Header Ads

Kafara la damu

KAFARA YA DAMU: 01
STORI: KAFARA YA DAMU

Ilikuwa ni asubuhi tulivu iliyopambwa na kila uzuri wa aina yake,huku jua likipiga kama ada yake,waendao kazini siku hiyo waljiandaa vema kuelekea makazini kwao,wenye vibarua nao hawakuwa nyuma kujitafutia riziki zao,na wale wafanya biashara ndogo ndogo(Maarufu kama Machinga) hawakukaa nyuma katika kujiafutia maisha yao,naam hilo ndio jiji la dare s salaam jiji ambalo huitwa na baadhi ya watu jiji la gharama,jiji lililojaa kila aina ya starehe ,jiji lililojaa kila aina ya ushetani,wizi,vifo,ubakaji,kamali ni miongoni mwa vitu vifanyikavyo katika jiji hilo,naam hilo ndio jiji la dare s salaam.

Katika chumba kimoja maeneo ya kiwalani ndani ya jiji hilo hilo la dar es salaam alionekana kijana mmoja akiwa anatafuta kitu chumbani kwake,hakukua na mtu ajuae anatafuta kitu gani lakini laiti ungemuona jinsi alivyokuwa anatafuta ungeligundua hakuwa anatafuta kitu   cha kawaida.
Alhamdulillah nimekipata”alijisemea mtu yulee”si kwamba alimshukuru mwenyez kufanikisha jambo lake bali alijisemea tuu kwa kudhania kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa matatizo yake.
Baada ya kukipata alichokuwa anakitaka alijiandaa vema kama kawaida yake ,akayapangilia vizuri mavazi yake ,lakni  kabla ya kuufikia mlango wake tuu wa kuondokea mara tuu simu yake ikaitaa,aaaaah atakuwa nani tenaaah…!! “alijisemea kijana yule” nahii ndio ilikuwa kawaida  yake
hupenda kujiuliza swali yeye mwenyewe na kujijibu yeye mwenyewe”ngoja nipokee tuuu,baada ya kusema hayo alishika kitufe cha kupokelea na kuipokea simu ilee.
UNAITWA NASEEB NI MZALIWA WA DODOMA ,UNA MAISHA MAGUMU LAKINI UNA NDOTO
SIKU MOJA UTAJILIKE,NA UISHI MAISHA MAZURI,SI NDIVYO KIJANA?”Ilikoroma sauti ile’bila ya kumpa nafasi kijana Yule  aijielezeee kama amekubali ama amekataa ile sauti ikaendelea kuongea “KAMA UNAUTAKA UTAJIRI SAA 6:00 UNATAKIWA UFIKE NJIA PANDA YA MTAANI KWENU ,NA YATAKAYO KUTOKEA USIMWAMBIE MTU’
Laa haulaaaaaa kijana Yule alihamaki si kwamba hakujua ninini kimetoka kuongelewa katika simu yake bali alijiuliza sana kuhusu sauti ile ya ajabu,hivi kaipataje namba yangu? Na je ni fanye nini niondokane na tatizo hili? Hayo ni machache tuu katika mengi aliyokuwa anajiuliza kijana Yule.

HISTORIA YAKE KIUFUPI
Jina kamili ni Naseeb makuka ,alizaliwa mwaka 1990, ni mtoto wakwanza na wa mwisho katika familia yao ,alizaliwa katika kitongoji kimoja mjini Dodoma,kutokana na ukame wa jiji hilo,ndipo alipoamua kuli saliti jiji hilo na kutumbukia katika jiji la dare s salaam,mwanzoni maisha yake yalikuwa magumu kiasi lakini uzoefu wa jiji hilo ulimfanya nayeye aanze kuzoana na watu mbalimbali .Naam hayo ndio maisha halisi ya Naseeb
Baada ya kujiuliza afanye nini kulitatua tatizo lake ndipo alipoamua kuelekea kwa rafiki yake aitwae john  ili aweze kumsaidia japo kwa mawazo tuu katika kulitatua tatizo lake.
          Akiwa njiani kuelekea kwa rafiki yake huyo cha kushangaza simu yake  ilita kwa namba ngeni ambayo niya ajabu , hapo ndipo akafanya maamuzi  ya kupokea simu huku akiwa na hofu iliyomjaa utadhani amekutatana na simba, mara baada ya kupokea simu hiyo ndipo akasikia sauti nzito na yenye mtetemo ikimwambia kwa msistizo’’USIMWAMBIE MTU YEYOTE MATATIZO YAKO NA UKIFANYA HIVYO UTAFANIKIWA LAKINI USIPOTEKELEZA HIVYO ITAKUGHARIMU MAISHA YAKO PAMOJA NAKUPATA LAANA KATIKA MAISHA YAKO YOTE’’
                Naseeb alibaki kuduwaa na asijue nini cha kufanya hapo hakutaka kuendelea na safari yake bali aligeuza na kurudi nyumbani kwakee. Saa sita usiku

ITAENDELEA…………………………………………………………………..
Unajua nini kitakacho endelea?
Je hiyo saa 6:00 ataenda njia panda?
Na je kama hakienda kipi  kitakachomkuta?
ungana na mimi tena kwa muendelezo wa riwaya hii.

Alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi  kupita kiasi ,laiti ungempima ungejua mapigo yake hayakuwa yakidunda kawaida,licha ya hivyo,aliogopa sana kauli hile,aliomba saa igande ama arudi maisha yake ya nyuma aliyokuwa akiiishi,lakini yote kwake yalikuwa ni mawazo tuu na ukweli ulikuwa haupingiki .
Ikiwa  umekaribia mda wa kwenda kukutana na mtu Yule asiyefahamika jina,mtu Yule mwenye sauti ya ajabu,mawazo tele yalimjia kichwani,si kwamba hakuitaji mali lakini alijiuliza ni vipi atapata pesa bila ya kuangaika au kujishughulisha na chochote.
Mhhhhhh…….!!!! Aliguna  tena kijana Yule aliyefahamika kama Naseeb,itabidi niende tuu,hapo akaenda chooni kuoga,akabadilisha nguo zake,alipomaliza akaanza kutoka na kuelekea  njia panda ikiwa kama ahadi aliyojiwekea na mtu Yule.
Alikata mitaa kadhaa ,huku akiwa na hofu moyoni,katika siku alizowai kuogopa siku hiyo ilizidi,licha ya kiza kuongezeka  lakini uliongezeka uoga kutokana na kutojua mtu gani anaenda kukutana nae licha ya kujua mada itakayokwenda kuongelewa.
Alifika mda muafaka kama jitu lile lilivyosema,akiwa  anatazama kila upande wa njia panda ile,mara atizame kaskazini,mara atizame kusini,mara atizame mashariki mara, atizame magharibiri,lakini hakuona chochote kile.
Alijifikiria kichwani kipi anatakiwa afanye ,je aondoke na arudi nyumbani kwake,ama abaki amsubir huyo mtu waliyewekeana ahadi?
Maswali mengi yalipita kichwani mwake,ingawa yote aliyaogopa lakini aliutaka sana utajiri.sasa iweje aondoke wakati bwana Yule amemuahidi kuwa tajiri?naseeb alibakii.
Ghafra bila ya kutegemea mara moshi  ukaanza kumjia mwilini mwake, akawaza sana katika akili yake je nikimbie? La haulaaaaaa mara ule moshi ukabadilika na kuwa mvua  ya damu.
Akili yake haikufanya kazi kwa mda ule,aliganda tuu,mfano wa mtu aliyepatwa na pumbazo,hakuelewa kipi kinachotaka kufanyika juu yake ila tamaa  tuu ndiyo iliyomuongoza kwa wakati ule.
Mara kwa  hali asiyotegemea akaanza kuona paka wametokea,wakaanza kulia kwa sauti,zao,ingawa paka sio wa kutisha lakini siku hiyo ,laitI ungekutana na paka hao lazima ungebadilisha njia.
Walikuwa nip aka weusi waliyokuwa na mabaka mabaka mekundu,macho yao yakin’gara kama paka wengine lakini upande wa mwili walikuwa ni wakubwa mithili ya mijibwa ya kizungu.
Kutokana na uoga uliyomjaa,hofu,wasiwasi kiijana Yule hakuweza kustahimili akazimiaaa.
Hahahahaahaha      hahahahaahahaha hhahahaahahaaaa vicheko vilishamiri katika eneo lile ,mara ghafla upande wa kusini lilionekana jitu kuuuubwa likija upande ule ,kwa jinsi ukimuangalia mtu Yule  na kumuona jinsi watu walivyompokea kwa furaha ungeligundua tuu kwamba Yule ndiye kiongozi wa kundi lile.
Kufaaaaaanaaa,kufaaaaaaana”walisalimia watu wale kwa lunga yao waliyokuwa wanaijua wao wenyewe,huku wakionekana wenye kupiga magoti.
Machaaaaaa machaaaaaa  jamiiiii zindabaaaa”liliitikia jitu lile”na hiyo ndio iliyokuwa salamu baina yake na watu wake wa zindabaaa.
Baada ya salamu zahapa na pale ndipo jitu lile likachukuwa nafasi kama kiongozi kuanza kuelezea agenda zilizowakutanisha pale,
NIMEWAITENI   ENYI   WANA   JAMII  YA  ZINDABA  KWA  LENGO  MOJA TUU ,NAZANI  MLIKUWA MLALAMIKA   SANA  JUU YA KIZAZI HIKI CHA ZINDABA  KWA NINI HAKIENDELEI,KWA NINI KIZAZI HIKI CHA ZINDABA  HAKINA WANAWAKE,BASI HUYO  MTU HAPO CHINI NDIYO SULUHISHO LA MATATIZO  YA WATU WA ZINDABA.
********************** ITAENDELEA****************************
JE unataka kujua kitakacho tokea?
UNGANA NA MIMI TENA KWA MUENDELEZO WA RIWAYA HII

No comments

Powered by Blogger.