Header Ads

Magonjwa ya ngono/zinaa na tiba zake






Ugonjwa wa zinaa wa Kaswende (Syphilis)
MAGONJWA YA NGONO














Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya protozoan vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama urethra na tupu ya mwanamke (vagina). Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas vaginitis au Trich (tamka “Trick”).
Trichomoniasis huathiri watu milioni 8 kwa mwaka Nchini Marekani na watu milioni 170 kwa mwaka dunia nzima. Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume labda kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis.
Nakumbuka mwanajumuiya mmoja wa TanzMed  aliuliza swali na hapa naomba ninukuu “madaktari, poleni na kazi za kila siku. mimi nina tatizo napata sana hizi yellowish discharge au niseme kama rangi ya maziwa hivi zinatoka huku chini kwenye tupu, asubuhi, mchana na jioni kama dose ya panadol. lakini hazina harufu kabisa, maana nilisoma makala zenu inasema kama zinatoa harufu ni dalili ya infections. Halafu za kwangu ni nzito hasa na zinavutika. Naomba msaada wenu sijui itakuwa ni nini?” mwisho wa nukuu.
Katika jibu langu nilimuahidi kuendelea na makala za magonjwa ya zinaa na leo naendelea na sehemu hii ya nne.
Nini hutokea wakati wa maambukizi/Pathofiziolojia ya ugonjwa (Pathophysiology)
Umbile la vimelea vya Trichomonas vaginalisni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana (10 μm) ingawa wakati mwingine ukubwa waweza kutofautiana kulingana na mazingira. Kutokana kuwepo kwa mfano wa mikono kwa nje inayojulikana kama flagellum ambayo husaidia vimelea hivi kuingia kwenye tishu za mrija wa kupitisha mkojo pamoja na tupu ya mwanamke na hivyo kuharibu seli aina ya epithelium na kusababisha vidonda (microulcerations)  katika tishu hizi. Hii ndiyo sababu kubwa ya kwanini watu wanaopata ugonjwa huu wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa ukimwi (HIV) na magonjwa mengine.
Wagonjwa huwa na dalili zipi?
Dalili za Trichomoniasis huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 mpaka ya 28 baada ya mtu kupata maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa wanawake, Trichomoniasis huathiri shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo, tezi zinazojulikana kama Bartholin glands na Skene glands. Kwa wanaume vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis hupatikana katika sehemu za siri za mwanamume, sehemu ya nje ya mrija wa kupitisha mkojo (anterior urethra), kwenye tezi dume (prostate), kwenye mirija ya kuhifadhi na kutoa shahawa (epididymis) na hata kwenye shahawa zenyewe.
Dalili kwa wanawake zinaweza kuwa;Uchafu unaotoka kwenye tupu ya mwanamke ambao unakuwa wa rangi mchanganyiko ya njano na kijani, au rangi ya kama kijivu na huwa mzito sana.
Maumivu wakati wa kujamiana (dyspareunia)
Harufu kutoka kwenye tupu ya mwanamke
Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo (kukojoa)
Shingo ya kizazi kuwa nyekundu – hii hugundulika wakati daktari anamfanyia mgonjwa uchunguzi.
Kuwasha sehemu za siri – Kwa baadhi ya wanawake sio wote
Maumivu chini ya kitovu – Pia kwa baadhi ya wanawake
Ingawa wanawake ndio huonyesha dalili na viashiria vya ugonjwa huu, muda mwengine wanaweza kuwa na vimelea hivi hata kwa muda  wa  miaka kadhaa hata kama vipimo vya uchunguzi havitaonyesha (negative) kama ameathirika na vimelea hivi.
Wanaume huwa hawaonyeshi dalili zozote lakini baadhi wanaonyesha dalili zifuatavyo;Kuwasha ndani ya uume
Kutokwa na uchafu au majimaji kutoka kwenye uume wake
Kuwasha au kama kichomi (burning sensation) baada ya kujisaidia haja ndogo au baada ya kutoa shahawa.
Vipimo vya UchunguziTrichomoniasis hugundulika kwa kutumia kipimo cha hadubini (Microscope), daktari humfanyia mgonjwa uchunguzi kwa kuingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke kinachojulikana kama speculum na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum (cotton swab) na kupeleka maabara kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas vaginalis. Kwa kufanya uchunguzi huu, daktari pia anaweza kuangalia kama kuta za ndani za tupu ya mwanamke au shingo ya kizazi kama zimeathirika kwa kuwa na vidonda ambavyo ni vyekundu (red ulceration). Kwa mwanamume, daktari huchukua kipimo cha uchafu unaotoka kwenye uume wake au hupangusa sehemu za siri za mwanaume kwa wale ambao hawatoi uchafu au majimaji yoyote kwa kutumia pamba na kupeleka maabara kufanyia uchunguzi.
Kipimo kilichochukuliwa na daktari kinaweza kuoteshwa kwenye maabara (culture) na kuangalia kama kutakuwa na uoto wa vimelea vya Trichomonas vaginalis baada ya siku tatu.
Daktari pia anaweza kuangalia kiwango cha kiwango cha tindikali (PH) kwenye tupu ya mwanamke kwa kutumia karatasi maalum ya kipimo hiki (PH paper), kiwango kitakuwa alkaline (PH zaidi ya 5). Kwa kawaida PH ya tupu ya mwanamke inakuwa ni ya tindikali (acidic) kuanzia 3.8 mpaka 4.5, magonjwa yanayobadilisha PH hii pamoja na Trichomoniasis ni Bacteria Vaginosis, atrophic vaginitis nk, na hivyo kumfanya mwanamke kuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti.
Kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis), na saratani ya tezi dume. Kipimo hiki kifanywe kwa wanaume wanaopata ugonjwa wa Trichomianisis  mara kwa mara au wale wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea na ambao wamepata ugonjwa huu, wafanye kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka.
Kipimo cha Pap smear – Chembechembe au seli za shingo ya kizazi huchukuliwa na kuchunguzwa kutumia hadubini. Kipimo hiki pia hutumiwa katika uchunguzi wa wanawake ili kujua kama wamepata saratani ya shingo ya kizazi au la. Wanawake wenye zaidi ya miaka 18 au wale wenye upungufu wa kinga mwilini wanashauriwa kufanya kipimo hiki angalau mara moja kwa mwaka ili wajue afya yao.
Elisa for HIV – Kipimo cha kuangalia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi
Urinalysis – Kipimo cha mkojo
Complete Blood Count ama FBP –Kipimo cha damu kuangalia wingi wa damu, chembechembe tofauti za damu na chembechembe bapa (platelets).
Tiba ya Trichomoniasis
Tiba ya ugonjwa huu ni kutumia dawa aina ya metronidazole au flagyl. Kwa wanawake wajawazito, dawa hii haitumiki kwa wale wenye ujauzito wa chini ya miezi mitatu au kwa wale ambao wananyonyesha. Ni vizuri kumuona daktari kabla ya kutumia dawa hii.
Wale walioathirika, wanashauriwa kupata tiba pamoja na wenza wao. Madhara ya dawa ya metronidazole ni pamoja na mcharuko mwili (allergic reaction), kichefuchefu, kukauka midomo, kuharisha, kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni, kushindwa kuhimili pombe na kushuka kiwango cha chembechembe nyeupe za damu (leukopenia) ambazo hutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na hivyo kumuweka mtu kwenye hatari ya kupata maambukizi tofauti tofauti. Kwa wale wanaokunywa pombe ndani ya masaa 24 baada ya kumeza metronidazole, hupatwa na madhara kama kutapika, kuharisha, kichefuchefu, kukojoa na kutokwa jasho kwa wingi.
Madhara ya TrichomoniasisHuongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi (1).
Husababisha mwanamke kuzaa mtoto njiti au mwenye uzito mdogo (3).
Kwa wanawake, huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi
Kwa wanaume, huongeza hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
UGONJWA WA KASWENDE KATIKA MISHIPA YA FAHAMU (NEUROSPHYLIS)




Madhara ya ugonjwa wa kaswende katika mfumo wa mishipa ya fahamu hutokea  miaka 10-20 baada ya mtu kuugua ugonjwa wa kaswende na ambaye hakupata tiba yoyote hapo awali. Madhara haya huonekana kwenye uti wa mgongo na kwenye ubongo. Kuna aina nne ya neurosyphilis kama ifuatavyo: 
Isiyo na dalili (Asymptomatic) – Katika aina hii mgonjwa anakuwa hana dalili zozote. Aina hii ndio huonekana sana kwa wagonjwa ambao hawakupata tiba hapo awali.
Ulemavu wa jumla (General paresis)
Inayoshambulia tando za ubongo na mishipa ya damu (Meningovascular)
Inayoshambulia sehemu za chini za uti wa mgongo (Tabes dorsalis)
General paresis hutokana na kuathirika kwa ubongo na hivyo kuleta upungufu katika ufanyaji kazi wa ubongo (impairement of mental function). Aina hii pia huweza kutokea kwa wagonjwa wa kisonono (gonorrhoea).
Dalili za general paresisKupungua uwezo wa kuzungumza (aphasia)
Kupungua uwezo wa kufanya maamuzi (impaired judgement)
Kutokuwa na uwezo wa kuhesabu kitu chochote
Kupungua kuhamasishika (impaired motivation)
Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita muda mrefu (loss of long term memory)
Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita karibuni/muda mfupi (loss of short term memory or recent events)
Degedege
Kushindwa kutembea au kutumia miguu, mikono na viungo vyengine vya mwili
Mabadiliko ya kitabia na kihisia (personality changes) kama
Delusions, kuona au kusikia vitu ambavyo visivyokuwepo (hallucinations)
Kukasirika kwa haraka (irritability)
Inappropiate moods
Low moodViashiria vya general paresisMboni za jicho kuwa katika umbile ambalo si la kawaida
Mboni kushindwa kupepesuka  (changes in pupil response)
Kupoteza uwezo wa kuhisi mgandamizo au mtikisiko katika ngozi (Loss of sense of vibration or position)
Kushindwa kusimama wakati mtu amefunga macho (romberg test)
Kushindwa kutembea vizuri
Viungo vya mwili kuwa dhoofu
Matatizo ya kusahau
Vipimo vya uchunguziFTA- ABS – Kipimo cha damu kinachofanya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum  wanaosababisha kaswende
RPR  (Rapid Plasma Reagin) – Kipimo hiki pia huangalia antibodies za Treponema Pallidum katika damu ya  wagonjwa wa kaswende
VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)- Kipimo cha kuangalia antibodies za  Treponema Pallidum, kipimo hiki kimeshahabiana sana na kipimo cha RPR.
Lumbar Puncture – Kipimo cha kuchukua maji ya uti wa mgongo ili kuangalia kiwango cha sukari katika maji hayo, presha yake, protini, chembechembe nyekundu na nyeupe za damu, rangi yake, madini ya chloride. Kipimo hiki ni muhimu sana kwani husaidia kutambua kama kuna magonjwa mengine kama ugonjwa wa uti wa mgongo, multiple sclerosis, hypoglycemia, kiharusi, saratani, jipu nk.
Cranial CT na MRI – CT Scan ya kichwa pamoja na kipimo cha MRI ili kuangalia kama kuna magonjwa mengine mbali na kaswende na kuangalia sehemu ipi ya ubongo iliyoathirika.
Nerve conduction test – Kipimo cha neva za mwilini
Vipimo vya macho
Dalili za meningovascular ni;Mboni kuwa ndogo
Kupooza kutokana na kuathirika kwa neva mbalimbali
Kuharibika mishipa ya damu mwilini
Kupooza upande mmoja wa mwili
Matatizo ya kumeza chakula – Kumeza chakula kwa shida
Degedege
Kupooza neva ya jicho (optic neuropathy)
Matatizo ya macho (chorioretinitis)
Ukiziwi
Vertigo nk.
Vipimo vya uchunguzi vya meningovascularVipimo vya hepatitis
ELISA for HIV – Kipimo cha ugonjwa wa ukimwi
PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba vya bakteria mbalimbali kama Chlamydia trachomatis, Trichomonas vaginalis nk.
Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
Tabes Dorsalis husababisha kudhoofika kwa viungo vya mwili kutokana na kuathirika kwa uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu. Hali hii ni hatari sana kwani ina kawaida ya kuwa endelevu na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa.
Dalili za Tabes DorsalisKutembea kwa shida
Mgonjwa kutembea huku ametanua miguu sana (wide based gait)
Kudhoofika viungo vya mwili
Kupoteza uwezo wa kuunganisha hisia na matendo fulani fulani katika mwili (Loss of coordination)
Kuwa na hisia zisizo za kawaida mwilini kama vile kujihisi vitu vinachoma choma (lightening pains)
Loss of reflexes
Vipimo vya uchunguzi vya Tabes DorsalisCBC (Complete Blood Count) – Kipimo cha wingi wa damu, kuangalia aina za chembechembe za damu nk.
Urinalysis – Kipimo cha mkojo
Lumbar Puncture for CSF – Kipimo cha kuangalia maji ya uti wa mgongo kama nilivyoeleza hapo juu.
CT Scan – Kipimo cha CT Scan ya kichwa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu.
MRI ya kichwa
VDRL, RPR, FTS-ABS, MHA-TP – Vipimo vya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum kama nilivyowahi kueleza.
Tiba ya Neurosyphilis
Tiba ya aina zote za neurosyphilis huusisha kwanza kutibu ugonjwa wa kaswende kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya penicillin G au doxycyline kwa wale wanaopata madhara ya penicillin. Hata hivyo kwa wale wenye matatizo na penicillin ni bora kumueleza Daktari mapema ili achukue hatua zinazostahili.
Kwa wale wagonjwa wasioweza kula, kuvaa nguo, wale waliopooza viungo, wasioweza kuzungumza, watahitaji tiba mbalimbali kama rehabilitation therapy, physical therapy, occupation therapy, speech therapy nk.
Dawa za maumivu na  degedege zinaweza kutumika kwa wale wenye kupata maumivu na degedege. Kwa wale viziwi, watahitaji vifaa maalum vya kuwasaidia kusikia (hearing aids) baada ya kuonana na Daktari wa masikio, pua na koo.

No comments

Powered by Blogger.