Header Ads

H/KIBAHA KUWAJENGEA SOKO WATAKAOBOMOLEWA MAILIMOJA

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo juzi kwa wananchi na wakazi wa Mailimoja wakiwamo wafanyabiasha ambao maeneo yao yanatarajia kubomolewa kwenye upanuzi wa barabara.

Ndikilo alifafanua kuwa Wakala wa Barabara (Tanroads) ilitoa notisi ya miezi mitatu ambayo utekelezaji wa bomoa bomoa unafanyika Novemba 23 mwaka huu, lakini umesogezwa mbele hadi January mwakani.

Alisema Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha tayari amepata mkandarasi wa kujenga soko, hivyo ni jukumu lake kutumia kipindi hicho cha miezi miwili kukamilisha kazi ili wafanyabiashara wapate sehemu ya kuendeleza shughuli zao.

Alisema bomoa bomoa ingekumba wafanyabiashara na wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara lakini baada ya kuwasiliana na Wizara ya Miundombinu ilikubali kupunguza kutoka mita 120 hadi 60 kila upande.

Alisema wafanyabiashara wote watapata maeneo ya biashara kwenye aneo la soko jipya lililotengwa na kwamba kila mmoja ataingia mkataba na Halmashauri muda wa kujenga vibanda hivyo.

Bomoa bomoa hiyo itawagusa wananchi wengi wakiwa wafanyabiashara ambao wamejenga mita 60 kutoka barabarani vikiwamo vibanda vilivyopo stendi ya Mailimoja Kibaha.

Baada ya bomoa bomoa hiyo magari ya mikoani pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia katika stendi ya Mailimoja daladala zitakuwa zinaingia kwenye kituo cha Njuweni.

No comments

Powered by Blogger.