Header Ads

WASALITI 100 CCM WAKIONA CHA MOTO

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza mjini hapa juzi, Katibu Mwenezi wa chama hicho mkoani hapa Saimon Mangelepa, alisema wanachama hao wanatoka katika wilaya nne za Nyamagana, Misungwi, Ukerewe na Kwimba.

“Baada ya kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kikao kilichofanyika Aprili 24, mwaka huu kiliridhia kuwa wanachama, viongozi na watumishi wa serikari waliotuhumiwa kukisaliti Chama Cha Mapinduzi wachukuliwe hatua kwa kuwa isipofanywa hivyo usaliti utazidi, hivyo Halmashauri Kuu za CCM ngazi ya wilaya ziliketi na kufanya maamuzi hayo na sisi CCM mkoa tulipokea taarifa hizo na maamuzi tumeshayatoa ya kuwafukuza na kuwavua uanachama watu 100,” alisema.

Magelepaa waliovuliwa uanachama na kufukuzwa ni waliokuwa wanashikilia nafasi za udiwani waliomaliza muda wao 2015 na wakagombea katika kura za maoni wakashindwa, wenyeviti wa kata wa CCM na wenyeviti wa Umoja wa Wanawake (UWT).

Wengine ni makatibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), katibu wa wilaya, mjumbe wa mkutano mkuu taifa, mjumbe wa kamati ya uchumi kata, wenyeviti wa matawi, makatibu kata, wenyeviti wa wazazi, makatibu wa wazazi kata, wajumbe wa halmashauri kuu wilaya, mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT wilaya, makada, wenyeviti wa mitaa, mabalozi na wanachama wa kawaida.

Mangelepaa alisema CCM mkoa imejipanga kukabiliana na wananchama wasaliti ili kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.

No comments

Powered by Blogger.