa Yesu na sio mashahidi , ili wajue kuwa huyu ndiye Yesu ambae habari zake zilinenwaa. Na wanabaki wakristo kawaida na hawaelewi maandiko na hata waliokoka waliotakiwa kuelewa maandiko hawaelewi maandiko maana wanajua wakiwa na upoko basi wataelewa maandiko, enhe haiendi namna hiyo. Na ukiweka akili mahali zinapotakiwa maandiko yatazungumza sasa na biblia haitakuwa kitabu cha dini au historia maana ni maelekezo ya Mungu.
Biblia ni maelekezo ya Mungu kwa wanadamu, angalia tena _Waebrania 5:14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya._.
Mungu alipomleta mwanadamu duniani alitegemea atumie akili ili kupambanua mema na mabaya. Na ndio maana alimuwekea mti, lakini Adam na mke wake hawakutumia akili na ndio maana walipata confusion na yale mabaya walisema ni mema na mema yakawa mabaya. Ndio maana biblia inasema aliwafunulia akili zao ili waweze kelewa maandiko. Shetani akitaka kuzuia watu wasiokoke anapofusha akili zao isiwazukie nuru ya Injili na Mungu akitaka kukuokoa huwa anakufunulia akili zako ili uweze kuelewana na maandiko. Na shetani akikuchanga anasema hii ni 6 wakati 9 anasema njoo utazame kwa hapa na wewe unasema ni kweli kwa sababu imeguzwaa. Na anakuondoa kwenye position yako ya kutazama.
Funika macho yako, hii ni neem asana kwa Mungu kauachilia somo la jinsi hii. Na Mungu anataka kukupeleka hatua nyingine na ndio maana Mungu anataka uokoke na anataka akaufundishe ili akili zako zifanye kazi. Mungu uliyehai katika jina la Yesu, naomba tembelea watu wako waliokuwa wamerudi nyuma au walikuwa hawakujui.ee Mungu wasaidie watu wako waseme ndio kwako maana mafanikio yao wamejitahidi kukutafuta na wameona hawasogei na Mungu wavute tena kwa upya ili wajue ni kitu gani kimepungua ili waziingize akili zao kazini kama ilivyokusudiwa. Shetani achia akili zao ili nuru ya injili iweze kuwazukia na nanyunyiza damu ya Yesu ili kuondoa huo utando ili waseme ndio kwa Yesu. Munguwape neema hiyo ili wapate kujua thamani ya wokovu.




Naongea na wewe ambaye hujaokoka yaani Yesu hajawa Bwana na mokozi wa maisha yako, inawezekana una matendo mazuri lakini unamhitaji huyu Yesu maana hatuendi mbinguni kwa kuwa na matendo mazuri bali imani.
Click maandishi haya ili kuungana nasi kwenye sala tuliyoifanya pale uwanjani.
Yesu akamwambia "Lisha Kondoo Zangu" (Yohana 21:17)- MANA TANZANIA
Soma kitabu cha hongera kwa kuokoka.
Yesu akamwambia "Lisha Kondoo Zangu" (Yohana 21:17)- MANA TAN

No comments

Powered by Blogger.