Header Ads

Bawasiri na Tiba yake





Ugonjwa huu wa bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa. Ugonjwa huu katika jamii hufahamika kwa majina tofauti tofauti hutegemea kabila na mahali.
              Ugonjwa huu umekua ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.
              Kuna aina kuu mbili za bawasiri 1; Bawasiri ya nje 2; Bawasiri ya ndani.
Bawasiri hii ya ndani ndio bawasiri mbaya kabisa kwa sababu ni vigumu mgonjwa kujitambua kua anatatizo na hii inatokana na tabia ya bawasiri yandani kutokua na maumivu wakati inaanza.




SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUPATA BAWASIRI
            
Ugonjwa huu wa bawasiri husababishwa na mambo yafuatayo;
(1) Tabia ya kuketi sehemu moja kwa muda mrefu mfano; madereva
(2) Tatizo sugu la kuharisha
3) Ujauzito
(4) Uzito wa mwili kupita kiasi
(5) Kufanya ngono kupitia tundu la haja kubwa  (kulawitiwa)
(6) Kupata haja kubwa ngumu
(7) Kua na mgandamizo mkubwa tumboni.
                     

bawasiri iliyotokeza nje katika mzunguko wa tundu la njia ya haja kubwa
ATHARI ZA BAWASIRI




* Upungufu wa damu mwilini
* Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
* kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
* kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
* kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
* Kupata tatizo la kisaikolojia
NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
* Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
* kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
* Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
* Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.




              TIBA YA KISASA   (KISAYANSI)
Kama tulivyo elezea ugonjwa huu ni kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa sasa njia zifuatazo hutumika kutibu ugonjwa huu.
1*  Mishipa ya damu kufungwa Rubber band
2*  Kuweka kemikali kwa njia ya sindano
3*  Upasuaji
             
TIBA ASILIA
Zifuatazo ni njia za kutibu  ugonjwa huo wa bawasiri kwa dawa za asili;
        
         1;  Mizizi ya mti wa Mkomamanga ya kutosha kuanzia ujazo wa robo kilo na kuendelea ichemshwe na lita moja na nusu ya maji na vijiko vitatu vya Ubani Makka. hakikisha unakunywa dawa hiyo mara tatu kwa kutwa kwa muda wa siku saba hadi kumi na nne




       2.     Juisi fresh ya jani lililokamaa la Aloe Vera ni dawa nzuri na huondosha bawasiri
      
      3.   (i) Asali nusu lita
            (ii) Unga wa Tangawizi vijiko vitatu
           (iii) Unga wa figili vijiko vitatu
           (iv) Unga wa kitunguu swaumu vijiko vitatu
vitu vyote vichanganywe vizuri mgonjwa awe anakula kijiko kimoja cha mchanganyiko huo mara tatu kwa kutwa kwa muda wa siku 21.

No comments

Powered by Blogger.