Mchachiko sehemu ya 28
MCHACHUKO……(28)
MTUNZI….EMMANUEL F. KWAY
Contanct….+256756 322432
AGE…(18+)
ILIPOISHIA
Chupa zilirushwa nyingi na kumchana Adrian usoni, sekunde cahche uso wake ulikua umelowa damu nyingi, alivyo muangalia Mathew mkononi vizuri aliona saa yake ya ROLEX sababu ndani ya saa hiyo kulikua kuna jina lake lililoandikwa na vidude vya dhahabu,
lakini hakua na ujanja tena walisha mpiga sana bila huruma yoyote ile, hapo ndipo Mathew alipo okota chuma na kumpiga nacho kichwani.
Maumivu aliyoyasikia hayakuweza kuelezeka kabisa damu zili mvuja kila sehemu ya mwili wake na watu kuzidi kuongezeka, kweli alipigwa sana mpaka kupoteza fahamu zake.
SONGA NAYO.
“Paaa, paaaa”
Mlio wa mtutu aina ya SMG ndio uliwa sambaratisha watu waliokua wana mpiga Adrian mpaka kupoteza fahamu zake chini haelewi tena kinachoendelea damu nyingi zina mtoka mwilini, ni baada tu ya kumshika mwanamke Jaqlin aliyekua Mrembo na kusingiziwa kuwa ni mwizi, hapo ndipo walipoanza kumpiga, aliye muokoa Ni mlinzi aliyevalia jezi zake mwilini akiwa katika lindo kwenye ukumbi huo,
Na hiyo ndiyo ilikua ponea ya Adrian na sio vinginevyo
“kuna nini?”
Aliuliza mlinzi huyo akiwa kashika mtutu mkononi mwake akijihami.
“huyu ni mwizi”
Alijibu Mathew
“Kaiba nini?”
“simu na pesa zangu”
“sasa kwanini msinge mpeleka kituoni, huoni kuwa mtaleta kesi hapa akifia eneo hili?”
“ndio tunaelewa”
Kupitia Redio upepo mlinzi aliweza kuwasiliana na jeshi la polisi usiku huo huo waliokua patro na defender, walifika eneo hilo na kumkuta Adrian akiwa amelala hasemi chochote,.
“hiri rijambazi rime kufa au”?
Aliuliza afande Chacha mmoja wao akiongea rafudhi ya kikurya
“sina uhakika sana kiongozi”
“embu turifanyie utaratibu turipereke hospitali kwanza”
Hapo ndipo walimchukua na kumpakiza ndani ya Deffender, bado alikua amepoteza fahamu zake hasemi kitu chochote, walimpeleka mpaka hospitali chini ya uangalizi maalumu wa jeshi la polisi.
**
“lakini Mpenzi Yule hakua mwizi”
“achana nae”
“kwani atakua amekufa au?”
“jaquee ingia ndani ya gari tuondoke”
“siendi popote, kwanini umefanya ivyo lakini?”
“kwani unataka kusema nini?”
“sio kusema nini, sio vizuri”
“au ni bwana ako?”
“tueshimiane Mathew, ushaniona mimi Malaya?”
“basi ingia ndani ya gari”
Maneno yaliyokua yakitoka kinywani mwa Jaqlin yalimaanisha japo kua hakumpenda Adrian ila aliamini kitendo kilicho tokea muda mfupi uliopita hakikuwa kizuri na kupelekea mpaka sherehe yake ya kuzaliwa kuharibia,
yeye alihesabia kuwa Mathew ndiyo chanzo cha mambo yote, moyoni alisikitika sana na kuumia mno huku akionesha hasira zake za waziwazi kwa Mathew mchumba wake,
ndani ya gari walinuniana mpaka alipo mfikisha mabibo hostel hakuna hata mmoja aliye msemesha mwenzake,
Alishuka na kushika pochi yake na kutembea haraka haraka akimuacha Mathew huku nyuma akiita jina lake lakini hakugeuka nyuma hata kidogo,
hiyo ndiyo ilikua sifa ya mwanamke huyo akinuna huwa hapendi kuongea tena, alifika mpaka kitandani na kujibwaga huku akiwa na mawazo tele kichwani mwake.
***
Maumivu aliyo yasikia hayakuweza kuelezeka kwa maelezo hata kidogo, alihisi kichwa chake kizito mwili mzima una muuma kupindukia, bado alikua haja yafumbua macho yake na kujaribu kuvuta kumbu kumbu nini kilitokea mpaka akawa kitandani tena mwenye maumivu,
taratibu kumbukumbu zilianza kumrejea , alikumbuka mara ya mwisho alikua na msichana Jaquee kisha mwanaume kutokea na kumtandika ngumi na baada ya hapo aliitiwa mwizi na watu kuanza kumshambulia na vitu vingi, kufikia hapo hakuweza kukumbuka kilichoendelea,
Taratibu aliya fumbua macho yake baada ya kusikia sauti ya msichana akilia kwa kwikwi karibu ya masikio yake, aliitambua sana sura ya msichana huyo alikua ni binamu yake Felista akilia kwa uchungu sana,
dalili zilionesha kuwa hata yeye aliguswa kwa hali aliyo muona nayo ndugu yake akiwa na bandeji kichwa kizima na sehemu za usoni akiwa ameumuka kama hamira,
Damu ni nzito kuliko maji! Bado alihisi uchungu na kutaka kujua ni kitu gani kilicho mfanya mpaka Adrian yupo katika hali mbaya kiasi hiko,
Alichomoka mpaka mapokezi na kuuliza , hapo ndipo alipo shangazwa baada ya kuambiwa kuwa aliletwa hospitalini hapo na defender ya polisi wakimshuku kuwa ni mwizi.
“hapana sio kweli, mimi nakataa”
Alikataa kata kata Fiona huku akitingisha kichwa chake
“ndivyo ivyo, kilicho tusaidia kupata namba yako, ni baaada ya kumkuta na wallet mfukoni mwake ina karatasi, na hiyo karatasi ndiyo ilikua na namba zako, kwani wewe ni nani yake?”
“mimi huyo ni kaka yangu kabisa, ndio maanaa nabis…..”
Askari aliyekuja mapokezi ndiye aliyekatisha mazungumzo na kutaka kujua hali ya Adrian inaendeleaje,
hakutaka kufunga kinywa chake taratibu alimsogelea askari aliyesimama kando yake na kuanza kumuhoji maswali.
“rire ni rijambazi razima riripe, rimeiba milioni moja,”
Aliongea uwongo askari sababu Alisha kula rushwa kutoka kwa Mathew ili amkandamize Adrian
“hapana, sio kweli, ilikuaje?”
“sina huo muda wa kukuereza ofkozi nina mambo mengi ya kufanya so prizi, embu nipishe nipite”
Aliongea kwa Nyodo afande chacha
Bado alikua na hali ya butwaa na kushindwa kuelewa nini akifanye hakutaka kuamini kuwa ni kweli Adrian aliiba kiasi hiko cha pesa sababu hakua na dhiki ya aina yoyote ile,
akili yake ilimtuma ni lazima tu yata kua ni mambo ya wanawake na wala sio kitu kingine,
“samahani namuulizia mgonjwa aliye letwa hapa usiku wa jana na defender ya polisi,”
Sauti hio ili mfanya Felista asimame na kugeuka nyuma, alimuona msichana wa makamo mweupe na kutega sikio lake vizuri.
“Yule waliyesema ni mwizi?”
Alihoji dada wa mapokezi
“nadhani ndio huyo,”
“Anaitwa Adrian?”
“ndio!ndio! ndio huyo huyo”
“nenda wodi namba 30j, ndio amelazwa hapo”
Hakupiga hata hatua nne alisimamishwa na Felista.
“dada samahani, unaenda kumuona Adrian?”
“ndio”
“ulijuaje kama kalazwa hapa?”
Aliuliza tena Felista
“jana tulikua wote, nilienda kituo cha polisi ndio waka niambia hapa ndipo walipo mleta jana”
“kwani ilikuaje dada?”
“ngoja nikuhadithie dada angu ukweli kutoka Moyoni huyu kaka alikua…”
Hapo ndipo Jaqlin alipoanza kuelezea kila kitu tangu alipo fika Adrian na Mathew kutokea na kusababisha ugomvi mkubwa kutokea uliosababisha mpaka Adrian akapigwa kipigo cha mbwa mwizi,
Walinyoosha mpaka chumba alicholazwa Adrian na kumkuta amelala, roho ya huruma ilimuingia Jaqlin na kuhisi maumivu, ni baada tu ya kumuona Adrian alivyo zungushiwa bandeji mwili mzima hasemi kitu,
dripu ya maji ikiwa mkono wa kulia, hakika hakustaili kipigo alicho pigwa, kwa hatua za taratibu alisogea mpaka pembeni yake huku akiwa ameibana mikono yake kwa mbele akisikitika hata yeye.
“Adrian naomba unisamehe”
Aliongea Jaqlin kwa sauti ya chini.
Sasa unaweza kusoma simulizi za mtunzi kway insta@storyzakway
ITAENDELEA
(kwa story nyingi za kusisimua tembelea hii link www.facebook.com/STORYZAKWAY)
[12/16, 10:10] +968 9121 7747: MCHACHUKO…..(29)
MTUNZI…EMMANUEL F. KWAY
Contact..+256756 322432
AGE…(18+)
ILIPOISHIA
dripu ya maji ikiwa mkono wa kulia, hakika hakustaili kipigo alicho pigwa, kwa hatua za taratibu alisogea mpaka pembeni yake huku akiwa ameibana mikono yake kwa mbele akisikitika hata yeye.
“Adrian naomba unisamehe”
Aliongea Jaqlin kwa sauti ya chini.
SONGA NAYO.
“uko wapi?”
“hospitali”
“ahaa!.. kwaio siku izi una kesha hospitali siku nzima, huna muda na mimi wala nini?”
“sio ivyo Methew”
“kumbe?”
“lakini…….”
“okay, hakuna tabu”
Wivu na hasira ndivyo vilimtesa sana Mathew ndani ya mtima wake mchumba wake alikua hawezi kupitisha siku bila ya kwenda hospitalini kumuangalia Adrian aliyekua hospitalini ana majeraha kila mahali,aliona jambo hilo lime kithiri sana,
“sasa subiri huyu demu hanijui vizuri”
Aliinua simu yake na kumtafuta rafiki yake mwanajeshi aliyeitwa Nyagogo .
“ndugu upo wapi?”
Aliuliza Mathew akiwa na simu sikioni
“nipo kazini”
“kuna kazi nataka uifanye”
“ipi hiyo?”
“njoo kwangu”
“poa nakuja”
Baada ya nusu saa mwanaume mrefu aliyevalia kombati za jeshi alikua amesimama mbele yake akitaka kujua nini alicho itiwa, hapo ndipo alipo ambiwa waongozane mpaka hospitali ya TMJ kwenda kumfanyia Fujo Adrian, alijua fika kuwa akitumia mwanajeshi huyo hakuna kitakacho haribika hata kidogo,
waliingia ndani ya gari na safari ya kwenda hospitalini kufanya fujo kuanza.
**
Ilikua furaha sana kwao kumuona Adrian ana weza kutembea na kuzunguka ndani ya wodi huku akifanya mazoezi,ilionesha hali ya matumaini kuwa sasa ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida kama hapo awali,
alishaweza kutabasamu na kuongea vizuri lakini bado alikua anatumia magongo yakimsaidia kutembea,
Brigedia Generali Said Adam Sangu mkuu wa majeshi nchini Tanzania akiwa na magwanda ya jeshi yaliyo chafuka nyota nyingi mabegani alikuwepo pia siku hiyo akiwa na walinzi wake wanajeshi pembeni,
alifunga safari kutoka visiwani Comoro mpaka Tanzania kuja kumuona rafiki yake kipenzi Adrian,
Wasanii mbali mbali kama Nassibu Abdul(diamond), Christian bella, na A.Y pia walikuwepo pembeni yake, Adrian muda wote alikua mwenye furaha sana.,
mpaka wakati huo Jaqlin hakuelewa Adrian ni mtu wa aina gani mpaka akajuana na watu wakubwa tofauti tena wengine mpaka viongozi wa serikalini, kweli alikua ni mtu wa watu.
“usiwe kama mwanamke, gangamala”
Alizungumza Brigedia Sangu
“mguu bado unaniuma”
“achia magongo hayo”
“siwezi!”
“Adrian lakini tangu juzi unatembea na magongo, msikilize kaka yako”
Alidakia Jaqlin akiwa pembeni, hapo ndipo Adrian alipo pata kidogo moyo na kuanza kuyaachia magongo taratibu na kuanza kutembea sasa taratibu sana.
Mathew tayari alipaki gari yake nje akiwa na Nyagogo pembeni,walishuka na kunyoosha mpaka ndani wodini na kilicho mshangaza Mathew ni baada ya kumuona Nyagogo akichapa mguu wake chini na kupiga saluti kuashiria kuwa aliyekua mbele yake ni mkuu wake wa kazi aliye mzidi vyeo vingi sana,
ni baada tu ya kuona nyota na kumtambua kuwa ni mkuu wa majeshi Tanzania na jasho kuanza kumtoka huku akijiuliza atajibu nini endapo akiulizwa ni kipi kilicho mleta.
“vipi kijana?”
Alihoji Brigedia Sangu
“hakuna kitu mkuu”
“nipo na kijana wangu namfanyisha mazoezi kidogo,kuna wapumbavu wame mpiga, sasa mimi nakutuma wewe hapo uende pale tegeta kamata vijana wote wa mtaani, ili wakaone cha mtema kuni”
“ndio mkuu”
“anza kazi sasa hivi tafuta kikosi,, uniletee hao watu, na nina mtaka huyo aliye muitia Mwizi, ndio ninae mtaka mimi haswa haswa!”
“ndio mkuu”
Maneno yaliyo tamkwa na Brigedia Sangu yalipenya kabisa kwenye masikio ya Mathew na kufanya haja ndogo ikaribie kumtoka na kuanza kusali kimoyo moyo walitizamana na Adrian kwa uso wenye kutia huruma sababu alijua nini maana ya kwenda kambini, alielewa mateso yake akifika huko.
**
Siku zilizidi kukatika huku masaa yakisogea kwa Adrian hali yake ilikua nzuri kabisa na kuruhusiwa kutoka hospitalini partson ndiye aliyekuja kumchukua na kumpeleka nyumbani kwake tegeta mwisho siku hiyo jioni,
Lakini bado akili yake ilikua kwa Jaqlin akimuwaza muda wote alisahau kipondo alichopigwa alijipa moyo sana kutokana na hali aliyo kua akimuoneshea hospitalini,
harakaharaka alichukua simu yake na kumtafuta hewani.
“nashukuru Adrian unaendelea vizuri”
Upande wa pili ulisikika baada ya kupokea simu
“nashukuru kwa kila kitu, lakini bado nilikua nahitaji kuzungumza nawewe”
“mmh…kwa sasa hivi nipo bize kidogo sitoweza”
“tafadhali”
“hapana Adrian”
Bado msichana huyo aliweka mgomo na kukataa katakata na kusimamia msimamo wake, Adrian alishashindwa kuelewa ni kitu gani akifanye, aliumia sana moyoni mwake, katika maisha yake hakuwahi kusumbuliwa na mwanamke kiasi hiko,
“kaka embu achana na huyo demu au mpaka ufe?”
Alisema Partson jr
“Partson, niangalie, acha nife tu lakini nimpate huyu mwanamke”
“ha ha ha ha ha, kweli umepatikana ndugu yangu, hapo umekamatika kakupa nini kwani?”
“hata nashindwa kuelewa, lakini lazima nimpate, sitokata tamaa mpaka nazeeka”
Maneno aliyotamka aliyamaanisha kutoka ndani ya mtima wake, aliwaza mambo mengi juu ya mwanamke huyo, japokua alishatukanwa matusi mengi lakini hiyo haikumfanya akate tamaa,
ndani ya moyo wake aliamini kuwa ipo siku atampata na watafunga ndoa japo kua kikwazo kilikua kimoja tu mwanaume aliyeitwa Mathew.
“tutapambana tu, nita tumia mbinu zote”
Aliwaza Adrian,ni kweli kabisa alishazama kihisia alikua kama chizi mapenzi, marafiki zake walijua juu ya swala la yeye kupenda walishangazwa, wengine walimcheka na kustaajabu sana sababu tu ya tabia yake ya kubadilisha wanawake kama nguo walijua ndio atakavyo mfanyia Jaqlin.
“ha ha ha ha Adrian haiwezekani hata kidogo, mimi ninakujua wewe, hata kwa Latifah ilikua ivyo ivyo, ukabadili mpaka dini ili umtoe bikra, haya yako wapi, sembuse huyo”
Alim-beza Rafiki yake siku hiyo asubuhi alivyokuja kumuona sababu hata yeye alishangazwa na habari hizo kutoka kwa Adrian.
“mimi sio Adrian aliye pita, mimi ni mwingine, ndio nakwambia Yule binti nampenda”
“ah wapi, hata uongee kitu gani, siwezi kuamini mimi nakujua, Tabia ni kama ngozi huwezi kubadili, embu achana na izo stori maana najua unani fanyia maigizo”
“nampenda jaqlin”
“acha kuchekesha umati”
Hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kuamini kuwa Adrian amebadilika, ilikua sio rahisi kubadilisha mawazo ya kila mtu aliye mjua.
Namba za wanawake wote alizifuta ndani ya simu yake, bado hakuchoka kumpigia simu kila siku mwanamke huyo akimjulia hali na mambo mengine,
Siku ziliyoyoma na sasa kurudi kibaruani, wafanya kazi wake walifurahishwa sana baada ya bosi wao kurudi kazini na kuendelea na kazi kama kawaida,
lakini kwa waliomfahamu walijua kua ana mabadiliko na kuna kitu kimempata sababu hakuonesha kuchangamka hata kidogo,
Alikua akitoka mapema kazini na kuondoka mpaka mabibo hostel akizidi kumsumbua jaquee, wakati mwingine alijua wenda ana kasoro lakini swala hilo hakutaka kulipa kipaumbele!.
“au nina kasoro gani jaqlin?”
Aliuliza Adrian kwa unyonge.
“wala hauna kasoro, wewe ni handsome, mtanashati una uwezo wa kuwa na mwanamke yoyote hapa duniani, lakini kama nilivyo kwambia siwezi kuwa na wewe”
“kwanini?”
“basi tu”
“niambie kwanini”
“nina boyfriend tayari”
“nipe nafasi hiyo, nikuoneshe jinsi gani mimi ninavyokupenda jaribu tu”
“hapana, nina mpenda nina mpenda sana”
Huo ndio ulikua ukweli wa mambo, hayo ndiyo majibu aliyokua akiambulia kila siku iendayo kwa Mungu, hata yeye mwenyewe binafsi alishindwa kuelewa na kumfata moja kwa moja Fetty ndugu yake mkubwa na Jaqlin aliamini wenda huyo ataweza kuwa ndiye msaada pekee kwake,
“jaribu kumuelezea ipo siku ataelewa”
Fetty alimjibu Adrian
“hapana miezi mitano sasa imeshakatika, tafadhali naomba umwambie ni jinsi gani navyo mpenda, nampenda sana,aniambie kitu gani nikifanye ili anikubalie mimi nitafanya”
Aliongea Adrian akitia huruma, hata Fetty ali muhurumia na kumuhaidi kuwa atajaribu kumuelezea rafiki yake juu ya jambo alilomwambia,
Siku hiyo hiyo Fetty alinyooosha mpaka kwa Jaqlin na kujaribu kumuelezea ni jinsi gani Adrian anavyoteseka juu yake.
“hapana, nimekwambia siwezi, unajua ni kitu gani kabisa kinacho nifanya nikatae umeshasahau au?”
“hapana sija sahau,”
“aya nenda kamwambie asijisumbue tena”
Maneno hayo tu machache ndiyo yaliyo mfanya Fetty aachane na jaqlin, na siku iliyo fuata kumtafuta Adrian ofisini kwake na kumuelezea kilichokua kinamfanya Jaqlin akatae kuwa nae kimapenzi.
“niambie tu, wewe niambie tu Fetty”
“sawa nakwambia usijali…….”
Je ni kitu gani hiko
Sasa unaweza kusoma simulizi za mtunzi kway insta @storyzakway
ITAENDELEA......
Post a Comment