Header Ads

Supastaa sehemu ya 5

Simulizi za Nyemo
NYEMO CHILONGANI
SUPASTAA-05
ILIPOISHIA
PHIZA: (Anatoa tabasamu pana, anaonekana
kukumbuka kitu, tabasamu linapotea,
anakiinamisha kichwa chake chini, anapokiinua,
anashusha pumzi ndefu)
Leah na yule mtoto wake anayeitwa Phillip Jr,
yaani akimaanisha Phillip mdogo badala ya mimi
mkubwa. Daah! Hii ni stori ndefu na yenye
kusisimua sana, sikutaka nielezee kabisa, ila ngoja
niseme ili kila kitu kiwe wazi.
SOFIA: Sawa.....tunakusikiliza.
PHIZA; Koh koh koh....ooopppsss....!!!!
ENDELEA..
PHIZA: Leah alikuwa miongoni mwa wanawake
wazuri ambao nilibahatika kuwa nao. Alikuwa ni
msukuma aliyeumbika kwa kila kitu, kwa nyuma,
alikuwa amejazia huku kifua chake kikimvutia kila
aliyemuona.
Nakumbuka siku moja nilikuwa Mwanza, na ndiyo
ilikuwa siku ya kwanza kuonana na huyu Leah,
nikatokea kuvutiwa naye kwa sababu umbo lake
kwa nyuma lilinipa shida sana. Aliponiona, Leah
akatokea kuvutiwa na mimi, sijui kama mimi ni
handsome au alivutiwa na ustaa wangu, ila
akanipenda na siku hiyo nikaomba kuonana naye
faragha, akanikubalia.
Kwa hiyo ikawa hivyo, nikaanzisha mahusiano na
Leah, nilipoona kwamba kwa Mwanza ilikuwa mbali
sana, nikamuhamishia Dar ili niweze kuwa karibu
na tunda langu. Sikutaka awe nyumbani kwangu,
nikampangishia nyumba nzima maeneo ya
Kijitonyama.
SOFIA: Kwa nini hukutaka kukaa naye nyumbani?
PHIZA: Mimi ni mzee wa majanga, kama
ningekubali kukaa naye nyumbani basi kuna siku
ningetoa boko tu. Sikuwa mtu wa kutulia lakini kwa
Leah, kiasi fulani nilitaka kutulia kabisa kwani kwa
muonekano wa nje, alikuwa msichana ambaye
nilikuwa nikimuhitaji ukiachana na Stellah.
Wakati mapenzi yamepamba motomoto, kuna siku
nikaanza kusikia tetesi.
SOFIA: Tetesi gani?
PHIZA: Kuna msanii mmoja naye alikuwa akimega
kisela kwa Leah. Kwanza nilikasirika mno,
kumegewa mtu wako na wakati una kila kitu, hizo
ni dharau, kingine mtu aliyekuwa akimmega
alikuwa wa kawaida sana, japokuwa alikuwa staa
lakini hakuwa na fedha kama nilizokuwa nazo,
hivyo nilimmaindi na kuamua kuachana naye.
SOFIA: Hukukaa naye kulizungumzia hilo?
PHIZA: Kukaa ilikuwa ngumu, nilikuwa bize sana
huku nikiwa mtu mwenye hasira, baada ya
kuambiwa hivyo sikutaka kuchukua uamuzi wa
haraka nikaanza kuchunguza na mwisho wa siku
nikawafuma pamoja kule Msasani Beach. Niliongea
kiutaratibu na huo ndiyo ukawa mwisho wa kila
kitu.
Baadae kabisa nikasikia akisema kwamba alikuwa
na mimba yangu na alijifungua salama, mara ya
kwanza nilihofia lakini baada ya kuyakumbuka
majanga yangu, nikasema sawa, kama vipi
tukapime. Kweli tulikwenda kupima na kugundulika
kwamba hakuwa mtoto wangu.
Sikutaka kulizungumzia hilo kwa kuwa niliamini
ningemchafua, sikutaka achafuke kama
nilivyochafuka, nilitaka aendelee na maisha yake
bila kujisikia aibu mitaani. Sikuhusika naye, na
hata baada ya kodi kuisha, sikutaka kumlipia. Pia,
hata gari langu sikutaka nilichukue, nikamuachia
aendelee kuwa nalo, nadhani atakuwa ameliuza.
Hayo ndiyo yaliyotokea kwangu na Leah.
SOFIA: NA vipi kuhusu Bertha, hakuendelea
kukusumbua?
PHIZA: Hahaha! Nilimwambia kwamba nilikuwa
tofauti sana na wanaume aliokuwa nao kabla,
nilimpenda na kumthamini mno, nilipomuacha,
alijitahidi sana kutaka kujirudi lakini sikuwa tayari
kwa hilo, niliamua kwamba ninataka kuwa peke
yangu tu.
Baadae ndiyo likaja suala la kuwatukana sana
wazazi wangu mpaka kutaka kumlipua kwa risasi,
alinikasirisha sana. Alipokuwa akiwatukana wazazi
wangu, nilikumbuka kipindi kile walipokuwa
wakipata shida kisa mimi, nilikumbuka kipindi kile
walipokuwa wakifanya kila liwezekanalo kisa mimi,
halafu leo mtu aje kuwatukana kizembezembe,
nilikasirika sana.
Baada ya kupita kipindi fulani, nikakaa chini na
kujitafakari sana kwamba kama kutembea na
wanawake, nilitembea wa aina zote, wanawake
wote wazuri unaowafahamu wewe, nishatembea
nao. Nimetembea na waswahili, wazungu, wahindi,
waarabu na wengine wengi, nikajiuliza, nilipata
nini? Kuna faida niliipata? Jibu likaja kwamba
hakukuwa na nilichokipata, hivyo nikaamua kutulia
na kufanya muziki.
Nilijitanua zaidi na kupiga mpunga wa maana,
biashara zangu zikakua na nilifanya sana shoo za
nje. Kuna kipindi nilitaka kuwanunulia wazazi
wangu magari ya kifahari, wakasema hawataki
magari bali walitaka fedha hizo za magari
niwajengee nyumba nyingine kwa kuwa ingekuwa
ni faida kwangu pia, nikawajengea.
Kuna wamama wengi ambao wanapenda
kununuliwa magari na watoto wao, lakini wangu,
waliona magari si kitu chenye faida, leo zima na
kesho bovu na mwisho wa siku linatelekezwa
gereji, lakini kwa nyumba, ilikuwa ni hazina tosha,
hivyo nilifanya hivyo na wao kuwapa gari la chini
sana la milioni nane.
SOFIA: Kwa hiyo wewe na Stellah inakuwajekuwaje
?
PHIZA: Kiukweli ninataka kumuoa, nikisema
kwamba ninataka awe mpenzi wangu tu, nitakuwa
najidanganya. Nimepanga kumuoa na kuishi naye
na ndiyo maana mambo ya kuwavua wanawake
sketi nimeachana nayo.
SOFIA: Una ujumbe gani kwa Watanzania?
PHIZA: Wajitume, mafanikio hayaji kiwepesiwepesi
kama wengi wanavyofikiria, mafanikio huwa
yanapatikana kwa watu wanaopambana tu. Ili
uyafikie mafanikio, yakupasa kujituma sana. Tatizo
letu ni moja sana, wengi tunatamani kuwa na
mafanikio lakini hatutaki kufanya vile vitu ambavyo
vinaweza kutupa mafanikio.
Mbali na hivyo, starehe zimekuwa nyingi sana.
Kwenye historia ya maisha yangu, utagundua
kwamba kila nilipofanya starehe, sikupiga hatua
kubwa ila nilipoacha, fedha zilikaa na nilipiga hatua
kubwa.
Kama unafanya starehe na kununua gari ya milioni
tano, amini kwamba usingekuwa mtu wa starehe
ungenunua hata gari la milioni kumi na tano.
Tubadilike tu na tumuamini Mungu. La mwisho
labda ninapenda kuwakaribisha katika harusi yangu
nitakayofunga na Stellah mwezi ujao katika Kanisa
la Praise And Worship pale Mwenge.
SOFIA: Ninashukuru kwa muda wako.
PHIZA: Nashukuru pia.
Kipindi kinakwisha.
MWISHO.

No comments

Powered by Blogger.