Header Ads

Kutembea katika hekima ya Ki-Mungu


Kutembea Katika Hekima Ya Ki-Mungu ·

Maana hekima ya dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu… (1 Wakorintho 3:19).
Kuwa mfanikiwa wa kweli maishani, ni lazima utembee katika hekima ya Ki-Mungu. Kutembea katika hekima ya Ki-Mungu maana yake ni kutembea katika Neno; kuliishi Neno, kwa sababu Neno la Mungu ni hekima ya Mungu. Wanaume na wanawake wakuu wa imani tuwasomao katika Biblia walijitofautisha kwa kufuata Neno la Mungu.
Yoshua, kwa mfano, alitembea na Mungu kulingana na maagizo aliyopokea kutoka kwa Bwana, na kuleta kushinda kwa ajabu kwa watoto wa Israeli (Yoshua 8:1-24). Isaka pia alitembea na Mungu. Kulikuwa na njaa katika nchi na wengi walikuwa wakihamia Misri kufuata malisho. Isaka alijiandaa kwenda Misri vile vile, lakini Mungu Akamwambia asiende. Badala yake Mungu Akamuagiza abakie Gerari ambako kulikuwa na njaa na apande katika nchi hiyo (Mwanzo 26:2-4).
Fikiria Mungu Anakwambia ubakie katika nchi iliyokumbwa na njaa, ambako mambo huonekana magumu na kavu; Je! ungesikiliza maneno Yake? Njia na "fikra" Zake zi tofauti na njia za mwanadamu. Ni hekima kufanya Asemacho na kufuata maagizo Yake, hata kama hayaleti maana katika fahamu za binadamu.
Isaka hakuendelea na mpango wake mwenyewe; alifuata mwongozo wa Bwana na kusitawi kupita kawaida katika nchi ile ile iliyokuwa imeharibiwa na njaa. Pale ambapo wengine walichimba ili kupata maji, hawakupata maji, lakini Isaka alipochimba kupata maji, alipata maji, katika nchi ile ile kavu. Biblia husema, "Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA Akambariki. Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ngómbe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamsujudu (wakamuonea wivu)" (Mwanzo 26:12-14).
Waweza tumia ufahamu wako wa kibinadamu kuyatafakari baadhi ya mambo maishani mwako na huduma katika nyumba ya Mungu, lakini hekima ya Mungu ni kuu kuliko hekima ya mwanadamu. Enenda katika, pamoja na, hekima na ufahamu wa Neno la Mungu. Fuata mwongozo wa Roho maishani mwako, na siku zote utakuwa mwenye kushinda.
Sala
Baba Mpendwa, ninakushukuru kwa hekima Yako itendayo katika roho yangu, ambayo pia imeongezeka hata sasa kupitia Neno Lako na nimepokea leo. Ninatembea katika hekima ya Ki-Mungu, nikitimiza mapenzi Yako kamilifu, na kukuletea utukufu katika kila ninachofanya, katika Jina Lake Yesu. Amina.
Mafunzo zaidi: Matendo 20:32; Mezali 4:7; 1 Wakorinto 1:24-25

No comments

Powered by Blogger.