Header Ads

Mchachuko sehemu ya 9

MCHACHUKO…(9)

MTUNZI…EMMANUEl

ILIPOISHIA

Adrian aligeuka na kuteleza alisimama haraka haraka na kuanza kukimbia ila mbele alikutana na Samia akiwa na mtu mrefu sana kwenda juu.
“ha ha ha ha ha ha h ha ha ha ha ha ha”
Jitu hilo lilicheka kwa sauti ya kukwaruza sana na kumfanya Adrian azidi kutetemeka mwili mzima.

SONGA NAYO

“Bosi Bosi”
“niachie niachieeee”
Adrian aliruka na kuparamia meza na kuuendea mlango mbio baada ya kushtuka katika njozi ile ya kutisha, mapigo yake ya moyo yalimwenda kasi sana, sababu ya kuota ndoto ile ya kutisha.
“bosi una tatizo gani”?
“hakuna kitu usijali”
“hapana niambie”
“hakuna kitu Martha, ndo muda wa kuondoka huu?”
“ndio muda umeenda sana”
Adrian alishusha pumzi ndefu sana na kuanza kutoka nje  kuliendea gari lake akiwa mwenye mawazo mengi sana, kabla ya kuingia ndani ya gari alitoa simu yake baada ya kuona ujumbe wa simu.
“BABY NINA MIMBA YAKO,ALAFU SINA KITU”

Ulikua ni ujumbe kutoka kwa Rebeca mwanamke wake aliye kutana nae Moshi Mwika kikazi baada ya kulala nae siku iyo alivyotoka disco akiwa amelewa, alivuta kumbu kumbu sana kabla ya kufungua mlango wa gari kisha kupiga namba zile.
“sasa huyo mtoto utakae mzaa tumuite kimario au Mwantumu”
“nani aliye kwambia nataka majina, nataka mahitaji”
“hivi ngoja nikuulize kitu wewe mwanamke wa kichaga, ulidhani siku ile nili lewa si ndio, nakumbuka nilitumia kinga sasa iyo mimba ime pitia wapi”?
“lakini lakini”
“embu achana namimi tena unikome shenzi wewe”
Adrian alimaliza na kukata simu kisha kuingia ndani ya gari na kuanza kuondoka taratibu, kulikua kuna foleni sana alichukua simu yake na kuanza kuangalia vitu mbali mbali kisha kutua kwenye jina Fiona , alivyoangalia Watsap aliiona picha yake akiwa amevalia kimini amelala kitandani, aliiweka picha hiyo vizuri na kuitizama kwa makini.
“MAMBO”
ALianza Adrian na kuona upande wa pili upo online kuashiria kua ujumbe unasomwa kisha baadae aliona typing.
“POA , NANI”?
“AAAH TAFADHALI BWANA,LAKINI UMEPENDEZA, HAPO WAPI”?
“KWANI WEWE NANI”?
“HUONI DP”?
“MI NAONA PICHA YA GARI, KWANI WEWE GARI”?
“AAAH TARATIBU FIONA, ACHA ZAKO”
“SIKIA NINA MAMBO MENGI YA KUFANYA”
Baada ya ujumbe huo kujibiwa ghafla aliona picha ya kivuli na kujua kabisa kuwa ameblokiwa, hakutaka kukubali aliamua kwenda hewani na kujitambulisha vizuri kwa Fiona.
“aah sorry Adrian, mi sikujua kwa kweli si unajua kuna watu wasumbufu sana”
“usijali upo wapi”?
“nipo hostel”
“nije nikufate mara moja chap”
“alafu twende wapi”?
“tuka tembee tu”
“nina course work hapa Adrian siku nyingine bwana”
“usinifanyie ivyo”
“kwani wewe upo wapi”?
“mi ndo natoka job”
“poa njoo mabibo Hostel, ukifika nambie”
Adrian alitabasanu na kuweka simu pembeni akitamani afike haraka mabibo hostel, taa ziliruhusu na kusonga mbele, alifika mabibo Hostel na kumtaarifu kuwa kesha fika tayari, alimchukua Fiona na kumpeleka Rivaside kwenye grocery inayoitwa MANDELA kisha kuagiza nyama choma huku wakipiga stori za hapa na pale, Kweli Fiona alijiachia sana kwa Adrian kana kwamba walijuana muda mrefu sana.sababu walikua mara kadhaa wakipiga stori huku wakicheka na kugonganisha mikono yao
“hivi wifi hajambo”?
“ha ha ha hajambo, nikupeleke ukamuone”?
“mmmh akuu”
“twende mara moja ukamuone alafu nakurudisha”
Sitaki nataka ile mwishowe Fiona alikubali kuondoka na Adrian, ndani ya gari Adrian alizidi kumthaminisha mrembo huyo, kuanzia juu mpaka chini jinsi anavyonukia bila kujali kuwa ni demu wa rafiki yake kipenzi,
ndani ya dakika arobaini tayari walifika Tegeta kibaoni kwa Adrian na kuanza kupiga honi ndani nyumba yake kubwa, mlinzi alifika na kufungua geti, mbele yake  ilionekana nyumba kubwa sana ya kifahari  na kumfanya Fiona azidi kustaajabu kile anachokiona, alimtizama kijana huyu mdogo na kushindwa kujua au ni mtoto wa kigogo ilionekana kabisa alikua na maswali mengi ndani ya ubongo wake wa nyuma medulla oblongata,
“karibu home”
“hapa ni kwako”?
“ndio, vipi kwani”?
“yaani kwako, namaanisha sio kwenu”
“ni kwangu, hapa ndo napoishi, hii nyumba ni yangu nimejenga mimi”

“mmmh”
Aliguna Fiona huku akiingia ndani na kushangaa  kuona vitu vya kisasa sana,hakuelewa aanze kuuliza jambo gani, alionekana dhahiri kuwa ana mambo mengi kichwani ya kuuliza.
Simu ya Adrian iliita kwa sifa akaweka LOUDSPIKA ili Fiona asikie mtu aliye kua akiongea nae.
“Christian Bella, za masiku rafiki yangu”?
“vipi Adrian, uko wapi ndugu”?
“nipo home hapa”
“sasa mimi takuja kesho nataka nikueleze kitu moya hivi ya kufanya sawa”
“saa ngapi Bella”?
“nitakutafuta Kwenye simu chunga”
“poa kaka”
Baada ya kukata simu ile hakutaka kuongea chochote zaidi ya kuzama kwenye friji na kutoka  na juice kubwa, kisha kumimina kwenye moja ya glass mbili nayeye kumimina pia.
“jamani una juana na huyu mkaka,  wewe umemtoa wapi Adrian ulimjua vipi Christian Bella”?
“ kwanza usiulize nime mtoa wapi, uliza kanitoa wapi mimi au kanijuaje, una nichukulia poa wewe, unataka kuongea na msanii gani niambie”
“jamani jamani, mi nawish kuongea na Ali Kiba, nampenda sana”
“subiri kidogo”
Adrian alichukua simu yake na kutafuta namba kisha kupiga namba za msanii huyo ila bahati mbaya namba ilikua haipatikani, kwa kumuonesha kuwa yeye ni bab kubwa aliingia kwenye Garelly na kumuonesha picha walizopiga na wasanii tofauti tofauti kama Ali kiba, T.I.D na wengineo wakiwa sehemu nyingi za kifahari wakila bata na kufanya starehe,

Adrian Alisha jua teyari kuwa mwana mke huyo ni dhaifu sana ana penda kushobokea wasanii ivyo hakutaka kufanya papara alijua ni lazima atamla piga ua, sababu alijuana na wasanii wengi tofauti wanamuziki na wa bongo movie pia , alicho fanya baada ya hapo alimuomba kesho asubuhi aende ofisini kwake ili akutane na Christian Bella msanii ambaye anaefanya vizuri ndani na nje ya nchi kutokea Kongo,
“huyu sina haraka nae,huyu naenda nae mdogo mdogo tu”
Aliwaza Adrian huku akimtizama mrembo huyo ambaye wakati huo alikua na glass ya juice mdomoni mwake, baada ya hapo waliongea mawili matatu na baadae kumpeleka  mpaka hostel kwao kisha yeye kurudi nyumbani kwake,

kabla ya kufika kwake alipokea meseji kutoka kwa Fiona akimsisitiza kuwa kesho asubuhi asisahau kumkutanisha na Chrisstian Bella.

Tayari kulisha kucha Adrian kama kawaida alikuwa njiani akielekea ofisini kwake, alishuka ndani ya gari ila cha ajabu alimkuta Fiona kesha fika tayari alimsubiri kwa hamu, aliingia nae mpaka ofisini kwake na kuletewa kahawa na kuanza kunywa taratibu huku akiperuzi gazeti lililo kuwa mezani kwake kwa wakati huo Fiona alikua na hamu sana ya kumuona Bella,
“yaah mwambie apite”
Adrian Alikata simu hiyo   kisha mtu mrefu wa wastani mweupe kiasi aliyependeza na kunukia marashi ya garama kutokea, Fiona aliye kua pembeni hakuyaamini macho yake  alikua akitetema mno akiwa ameduwaa,
“Bella mwenyewe!”
Aliongea Adrian na kusimama kisha kupeana mikono huku Fiona akimtizama Mwanamziki huyo aliyekua akitabasamu muda wote.
“msalimie Fiona”
Christin Bella alimtizama binti huyo kisha kumpa mkono wake na kuendelea na mazungumzo na Adrian hakuonesha kumbabaikia hata kidogo kama wafanyavyo watu maarufu.
“niambie sasa nakusikiliza Bella”
“kilichonileta hapa bwana Adrian, mimi nina safari kesho kutwa nilikua nataka wewe unishikie mali zangu na magari, kuna project naenda fanya na Lina Sanga Afrika kusini, kuna nyimbo ya mupya aliniomba nifanye nae muziki”
“hapo hapo embu niimbie kwanza mbele ya mtoto mzuri hapa, kipande kimoja”
“okay subiri….switiiiii.mmmmh aaaah , ukilia mamaaa namimi pia nitaliiiaaa, unavyolalamika jua moyo  unani chomaaaa,kutafuta tu mapesa ndo inanifanya niwe bizeee,oooyoo maii yee, sijapenda uwe Lonely aaiiiii.we ndo kiboko wangu uuuh uuuh, mtoto mzuri kama wewe unahitaji matunzoo, na  nikiwa sina pesa itakuaaaje,wasije wenye mapesa zao wakakuchukua taratibuuuuu uuuuuu  aaaah binti ”

Alivyokua akiimba Christian Bella hata wewe ungebahatika kumsikia ungekiri kuwa ni kama unavyomsikia kwenye nyimbo zake, sauti yake ilikua ni ile ile, ilimfanya Fiona abaki akimtizama, na  kumtumia Adrian meseji pale pale kuwa amuombe apige nae picha tu, baada ya mazunguzmo kuisha Adrian alimuomba msanii huyo wapige wote picha kweli hakua na shida yoyote walipiga Selfie na pale pale Fiona kuweka kwenye DP yake ya watsap, na kuituma picha hiyo kwenye magrup yake yote bila kuulizwa walipiga picha nyingi tofauti na kumfanya Fiona awe mwenye furaha sana.

“sasa Adrian nataka niwaphotoe picha na shemeji hapo kaeni hapo”
Adrian alisimama na kumuendea Fiona kisha kusimama.
“mshike kiuno nataka muwe muna romance ile kitu inapenda, munyonye iyo midomo yake”

Aliongea Bella huku akiweka simu yake kubwa vizuri,, kwa Fiona ili  kua mtihani mkubwa kwake lakini hakuwa na jinsi sababu kauli hiyo ilitoka kwa Bella,
Adrian taratibu alipeleka mdomo wake juu ya mdomo wa Fiona na kuanza kumnyonya Lips zake huku picha mbali mbali zikipigwa na kuzidi kunogewa wakizidi kubadilishana mate na kumfanya Fiona afumbe macho yake sababu hapo ndipo udhaifu wake ulipo kwenye lips.

ITAENDELEA.......

No comments

Powered by Blogger.