Nitampata wapi Kama Yule
STORI:NITAMPATA WAPI KAMA YULE
MTUNZI:ABDALLAH &NASEEB
SEHEMU:1
Akiwa amejiinamia huku akiwa hajui la kufanya mara baada kupata ujumbe ule ambao alioupokea kutoka kwa rafiki ake kipenzi aitwae.’ABDALLAH’’ ujumbe ulisomeka kama ifuatavyo katika simu ya NASEEB.
’Mara baada ya kipindi kirefu ndugu yangu leo hii KHADIJA ameamua kuolewa na aliyekua akimuhudumia toka akiwa shule ya sekondari Sengerema ambaye ni mtoto wa kigogo mmoja. na Leo hii ndio harusi yao.‘
’Bila kupoteza muda Naseeb akahitaji kwenda moja kwa moja katika harusi hiyo, kabla yakufanya maamuzi hayo ndipo rafiki yake, Abdallah akaingia nakumtuliza Naseeb, pamoja nakumtaka asiwe na presha
. hapo ndipo Abdul alituliya na kutafakari kwa kina nini anahitajika kufanya, baada ya tatizo hilo kumkumba. baada ya muda kidogo Abdallah alimtaka Naseeb amueleze nini ambacho anafikiria kufanya.
kwa Naseeb haikuwa kazi rahisi kujiuliza kwani alishindwa hata kufikiria nini cha kufanya kwa wakati hule, ndipo Naseeb akataka kujiua mbele ya rafiki yake Abdallah.
Mara baada a kuhitaji kufanya maamuzi yale Naseeb alitulizwa na swahiba wake Abdallah.
,baada ya hapo Naseeb alitulia nakuanza kuchemsha ubongo wake ili afanye maamuzi ambayo ni sahihi akiwa kama mwanaume.
baada ya kutulia ndipo ambapo wakaanza kujadiliana Naseeb pamoja na rafiki yake Abdallah wachukue hatua zipi.Hii ni kwasababu Naseeb na Khadija walikuwa ni wapenzi wenye mapenzi yaliyoshibana pia walikuwa na ndoto za kuwa kuja kutengeneza familia bora isiyokuwa na shaka ndani yake kwani mapenzi kati ya Naseeb na Khadija yalivuma kiasi kwamba watu hawakutarajia kama yataharibika.
HISTORIA YAO KABLA:
Siku hiyo ilikuwa ijumaa tulivu Naseeb akiwa zake nyumban anafanya home work ya shule kisha akimaliza aende zake msikitni kama ilivyo ada kwa waislamu kila ifikapo ijumaa huenda masjdi
.Alipomaliza kufanya kazi yake ndipo alipo amua kwenda masjdi kwani muda ulishafika.
wakati akifikiria hayo mara simu yake ikaita, huku jina likisomeka mpigaji yule ni khadija.
kwa bashasha alijiandaa kupokea simu hiyo mithili kapigiwa na mtu maarufu .Alipopokea tuu simu ile. wote wawili waliongea kwa pamoja bila kutegemea hii ni kwasababu kila mmoja alikuwa na shauku na mwenzake. ndipo kimya kilitawala kidogo na Khadija akanza kwa salam ya kiislaam yaan ASSALAM ALLAIKUM,kwa upole na nidhamu wa hali ya juu huku Naseeb akiipokea salamu hile kwa kuitikia kwa kusema ALHAMDULILLAH.
baada ya kumaliza kuitikia salam hile ukimya ukamvaa Naseeb na kusikiliza kwa utulivu .
Lengo lakufanya utulivu huo Naseeb alikuwa na hamu ya kupata majibu mazuri kutoka kwa kwa Khadija .
ambae katika simu na yeye alikuwa na furaha kubwa mara baada ya Naseeb kupokea simu yake kwa bashasha,
Mara baada ya salaam Khadija alimwambia Naseeb kupitia simu kwamba’’Naseeb nimekuelewa ulivyo niambia nakumalizia kwa kusema
‘’I LOVE SO MUCH NASEEB ,KHADIJA ALIENDELEA KUMSIHII NASEEB KWAKUMWAMBIA NAOMBA UNITUNZE PENZI LANGU ILI TUJENGE FAMILIA BORA.
’’wakati hayo yakiendelea katika simu Naseeb alishindwa kujibu kitu na kubaki mdomo wazi huku akishindwa kujua nini amwambie mwanamke huyo ambae alimtongoza tokea wakiwa katika kidato cha nne,kisha jibu lake anampatia wakiwa kidato cha tano .
Naseeb alipatwa na bumbuwazi sio kwamba hakujua hajibu nini ila furaha tuu ilimuandama mwilini kiasi kwamba alikuwa kaduwaa tuu.
Khadija akaendelea kuongea"nilikupenda sana Naseeb na sio kwamba nilikuwa na kuzungusha siku zote, ila uwoga ndio ulionitawala sana moyoni hali kadhalika masomo yalikuwa yamekaza kwa kipindi kile.
NAKUPENDA SANA NASEEB "Alimaliza KHADIJA kwa maneno yake.
Naseeb alifurahi sana siku hiyo laiti ungelitangulia kumuona wakati akiambiwa maneno hayo ungekili kweli mapenzi huwa na furaha sana endapo pande zote mkipenda .
NASHUKURU KHADIJA KWA MANENO YAKO NAKUAHIDI SITOKUACHA KATIKA MAISHA YANGU, WEW E NA MIMI MBAKA KIFO"Alitamka kijana Yule laiti angejua kuwa mapenzi ni furaha ya mda mfupi asingetamani hata Mara moja kumkaribia Khadija.
Naam huo ni mwanzo tu wa riwaya hii iliyowakutanisha marafiki wa wili kufanya ubunifu kuleta kigongo hiki chenye kusisimua
STORY BY. ABDALLAH KIYOMOLE &
NASEEB MAKUKA
ITAENDELEA...............................
Post a Comment