ALIKIBA, MR BLUE KUMRUDISHA ABBY SKILLS
Msanii ambaye alifanya vizuri
kipindi cha nyuma na nyimbo ‘Maria’ na ‘Mimi na Wewe’ Abby Skills anajipanga
kurudi upya katika game la muziki na wimbo ‘Averina’ akiwa na Ali Kiba.
Staa huyo wa muziki nchini amesema,
AliKiba na Mr Blue ndiyo watu ambao wanamsimamia kwa sasa ili kumrudisha upya
kwenye chati ya muziki nchini.
“AliKiba na Mr Blue walikaa chini na
kuamua kunisaidia kunirudisha kwenye game, waliniambia tumeona una kipaji
kizuri, una melody ngoja tushirikiane ili kukupeleke sehemu fulani,” amesema
abby Skills.
“Hata hii project yangu mpya na
AliKiba ‘Averina’ wao ndio wanasimamia kila kitu, kwa hiyo kuna mambo mazuri
yanakuja hivi karibuni na mashabiki wangu kaeni mkao wa kula,” aliongeza abby
Skills
Muimbaji huyo amesema, kazi yake
mpya aliyomshirikisha AliKiba itatoka hivi karibuni kwa kuwa tayari ameshashoot
na video.
Post a Comment