Mchachuko sehemu ya 28
MCHACHUKO…..(26)
MTUNZI EMMANUEL F. KWAY
****
Chakula kili kua hakipiti tena mdomoni, picha ya mwanamke mrembo jaqlin aliye kiri kuwa ni mzuri ndiyo ilikua ndani ya medulla oblongata yake,
kitu kingine kilicho mshangaza ni juu ya msichana huyo kutompa nafasi hata ya kukaa na kuongea nae, hapo ndipo aliona kuwa ana faa sana na kuwa mke wake wa maisha, neno ndoa ndilo lilikua ndani ya akili yake na wala sio kitu kingine,
licha ya kuwaza hayo yote hakuelewa amfate kwa njia gani, aliweka kijiko cha kwanza kinywani cha pili lakini cha tatu hakuweza tena usiku huo,
Alitembea ,mpaka chumbani na kujimwagia maji na kujitupa kitandani, katika akili yake bado alizidi kumfikiria Jaqlin kila sekunde aliji geuza kila upande lakini usingizi haukuweza kumchukua mpaka kuna kucha, kweli alikamatika kabisa,
Asubuhi na mapema aliwasha gari mpaka Sinza kwa Felister alivyofika tu ili bidi amuelezee shida yake akiomba msaada kwa binamu yake huyo sababu njia zote alizo tumia kutupa mawe zilishindikana.
“eeeh eeh eeh Adrian usinieleze huo upuuzi, sitaki kusikia hata kidogo, ishia hapo hapo, sitaki kabisa”
Alifoka Felister baada ya kukumbuka kuwa alishawahi kubakwa kwa sababu tu ya kumuunganishia wanawake Adrian, bado alikua na kumbukumbu hizo kichwani mwake
“Felister huyu msichana nataka nimuoe”
“yaani hata useme nini, ndio nimemaliza ivyo”
“Felister nisikilize wangu!, nipo chini ya miguu yako”
“sitaki ADRIAN embu nenda tu, mengine nitakusaidia ila ukitaka wanawake tongoza mwenyewe”
Kila aliloliongea Felister alilimaanisha na kumfanya Adrian ashindwe kutengua msimamo aliokua nao mwanamke huyo.
**
“Jaqlinnn, Jaqliiiin, njoo njoo njooo”
“kuna nini?”
“wewe njoo, njoo nje”
“jamani Fettty niambie,mbona ivyo?”
“vaa nguo upesi twende”
Fetty alizidi kupiga kelele akimharakisha ndugu yake huyo aweze kuvaa haraka haraka kwani kuna jambo anataka akamuoneshe nje,
alimvuta haraka haraka na kushuka ngazi hata yeye ndani ya moyo wake alishindwa kuelewa ni nini kilimfanya ndugu yake amvute kiasi hiko,
alijua tu ni lazima kutakua kuna jambo la muhimu, walishuka ngazi haraka haraka lakini alisua kidogo, baada ya kutoka nje na kumuona Adrian yupo mbele ya gari AUDI huku nyuma ya gari hilo kuna gari aina ya MARCEDEZ BENZ mpya haina namba za usajili,
hakuelewa nini kinaendelea, alimgeukia Fetty na kumkata jicho kali.
“Jaqliin!”
Aliita Adrian na kutabasamu, aligeuka nyuma na kumuita dereva aliyekuwa anaendesha gari hiyo benz na kumuomba funguo za gari.
“hili ni gari lako kama zawadi tu, naomba upokee”
Alizungumza Adrian huku akining’iniza funguo hizo za gari na kusubiri jibu,
alishampenda sana mwanamke huyo ki ukweli, ndani ya moyo wake alikua hajiwezi kabisa, njia zote alizo tumia zili gonga mwamba hazikuzaa matunda na kuamua kumnunulia gari ndogo saloon ya kutembelea hapo chuoni.
Fetty aliye kua mbele alimkanyaga Jaqliin ili aweze kupokea zawadi hiyo ya gari kutoka kwa Adrian .
“No ahsante sana!”
Kauli hiyo ndogo kutoka kwa Jaqlin na kurudi hostel ili kata maini ya Adrian na kumfanya aishiwe pozi hakutegemea hata yeye,
wana funzi wa kike waliokua karibu walibaki kuyatoa macho yao, hata wao walimshangaa sana Jaqlin kwa kitendo alichokua kakifanya cha kukataa usafiri huo wa gari.
Chuoni ilishaanza kuwa stori kila msichana alimlaumu Jaqlin kila mtu alimzungumzia mwanamke huyo
“eti kakataa gari, atakuja kujuta”
“mmmh mwenzangu, shutuuuu!”
“au anajionaje,. Mimi nataka namba ya Yule mkaka ili nimuoneshe, yeye si kamkataa?”
“subiri namba nita ipata tu shoga angu ”
Hayo ndiyo yalikua mazungumzo kati ya Natu na rafiki yake hapo Hostel kwao, kila mtu alimtolea Udenda Adrian
**
Mapenzi tele alimuonesha Mathew aliamini kuwa huyo ndiye mwanaume wake pekee na ndiyo huyo alikua akimpa jeuri hapo chuoni na kufanya awakatae wana ume wote hapo chuoni na sehemu nyingine zote,
Alisha fika tayari Masaki kwenye jumba kubwa la Mathew, baada ya Jaqlin kugonga geti alifunguliwa na mlinzi na kumkuta Mathew akiwa seblen ametanda juu ya sofa.
Pale pale alimrukia na kuanza kunyonyana midomo yao.
“baby wait leo nataka nikupikie ufurahi,”
Alizungumza Jaqlin kisha kusimama kwenye sofa na kunyoosha mpaka jikoni, aliandaa kila kitu na kupika baada ya chakula kuiva alikitenga mezani tayari kwa kula.
Kabla ya kuanza kula simu Ya Mathew iliita ilionekana kuwa ni simu ya dharura kwake, simu ambayo ina muhitaji ofisini mara moja, baada ya kukata simu alimgeukia Jaqlin na kumuelezea kile alichoambiwa.
“lakini mpenzi si ungekula kwanza ,nime kupikia chakula ili ule, nime kuja kwa ajili yakoleo”
Aliongea jaquee kwa unyonge na sauti ya chini ya upole
“baby sikia, nakuja sasa hivi nisubiri sasa hivi”
Aliaga Mathew na kumpa busu kisha kuanza safari yake haraka haraka akitoka nje ya mlango.
“poa baby take care”
Aliitikia kwa unyonge sana ila hakutaka kuonesha hali yoyote ile ya kukasirika, hakuona haja ya kula chakula alilala juu ya sofa kwa muda mrefu sana, alivyo shtuka ilikua isha fika jioni saa moja, alitoka nje na kumuulizia mlinzi wa getini kama Mathew alisharudi.
“bado hajarudi dada angu”
Jibu hilo lilizidi kumkata maini na kumfanya achoke mwili mzima.
Sasa unaweza kusoma simulizi za mtunzi kway insta@storyzakway
ITAENDELEA......
Post a Comment