Header Ads

Zifahamu njia za uzazi wa mpango za dharura










NJIA YA UZAZI WA MPANGO YA DHARURA



Uchaguzi wa njia hizi siyo kitu rahisi kwa kuwa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kufanya maamuzi yeyote. Lakini awali kabisa, inabidi ujifunze njia mbali mbali, ili kuweza kubaini ni njia ipi itakayokufaa pamoja na mwenzi wako kupanga uzazi. Mnaweza pia kuwasiliana na muuguzi au daktari anayeusiana na masuala ya uzazi wa mpango kwa ushauri, ili muweze kuchagua njia sahihi itakayowafaa.Pia tulijifunza kuhusu njia mbali mbali tukiangalia faida na hasara zake.
Zifuatazo ni njia nyinginezo
ambazo zaweza pia kutumika kupanga uzazi. Njia hizi ni kama njia ya dharura na njia za vizuizi.
1.Njia ya dharura za uzazi wa mpango huusisha matumizi ya dawa za kumeza(morning after pills).



Njia hii humsaidia mwanamama asipate ujauzito endapo atajamiiana bila kutumia njia yeyote, au pengine njia aliyoitumia kwa ajili ya kupanga uzazi haikutumika kwa usahihi au haikufanya kazi (mfano kupasuka kwa mpira wa kiume). Kuna wakati pia mwanamama anaweza kusahau kumeza vidonge vya uzazi wa mpango.
Njia hii ya dharura imekuwa muhimu sana kwa watoto wa kike na kinamama wanaotendewa ukatili kwa kubakwa au kushawishiwa kushiriki katika vitendo vya ngono na watu wenye hila mbaya.
Dawa za dharura za uzazi wa mpango hutumiwa katika dozi moja au dozi mbili. Dawa iliyo na dozi moja hufanya kazi sawa na ile iliyo na dozi mbili. Dawa hii ya homoni hufanya kazi kwa kuzuia upevushaji wa yai katika ovari au kuzuia mbegu za kiume (sperm) kurutubisha yai. Dawa hii hutumika kabla ya saa 72 kupita baada ya mwanamama kujamiaana bila kutumia njia yeyote kupanga uzazi.
2.Vizuizi ni aina nyingine za njia za uzazi wa mpango ambazo haziusishi matumizi ya dawa za homoni .Njia mojawapo hujulikana kama kiwambo (diaphragm). Kiwambo hiki hutengenezwa kwa  kutumia mpira na chenye umbo la bakuli ndogo. Kiwambo hiki hupatikana katika ukubwa tofauti, na mwanamama atahitaji msaada wa daktari ili aweze kufahamu ukubwa wa kiwambo kitakachomfaa. Uwekaji wake hautahitaji msaada wa daktari kama ilivyo kwa vipandikizi.
Kabla ya kujamiaana mwanamama hukiweka kiwambo kufunika mlango wa kizazi (cervix). Kiwambo hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume kuogelea kuelekea tumbo la uzazi na huitaji kuondolewa ndani ya muda wa saa 24.
3.Mipira ya kike(female condom), ni aina nyingine ya kizuizi, ambayo huvaliwa na mwanamama katika uke. Njia hii hufanya kazi kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia katika tumbo la uzazi.Aina hii ambayo hutengenezwa kwa mpira mwembamba ina ringi mbili.Ringi ya ndani(iliyo ndogo) ambayo huingizwa na kujishika kwa ndani na ringi ya nje(iliyo kubwa) huzuia sehemu ya nje ya mpira kuingia ndani ya uke wakati wa kujamiiana. Mpira huu waweza kuvaliwa masaa 8 kabla ya kujamiina na humpa uhuru zaidi mwanamama katika maamuzi ya kutumia mpira ukilinganisha na mipira ya kiume. Mpira utahitajika kubadilishwa endapo mwanamama atajamiiana tena. Mpira huu usitumike pamoja na mpira wa kiume kwa wakati mmoja.
4.Mpira wa kiume(male condom), huvaliwa kwenye uume baada ya kuhemka.Aina hii ya kizuizi hutengenezwa kwa mpira (latex,polyurethane).Kila wakati mwanaume anapojamiaana huitaji kubadilisha mpira mpya.
Ili isipoteze ubora wake mipira ya kiume na kike inahitaji kuhifadhiwa sehemu kavu na isiyo na joto. Epuka kutumia vilainishi vya mafuta kwa kuwa huaribu mpira na waweza kupasuka.Vilainishi kama gel zinazochanganyika na maji zaweza kutumika mfano K-Y Gel®.
Je njia zote za uzazi wa mpango zaweza kuzuia HIV na magonjwa ya zinaa?
Jibu ni hapana. Mpira wa kiume ndiyo njia pekee iliyofanyiwa utafiti na kuonekana kuwa na uwezo wa kukinga magonjwa ya zinaa na HIV ingawa siyo kwa asilimia mia moja. Tafiti zinaendelea kuchunguza  mipira ya kike kama yaweza kuzuia maambukizi ya HIV na magonjwa ya zinaa.
                                                                 Ahsante
Kwa mawasiliano na ushauri
Whatsapp 0684127127,0765896355
Facebook  welfare jambo

No comments

Powered by Blogger.