IZZO BIZNESS-HAKUNA KITU KITAKACHOIYUMBISHA “THE AMAZING”
kundi hilo limejipanga kukabiliana
na changamoto ambazo zimekuwa zikiyakabili baadhi ya makundi mengine ya muziki
hapa nchini.
Staa huyo na rapper ambaye
ameshirikiana na muimbaji, Abela kuunda kundi hilo, amesema kabla ya kuunda
kundi hilo walika chini na kuangalia namna ambavyo wataweza kukabiliana na
matatizo.
“The Amaizing tumejipanga kupambana
na changamoto zote, mpaka kuja au kufikia maamuzi ya kuungana na kuanzisha
kundi tayari tumeshasomana tabia, yaani sisi tuna mengi ambayo tuliyaangalia,
kwahiyo naweza sema tupo vizuri tunaomba Mungu atusimamie tu,” amesema Izzo
Rapa huyo amesema, muziki kwa sasa
umebadilika na kuwafanya wasanii kuacha kutegemea show pekee.
“Kwa sasa ukifanya muziki mzuri
utaona matunda ya muziki wako kwa sababu sasa hivi wasanii hatutegemei shows
tu, watu wanapata deal kubwa za kupiga show za mkampuni, endorsement na mambo
mengine. Kwahiyo mimi naona kuna mashavu mengi sana kwenye muziki kama ukiandaa
kazi nzuri,”
Post a Comment