Header Ads

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

U.T.I ni kifupi cha maneno ya kiingereza: ‘Urinary tract infections’, ni maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo. Ni moja ya ugonjwa unaowakumba sana wanawake kwa sehemu kubwa ingawa hata wanaume pia wanapatwa na ugonjwa huu. Zaidi ya wanawake milioni 8 wanauguwa ugonjwa huu kila mwaka nchini Marekani peke yake.

Kama ulishawahi kupatwa na U.T.I basi hutazisahau dalili zake ambazo mara nyingi huanza kwa hitaji la ghafla la kutaka kwenda kupata haja ndogo na unapofika bafuni mara baada ya kutoa kiasi kidogo cha mkojo utaanza kusikia maumivu kwenye kibofu cha mkojo na hata kwenye urethra. Katika dalili kubwa zaidi utaishia kujisikia homa, baridi kali, maumivu nyuma ya mgongo na hata damu kutoka pamoja na mkojo.

Habari njema ni kuwa kuna dawa mbadala za nyumbani unazoweza kuzitumia na ukajikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Kinachosababisha U.T.I:

Kisukari
Maumivu ya mishipa
Ajari katika uti wa mgongo
Ushoga (kwa wanaume)
Usafi duni
Upungufu wa maji mwilini
Kushikilia mkojo muda mrefu
Kurithi
Kuongezeka ukubwa kwa kibofu cha mkojo au mawe kwenye figo.

Baadhi ya dalili za kawaida na zisizo za kawaida za U.T.I

Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo
Kukojoa mara kwa mara
Kupatwa ghafla na hitaji la kutaka kukojoa
Maumivu kwenye kibofu cha mkojo
Mikojo kukutoka pasipo kutaka
Hali ya kusikia kuungua wakati wa kukojoa
Kukojoa damu
Harufu nzito au mbaya ya mkojo
Homa
Kusikia baridi
Kutokujisikia vizuri
Kujisikia uchovu

Dawa mbadala 9 zinazotibu U.T.I

1. Baking Soda


Baking Soda

U.T.I ambayo imedumu zaidi ya siku mbili inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.T.I isiyotibiwa mapema inaweza kuepelekea matatizo zaidi kwenye figo na kuleta matatizo mengine makubwa zaidi. Ili kuzuia U.T.I isijiimarishe zaidi jaribu kuongeza kijiko kimoja cha chai cha baking soda kwenye glasi ya maji na unywe na hivyo kusaidia kupunguza makali au kuendela kwa maambukizi ya U.T.I. Baking soda itapunguza hali ya uasidi katika mkojo wako na kupelekea nafuu haraka. Baking soda ni ile kinamama wanatumia wakati wanapika maandazi. Siri iliyopo hapa ni huko kupunguza asidi kwenye mkojo na mwilini kwa ujumla na hivyo kuongeza hali ya ualikalini mwilini.

2. Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries):


Zabibu nyeusi


Zabibu nyekundu

Zabibu nyeusi (Blueberries) na zabibu nyekundu (cranberries) ambazo zote zinatoka katika mti wa aina moja na zina sifa sawa ya kudhibiti bakteria. Katika utafiti mmoja, juisi ya zabibu nyeusi iligundulika kuwa na uwezo wa kudhibiti U.T.I. Pendelea kutumia juisi ya matunda haya glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na hata kujitibu na ugonjwa huu.

3. Nanasi


Nanasi

Kula Nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya mhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ‘Bromelain’. Katika utafiti mmoja, watu wenye U.T.I waliopewa hii bromelain sambamba na antibiotic zao walifanikiwa kuondokewa na maambukizi ya U.T.I. Kula vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu.

4. Maji


maji

Kama unasumbuliwa na U.T.I au inakutokea unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara, basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji. Mara nyingi mtu mwenye U.T.I huwa ana upungufu wa maji mwilini na ikiwa utauchunguza mkojo wake utaona ni wa rangi ya njano. Kunywa maji ya kutosha kila siku na kama matokeo yake bakteria wote wanaokupelekea upatwe na U.T.I watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa. Kujifunza zaidi kuhusu tiba kwa kutumia maji bonyeza hapa.

5. Vitamini C


Vitamini C husaidia kuzuia uzarishwaji wa bakteria wabaya mwilini

Baadhi ya madaktari wanashauri mtu atumiie mpaka mg 5,000 za vitamin C kwa siku kwa mgonjwa anayesumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara

No comments

Powered by Blogger.