Header Ads

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto













 
Afya na uchumba na Kundi la damu







1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe


2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antigen.
kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen

Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A

Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B

Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB 

Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O


3. katika seli hiyo hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor 

3. a.      Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya +
mfano A+, B+, AB+ au O+





3. b.     Mtu ambaye cell zake nyekundu hazina hii antigen D, blood group yake inaandikwa na alama -
mfano A-, B-, AB- au O-


4. hii alama ya + au - inapatikana je?
4. a.     Baba hutoa Rh moja kwa mtoto, inaweza kuwa Rh+ au Rh- na mama hutoa Rh moja inaweza kuwa Rh+ au Rh-
4. b.     mtoto akizaliwa akiwa na Rh - manake baba alitoa Rh- na mama alitoa Rh -
4. c.   Mtoto akiwa Rh+ anaweza kuwa baba alitoa Rh+ na mama alitoa Rh+
mtoto mwenye Rh + anaweza kuwa alipata Rh- na Rh + ila hatuoandika Rh+Rh- kwa sababu Rh- ni kma haipo






5. UCHUMBA NA KUZAA /UJAUZITO

mvulana akiwa na damu yenye + ( mfano  A+, B+, AB+ au O+ )
Anaweza kuoana na msichana yeyote mwenye damu group yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) na watapata watoto bila tatizo lolote.


6. Mvulana akiwa na group mfano ( A+, B+, AB+ au O+) akioa msichana mwenye A-, B-, AB- au O-
6. a. Mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri, na ikitokea MSICHANA AMEJIFUNGULIA NYUMBANI au NJE YA HOSPITAL, ambako hakugundulika kwamba ana damu negative... Mtoto wa kwanza ataishi vizuri kabisa na afya nzuri. ila watoto wanaofata hawataweza kuishi au watakufa kabla hawajazaliwa kwa sababu,
6. b. Msichana mwenye negative blood group ( Rh-) yaani hana D antigen, alipojifungua mtoto wa kwanza mwili wake unakuwa sasa umeandaa kujikinga (antibodies kupambana na D antigen ( Rh +) kwa baadae
MTOTO WA PILI akitungwa mwili wa mama tayari una Antibodies dhidi ya Rh+ ( mtoto anazo hizi Rh+), hivyo matokeo yake ni kuwa seli nyekundu za mtoto zitashambuliwa na kufa.
Mtoto akibahatika kuzaliwa hai, atapoteza uhai muda sio mrefu kwa vile anakuwa hana seli nyekundu za kusambaza damu mwilini.






7. Endapo Msichana huyu alijifungulia MTOTO WA KWANZA HOSPITAL, madaktari wanakuwa wameshajua kwamba ana damu negative, hivyo wanasaidiana na mmewe kufanya maandalizi ya sindano yenye dawa ( SIITAJI HAPA )
alafu msichana akijifungua tuu MTOTO WA KWANZA anachomwa hiyo sindano
na akija kupata mimba baada atachomwa hiyo sindano wakati wa mimba na pindi anapojifungua.

No comments

Powered by Blogger.