Header Ads

Nitampata Wapi kama Yule sehemu ya pili

NITAMPATA WAPI KAMA YULE :02
STORI:ABDALLAH &NASEEB

Endelea...............................
mapenzi ni furaha endapo utakaempata yule ambae atakupa furaha mda wote ,lakini mapenzi hayo hayo yaweza kuwa huzuni endapo yule utakaempata hatokupa furaha.mara nyingi mapenzi huanza na furaha mda wote ,mbaka unaweza kufikiria yule ulienae ndio atakae kuwa wako wa milele lakini mwisho wake na yeye huishia kwa kukusaliti.

SONGA NAYO..........................
baada ya kuambiyana mawili matatu  huku pande zote mbili zikionesha kuwa zenye furaha ndani yake,kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza waliongea mambo mengi,mpaka wanafika saa 8 walikuwa tu bado wanaendelea tuu kuongea.

siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana  kwao waliulizana maswali kadha wa kadha huku mada za mapenzi zikichukua nafasi
Khadija:hivi  nikuulize swali mpenzi wangu?
Naseeb: usijal hubby wangu niulize chochote utakacho.
khadija: hivi umenipendea nini?
Naseeb: Hahahahah bby bwana kwa nini umeniuliza swali hilo
Khadij:Nijibu huko mimi sitaki maswal bwana aliongea kwa kudeka,laiti ungemuona jinsi alivyokuwa anaongea na madeko yake hakufanana na mtoto adekae kwa mama yake"
Naseeb: Nimekupenda khadija kutoka katika moyo wangu kiukweli nimekupenda tuu jinsi ulivyo,uzuri wako ,sura yako,tabasamu lako,tabia yako.vyote hivyo ni katika moja ya vitu vilivyonivutia."alimaliza kwa kuzitoa sifa zile"

Nashukuru sana mpenzi wangu nafurahi kuyasikia yote uliyoniambia niseme tuu nakupenda sana naseeb sina mengi ya kuongezea ila mengine mengi tutaongelea shule,nikutakie usiku mwema"aliongea khadija"
sawa mpenzi lala salama eeh tena baby usisahau kuniota.
hahahaha "Alicheka khadija,usijali mpenzi nitakuota tuu wewe ndiye wa ubani wangu nisipokuota wewe nimuote nani sasa."alimaliza khadija
na huo ndio ulikuwa mwisho wa maongezi hayo,hapo kila mtu akaisaliti simu yake na kisha kukifakamia kitanda,na ndipo usingizi  ulipowachukua.

ilikuwa ni asubuhi ya siku nyengine ,siku ambayo hupendwa sana na vibarua mbalimbali,hupendwa sana na wafanyakazi lakini huchukiwa sana na wanafunzi.

siku hiyo ilitambulika kama jumaa tatu,waendao kazini siku hiyo waliamka mapema na kufanya maandalizi kwenda kutafuta rizki,madeleva wa magari ,pikipiki nao hawakuwa nyuma katika kutafuta maisha yao huku wanafunzi nao wakiusaliti usingizi na kuelekea moja kwa moja shuleni.

Naseeb aliamka mapema kama afanyavyo siku zote,alijiandaa kama kawaida yake,baada ya kuhakikisha kila kitu kwake kipo vizuri ndio alipoiyanza safari yake kuelekea shuleni.

akiwa njiani kuelekea shuleni hapo mara akakutana na rafiki yake Ally ,wa kaanza kutembea huku stori mbili tatu zikiwatawala katika maongezi yao.
Ally eeeh sikiya mshikaji wangu,unamkumbuka yule demu aitwae khadija anaesoma form six EGM?"aliuliza naseeb"
Khadija khadija khadijaaa Eheeee nishamkumbuka kamanda wangu si yule mkali wa Mathematics?
Eheeee ndio huyo huyo mshikaji wangu,yule dem dah nilimtokeaga toka kitambo ila alikuwa ananileteaga miyeyusho,ila uwezi amini mwanangu jana kanipigia na kukubali kuwa na mimi kimapenzi."aliongea naseeb"
wacha weee kwa hiyo khadija shemeji yangu au sio,dah we mshikaji kiboko sanah,ila sasa na Nasra yule mtoto wa kipemba utamuacha?
sikiliza mwanangu madem wa siku hizi sio wa kuwapenda kabisa yani hawa wakuwachezea na kuwatema kama bigijii"aliongea naseeb"
na huo ndio ukawa mwisho wa stori zao kwani walikwisha karibia shule ,hapo zikahamia mada za masomo mpaka walipofika shuleni.

uwepo wa mali katika familia yao ulimbeba sana,hakuwa na shida yoyote,licha ya hivyo kila alichokihitaji alikipata kwa mda anaoutaka,
baba yake alikuwa ni mwanajeshi mstaafu huku mama yake akiwa ni wakili.
licha ya hivyo aliuhitaji sana upendo,sio upendo wa baba na mama la hasha bali upendo wa ki mapenzi.
katika maisha yake hakuwai kuwa na mwanaume yeyote,lakini alikuwa anaziskia stori tuu za marafiki zake kuusiana na wanaume.
alikuwa muoga sana na wanaume ,aliwaogopa sana lakini alikuja kuutoa uoga wake baada ya kuzama kwa kijana machachari Naseeb.

ingawa alimpenda lakini alikuwa muoga sana kumwambia lakini siku hiyo ndipo alipojitoa muhanga na kumwambia ukweli.
alikuwa anagalagala kitandani,huku mawazo yakimchukua kichwani,mawazo yake yalikwenda mbali mpaka akawa anafikiria siku atakapo kuwa kitandani na mwanaume huyo,kuja kustuka shuka lilikua limeshachafuka na hapo ndipo alipoacha kuwaza na usingizi kumpata.
asubuhi aliamka kama kawaida,alimshukuru mungu kwa kumuamsha salama,alijiandaa na kuchukua gari limpelekeo shuleni kila siku huku akiwaza pindi atakapo kutana na Naseeb itakuwaje.

ITAENDELEA...................................

No comments

Powered by Blogger.