Bambucha sehemu ya 1
Eliado Love Stories
CHOMBEZO: BAMBUCHA
SEHEMU YA 1
MTUNZI: ELIADO TARIMO
MAWASILIANO: 0714 555 195
UMRI: 18+
Maisha safari japo si lazima ianzie stend. Dunia
ina mambo tena vijambo toka kitambo. Eti
ikisimama panda, ukipendwa penda.Mimi sio
fumbo usiangaike kunifumbua mimi ni zawadi
ikiweza nifungue.Nimezaliwa na ulimbo ukigusa
utanata,ukinitaka utanipata.Pesa ndo kila kitu
ukiwa nayo utakula kuku mpaka bata. Maisha si
lele mama ukishikwa shikamana.Dunia kweli
kizingumkuti japo si jumba la makuti. Mungu
nikijikuta nimeathirika nipe hata umauti maana
sitaki kukonda kama kijiti. Yaani Sukari nigueke
ugali, hili silitaki hata kwa mali.Mungu nipe
heri,niepushe na shari, nataka kutoa funzo kwa
Watanzania na walio mbali.Ukiona ghali gharama
basi tafuta vya kuparama.Ila chunga sana usije
kuniparamia maji utaita mmmmaaa.Mimi sio wa
jana wala juzi mimi ni wa enzi nakula visivyoliwa
na ninanyoa zaidi ya kinyozi.Aaaaaaaaaaah wacha
nicheke mie eti unielewi kwa yangu misemo.Mimi
sio mzaramo mimi ni mpogoro wa kule Mahenge
Morogoro. Mimi sina soni kama mvivu wa
kusoma, leo utakoma,sikuchambi wala sipiki
tambi,sitaki rambi rambi, refa kashapiga filimbi
weka sikio nikupe na moyoni.
Najua ushadata kwa Eliado kunipa nafasi kwenye
ukumbi huu matata wa visa na visasi. Wacha
nijinafasi mie, maisha yenyewe mafupi,kuna utamu
uchungu na ukakasi.Mimi ni mshabiki wake wa
mda mrefu japo si mrefu napenda sana kusoma
simulizi zake kwa kina na marefu. Leo nimeona si
mbaya bishosti mimi mama la mama, mutoto ya
mujibu kuwasimulia yaliyonikuta maishani .Japo si
mabaya wala mazuri ila naamini mtajifunza
yanayojiri huku duniani. Naitwa Bambucha, ndio
Bambucha kinachokufanya ushangae ni
nini?.Bambuha maana yake kubwa kuliko (Extra-
large).Ndio hivyo nimejaliwa mwenzenu yaani ya
kwangu kumbwa kuliko alafu tamu kama asali.
“Mwone ushaanza kuwaza ujinga japo ni
mjanja”,mwenzio nimetania maana fupi tamu ndefu
inakera ila hii simulizi ni Bambucha. Kama huna
pesa weka mbali na watoto wenzio wananijua
ikisimama panda si kuku mimi ni bata mzinga. Ila
majina yote haya si niliyopewa na wazazi wangu
bali ni niliyopewa kutokana na kazi yangu.Sasa
sitaki maswali subiri nikupe asali.Siunajua tena nzi
naye akiacha ujinga siku moja atatengeneza asali.
Sina shombo la samaki, mimi ni nanasi wewe nipe
nafasi, nisome mwanzo mpaka mwisho.
Mimi wa kitambo kidogo maana nimezaliwa miaka
30 iliyopita kaatika kijiji cha Kwiro huko Mahenge
Ulanga Morogoro.Wazazi wangu waliponizaa tu
waliniita Vaileth.Nasikitika jina hili limekufa,
kuzikwa na kusaulika.Sasa naitwa Bambucha
mama la mama, bishosti wa mujini ninayekula kwa
akili. Mwenzenu nilizaliwakwenye familia ya
kimasikini sana. Familia ya mzazi mmoja tu yaani
mama yangu ambaye alikuwa maarufu kwa jina la
mama Vai kifupi cha Vaileth. Sikuwahi kumjua
baba yangu mpaka leo hii nimefikia umri
huu.Mama yangu naye ni moja ya watu ambaye
historiayake nayo ilikuwa ngumu sana. Kwa mujibu
wake ni kwamba hata yeye alikuwa hawajui wazazi
wake.Inasemekana walifariki yeye akiwa mdogo
kabisa. Baada ya hapo alilelewa maisha ya kuunga
unga mpaka hapo alipojitambua. Hakuweza
kusoma zaidi alipata tu elimu ya kufuta ujinga
nakwa maneno mengine naweza kusema aliishia
darasa la saba.
Katika harakati zake za kutafuta maisha ndipo
akaamia hiyo sehemu ambayo kilichompleka hapo
ni shughuli ya kuuza chakula.Yaani alikuwa ni
mama ntilie maarufu sana ukanda huo ambapo pia
shule ya sekondari ya wavulana Kwiro ilikuwa
ikipatina. Kwa Mujibu wa mama yangu ambaye
kwa sasa ni marehemu ni kwamba eneo hilo pia
kwa mbele kunapatikan madini aina ya Ulanga na
rubi. Hivyoo kufanya watu wengi sana kuja huko
kujitafutia maisha.Hivyo mama yangu alifanikiwa
kukutana na bwana mmoja mchimba madina
ambaye alitokea kumpenda sana. Mama yangu
anasema kipindi hiko kilikuwa ni kigumu sana
kwake hivyo ikamlazimu pia kuwa mjanja mjanja ili
kufaya maisha yake yasonge. Anasema hakuwa
akijiuza maana tayari alikuwa na biashara yake ya
kuuza chakula na kujipatia kitu kidogo. Lakini
kama alitokea mwanaume mwenye fedha za
kutosha hakuacha kumchuna na kuendeleakupamb
ana na maisha.
Katika miangako hiyo ndipo alikutana na
mwanaume wa mgodini.Upendo ukakolea na
hatimaye akabeba mimba yangu. Anasema
bwanahuyo siku za mwanzo alioneshaupendo wa
hali ya juu sana lakini baadaye alipomwambia ana
ujauzito bwana huyo aliruka viunzi. Mama yangu
alikomaa hivyo hivyo mpaka akajifungua. Basi
nilivyozaliwa mama yangu akaendelea kupambana
na maisha. Mama yangu naye alikuwa ni mzuri
tena mzurii wa asili. Hali hii ilimfanyia pia
wanafunzi wapapatike sana naye. Pia hakuacha
kuwachuna. Ikawa mradi tu mwanaume na pesa
nzuri basi alimkubali. Mama yangu aliaapa kunilea
na atafanya lolote ilimradi tu nisome na nije kuwa
mwenye mafanikio makumbwa sana duniani. Maiha
yakaendeea na mimi nikaendelea kukua.
Lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa mkumbwa kuna
tofauti kidogo ilitokea. Yaani mwili wangu ulikuwa
ni mkubwa hata matiti na makilio yaliaanza
kuonekana nikiwa kwenye umri mdogo sana. Hali
hii haikumshangaza sana mama yangu maana hata
yeye alikuwa si haba alijaliwa kiukweli kwa maneno
mengine yaliyomo yamo. Nikiwa tu darasa la tano
nikaanza kuwa kivutio cha wanaume wengi sana
hasa hao wa kutoka Kwiro Boys. Mama yangu kwa
kuwa alikuwa akizijua tabia za wanafunzi hao na
kwa jinsi wanavyoweza kutumia fedha zao
kumlaghai alianza kunipa mafunzo ya kiutu uzima
ambayo aliamini kuwa yatawea kunisaidia na
kujitambua. Alinambia kuwa wanaume ni watu
wabaya sana na ndio maana hata baba yangu
alinikataa. Taratibu taratibu akaanza kunijenga
kisaikolojia na kuanza kuwachukia wanaume.Kwa
hiyo nikawa wa kujitenga na kuwaepusha na
wanaume wasio kuwa na aibu ambao walianza
kuninyemelea nyemelea bila hata aibu. Hatimaye
Mungu naye akawa ananilinda mpaka nikafanikiwa
kumaliza darasa la saba salama.
Hapo sasa uzuri wangu huu wa kibantu ulianza
kuonekana.Mtoto mdogo makalio
makumbwa,chuchu ndo usiseme kama embe dodo.
Miguu mizuri wenyewe waliita ya bia, sura kama
ua ukicheza utajichua,umbo lenye mvuto mapozi
utafikiri mtoto wa kishua. Kweli asante Mungu
maana ulininyima vingine ukanipa uzuri.Mimi
mzuri bwana,niliumbwa nikaumbika,sipigi
napigiwa. Aaaah mshaanza kuona wivu vingine
utani tu.Sasa hapo ndipo nilianza kuyastaajabu ya
dunia, mibaba mijitu nzima ilianza kunisumbua.
Nikawa naachiwa mpaka chenchi hapo kwenye
kibanda cha mama.Kule shuleni Kwiro ndo usisme
nikifika mimi na utoto wangu wauzaji wengine
ilibidi wasubiri mpaka nimalize. Mama yangu
alikuwa mwenye furaha sana maana biashara yake
ilichanganya. Jina la Vai likawa kubwa sana na
hakuna hasiyenijua. Kibalehe cha kwanza
nachenyewe kiliniwahi sana nikajikuta naanza
kusahau maonyo aliyokuwa akinipa mama.Nilitaka
na mimi nijaribu hayo mambo ambayo mama kila
siku alaikuwa akinikataza.
Kipindi hicho cha kusubiri matokeo ya darasa la
saba kilikuwa kigumu sana kwangu. Wanafunzi wa
Kwiro, walimu na hata wananchi wengine kila
mmoja alikuwa akinitaka ili anionje na kuniingiza
kwenye ulimwengu wa mapenzi. Ilikuwa ngumu
sana kwao kutokana na uwoga ambao mama
yangu alinijaza. Mama yangu alidiriki
kuniambiakuwa yeye ni muathirika hivyo nikicheza
na mimi nitapata ukimwi. Nikweli mama yangu
alijikwaa lakini kwa bahati nzuri mimi alinizaa
nikiwa salama bin salimini.Siku moja majira ya sa
mbili usiku ilisikika sauti kutoka shule ya
sekondari ya wasichana St Agness ambayo ilikuwa
ikiangalia na hiyo ya Kwiro Boys kuwa kuna moto
ulikuwa ukitokomeza majengo yao.Basi Mama
yangu na yeye alitoka kwenda kushuhudia na
kuniacha mimi nikiwa nimelala. Kwa bahati nzuri
au mbaya na mimi nilishtuka kutoka usingizini na
kusikia kilele hizo za wanafunzi wa kike.
Basi kwa kiherehere changu na mimi ilibidi nitoke
ili kujua nini kinaenelea. Uzalendo ukanishinda
kelele zamabinti hao zilikuwa juu nikasema ngoja
na mimi niende kujionea sio kesho nasimuliwa.
Siunajua tena mwanamke umbea babuu eeeeh.
Sasa kwa mahali ambapo sisi tulikuwa tunaishi
ilikuwa ni lazima uzunguke Shule ya Kwiro au
upite katikakati.Kwa kuwa nilikuwa na haraka
haraka zangu niliamua kupita katikati japoilikuwa
ni usiku. Ile nakatisha kwenye migomba nilisikia
kama sauti za wanaume lakini niliona kwa kuwa
wananjua hamna shida ngoja niende tu. Masikini
ya Mungu nilishtukia nimepigwa mtama
nikadondoka chini na kabla sijakaa sawa
nikavutiwa migombani..Walinibeba wanaume kama
watatu juu juu na kuanza kunipeleka nisipoapajua.
Nilipiga kelele lakini kelele zangu zilizuiliwa na
wanaume hao ambao walikuwa wamejazia vizuri
misuli utazani wacheza mieleka.
*******ITAENDELEA********
Post a Comment